Mkutano wa Umoja wa Afrika: Nchi 23 zaweka saini mkataba wa anga huru; Tanzania hatumo

Sijaziona Algeria, South Africa, Libya, Nigeria Morocco au wao pia hawajielewi?? Think twice
Nilisahau kuiweka South Africa WALISAINI,
Algeria.
Rais HAKUWEPO bali WAZIRI MKUU.Ambaye hawezi kusaini mikataba kama hiyo
Nigeria pia sikuwa nimeiweka WALISAINI
Morocco/ Mfalme wao HAKUWEZA kuhudhuria.
 
Soma historia ya Mashirika uliyoyataja.
1.Libya kuna nini? Si ni Vita tupu.
HAWANA shirika kawa sasa linalotambuliwa Kimataifa.
Morocco shirika li dogo. Namfalme

Aisee!
Mbona umeitaja Libya tu hizo nyingine nazo pia ni vita tu.. Na ukisema shirika sisi ndo kwanza tunaanza kufufua shirika, ndege zetu hata south haziendi Sasa ulitaka sujui tukasaini nn..
 
Kusaini mkataba wa Uhuru wa anga sio jambo la kukurupuka. Lazima pia tujue mipaka ya uhuru huo, la sivyo tutakuta maadui wametua Ngerengere na kutupigisha kwata .
Si jinsi wewe inavyofikiria. Haina maana kuwa basi inakuwa ni kama Dala dala. Bali usalamam wa nchi unabaki pale pale. Jamni hili ni rahisi sana kulielewa japo ni geni kwetu,
 
Nilisahau kuiweka South Africa WALISAINI,
Algeria.
Rais HAKUWEPO bali WAZIRI MKUU.Ambaye hawezi kusaini mikataba kama hiyo
Nigeria pia sikuwa nimeiweka WALISAINI
Morocco/ Mfalme wao HAKUWEZA kuhudhuria.
Basi hata sisi pia Raisi hakuweza kwenda, Mbona hao wengine unawatetea unashindwa kumtetea Raisi wako
 
Kwahiyo walioenda huko waligeuka watalii?
Si MARAIS wa kusaini mikataba na WAKUU wa nchi.
Protokali ni kuwa ni Rasi na Rais ama KIONGOZI wa nchi na Kiongozi wa nchi,
Si MTEULIWA wa kiongoziwa nchi anaweza kufanya hayo.
Unless ni mambo yasiyohitaji MARAIS anaweza kufanya hivyo.
 
NOD,
Mkuu,
Hao waliosaini na nchi zao hazina shirika la ndege au safari hata kumi za ndege kwa wiki pale AU Addis Ababa pana kitu kinaitwa "Corridor diplomacy and Briefcases diplomacy... Ni kitu kinaua a lot of resolutions and decisions of leaders and representatives in AU"
Hapo ndiyo pana shida sana kuwa na maamuzi sahihi kwa baadhi ya nchi na wawakirishi wake kwenye vikao hivyo na decision zake.

Mfano, apa hapa JF nikiuliza Ethiopia Airlines and KQ Kenya Air ways ni nani hass mmiliki wa hizo ndege utashangaa majibu yake.

Ukirusuhu free aviation market, utakuta nchi zote za nje ya Africa zinafuta majina yake halisi kisha wataandika KQ, RwandaAir, Ethiopian Airline, EgpyAir. Morocco Air n.k.n.k ili.kukwepa kodi huku shirika husika likila faida na nchi aliyebeba jina la kampuni yake kwa jina la Taifa.

(Hapo pana concepts zinatumika - trade deviation/ trade creation ila hapo kwenye udanganyifu pana angaliwa na concept ya rule of origin)
Kwa hiyo, mashirika mengi ya Africa yatakufa.

Pia, nchi nyingi kiusalama zitakuwa kwenye crisis kubwa kuhandle airspace espionage. Maana, ukileta ukali kwenye ndege za jirani watakuja na kukukoromea kuwa unavunja mkataba wa mkutano na kikao Namba fulani huko chenye resolutions hizi na hizi. Hivyo tutaburuzwa sana kiusalama.

Any way, hili jambo likitazamwa kirahisi ni sawa na kumtuma mtoto anayejifunza kutembea akakuletee tray iliyojaa mayai.

Serikali imechukua uamuzi sahihi kabisa, kwa kukataa hii proposal.

Duniani, biashara, uchumi na usalama wa nchi yoyote ile ndiyo mstakabali wake.
NOD, unaelewa fika kuwa tatizo letu kama NCHI tumejaa HOFU/PHOBIA. na hii haikuanza jana ni mAbaki ya serikali za kijamaa
Ambazo kila mtu alikuwa na wasiwasi na mwingine yaani HAWAAMNINIANI.

Mtindo huu wa Kimashariki ulikuwa nikuwa katika watu 10. Watu 5 ama8mni INFORMERS wa Security organs.
Watu waliishi kwa hofu sana.
Hamna anayem trust mwingine.

Wengine wetu tuliowahi kuwa nchi hizo ni kuwa ilikuwa VIGUMU MTU WA URUSI atoe TABASAMU hata baada ya USSR kuanguka na nchi kugawanyika vipande vipande .
Bado zile nchi zilizojitawala walikuwa na PHOBIA na kila mtu akiogopwa KWAMBA NI MWANA USALAMA wa taifa maana walikuwa WAKITESA WATU.

NDO HALI yetu na HANGOVER in the name of eti Kulinda usalama WA NCHI.DHIDI YA MAADUIWA NJE.
Maajabu na hangovers hizi za security fears of unknown sijui sitatutoka kweli?

Katika nchi yetu ilifikia Ofisa wa TISS anaogopwa kama yeye ni ka mungu badala ya kumwona kama ni mtumishi tu wa serikali akifanya majukumu yake.
Ndo maana ilifikia wengi hata KULIJIFANYA kuwamaofisa wa TISS kinyume cha sheria.
Ni LAZIMA hofu zisizo na maana TUZITUPILIE mbali.

Zibaki HOFU za kimamboleo kama TERRORISM. na mabo yanayofanana na hayo
Hapo nilazima kilamwananchiawe macho.
IKIFIKA katika mambo ya uchumi wa nchi yetu tusijifiche nyuma ya pazia la Imaginary Security threats at the expense of our economy.
Huo nimtazamo wangu.
 
Basi hata sisi pia Raisi hakuweza kwenda, Mbona hao wengine unawatetea unashindwa kumtetea Raisi wako
JPM wangu nampenda sana wa JMTZ.
Kumpenda haimaanishi kuwa kila kitu niseme Yes sir!
Kuna ka wazo ka kushauri.
Na wala simlaumu.

Natoa MAWAZO yangu jinsi NINAVYOELEWA hasa katika uhuru wa kujieleza.
Ili mradi HUFUNJI SHERIA.
Na si lazima akubaliane nami.

Mimi sipendi UNAFIKI eti nisifie tu for the sake of it.

Mahali anapohitaji kushauriwa kwa heshima na HEKIMA atashauriwa
.Maana Rais Magufuli HUSIKIA ushauri.
He is a good man.
Anaweza KUPINGA kama hajapata FULL information ama jambo halijamwingia sawa sawa.
Huo ni ubinadamu uliomo ndani ya kila mtu.
 
Mbona umeitaja Libya tu hizo nyingine nazo pia ni vita tu.. Na ukisema shirika sisi ndo kwanza tunaanza kufufua shirika, ndege zetu hata south haziendi Sasa ulitaka sujui tukasaini nn..
jarubu kujifahamisha utaelewa. Hata kama una ndege moja bado uko sawa tu.
 
Katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Nchi za Afrika AU uliokutana Addis Ababa chini ya Kiongozi wake mpya wa umoja huo Rais Paul Kagame, liweza kuwashawishi viongozi wa Kiafrika kukubali na katika huweka saini mkataba utakaojulikana kama Single African Aviation Market.

Yaani mkataba wa ANGA HURU ndege za nchi yetu zanaweza kwenda huko na zao kuja kwetu huku kukiwa na TOZO dogo sana la Ushuru miongoni mwa mambo mengine yaliyozingatiwa.
Swali kwa nini Tanzania HATUMO?


Swali linalonisumbua ni kuwa. Huku tunataka tuwe na ndege ZETU tufunguliwe ANGA za nchi zingine, huku Viongozi wetu husika HAWAHUDHURII mikutano kama hii na wanaohudhuria ni wa NGAZI za CHINI si wa kiwangocha MKUU wa NCHI {Heads of State}

Na hivyo kuwafanya mambo mengine kuwawia VIGUMU kuweka saini kwa niaba ya Rais katika mambo makubwa kama haya?.

Sasa kama tunazidi kuongeza ndege mpya, hizi ndege ni za KWENDA WAPI na ANGA lipi?
Wakati Rais Magufuli HAHUDHURII mikutano kama hii ambayo ni muhimu?

Najua lame excuses ni kuwa oh Rais aalikuwa na Majukumu mengine, kwani haya majukumu huwa hayaishagi. Si LAZIMA tunaaangalie PRIORITIES/Mambo MUHIMU kwanza?

Je ndoto zetu za kuwa na shirika KUBWA la lenye FAIDA litatimia kweli kama Tanzania tuna SKIP/Epuka mikutano itakayoyupatia TIJA KAMA HII?
Baadhi ya nchini kama ifuatavuyo:
1,Rwanda.
2,South Africa {sikuwa nimeiweka}
3.NIGERIA,
4.Sierra Leon

5.Benin
6.Botwsana
7.Bukina Faso,
8.Cape Verde,
9.Republic of Congo siyo {DRC},
10.Ivory Coast,
11.Egypt,
12.Ethiopia,
13.Gabon,
14.Ghana,
15.Guinea,
16 Kenya,
17.Liberia,
18.Mali,
19.Mozambique,
20.Togo
21.Zimbabwe
22.Angola.
23Tunis Air
Je TANZANIA kwa nini sisi HATUJIHUSISHI wala kuionyesha interest katika mambo kama hayo.
Hata kama ni Trade/Economic Protectionism policy naona tunatakuwa TUMEJITENGA sana.Inaweza ikawa conterproductive in long term.
Na si nzuri kwa uchumi wa nchi yetu.

Ni nani atatukaribisha kwenye ANGA LAKE kama sisi wenyewe HATUTAKI kuwakaribisha wengine?
Watanzani hatuna shukurani , tungeingia kwenye list tena ungekuja na story oooh pangaboi zitaenda nchi ya nani nani azitake. Ndo maana hatuendelei sababu ya kutoa only negative impact kwa serikali basi ungekuja na angalau agreement chache kwenye mkataba tungekuelewa. Kama tumewekwa pending mpaka tupate ndege za Masada marefu ndo tuingie? Najua utakuja na story nyingine ya kujidhalau wenzetu wana ndege nyingi sisi moja tu. Bora tuache.
Watanzania tubadilike tusipojikubari wenyewe Mani atatukubali? Mataifa mengine yanaendelea sababu watu wake wanamapenzi na nchi zako. Tubadilike.
 
Watanzani hatuna shukurani , tungeingia kwenye list tena ungekuja na story oooh pangaboi zitaenda nchi ya nani nani azitake. Ndo maana hatuendelei sababu ya kutoa only negative impact kwa serikali basi ungekuja na angalau agreement chache kwenye mkataba tungekuelewa. Kama tumewekwa pending mpaka tupate ndege za Masada marefu ndo tuingie? Najua utakuja na story nyingine ya kujidhalau wenzetu wana ndege nyingi sisi moja tu. Bora tuache.
Watanzania tubadilike tusipojikubari wenyewe Mani atatukubali? Mataifa mengine yanaendelea sababu watu wake wanamapenzi na nchi zako. Tubadilike.
Nsuumba.Ndo nafikiri una comment kuhusu.MaDA yangukwa mara tya kwanzaHatujakutana humu JF..

Kwanza kabisa naomba uondoe neno "NEGATIVE IMPACT" Halihusiani kabisa na MADA hii.
.. Nafikiri hukunielewa.
The negative impact aspect as per your perceptions ni kuwa what would be the consequences of our abstention from such a treaty?

Hata kama tuna ndege moja ama mbili. It does not negate the facts kwamba faida kubwa na pia kuwa NAULI za ndege zitapungua kwa kiasi kikubwa,

Unaweza kwenda wikendi Lagos na Urudi Jumapili. Na Jumatatu uko kazini.Ndo maana ULAYA wamefanikiwa. NAULI ni CHEAP sana.

Ndo maana mtu anatoka Nchi moja wikendi kwenda nchi yingine within ULAYA. Na anarudi.
Hiyo ni moja ya FAIDA ZAKE.

Mbali na hayo Biashara, Watalii, MAHOTELI yetu KUJAA, Hela za kigeni, AJIRA nk.
Usiangalie ki ufinyu angalia picha KUBWA..

By the way acha nikukosoe kidogo tu.
Questioning my Patriotism is nonsensical!!
It does not add up mkuu.

I am proud of being a Tanzanian/Najivunia kuwa Mtanzania./ Na najivunia Rais wangu Dr.JPM na nchi yangu.
Nevertheless that does not forbid me from expressing my VIEWS as I view things in different perspective.

Hilo ni kusema that does not make me a less Patriotic/AsiyeMzalendo. My Patriotism is unquestionable.
Na kama Mtanzania aliye na uhuru wa kutoa maoni natoa ili mradi mtu havunji sheria.
Huo ndo uzuri wa Tanzania yetu.

MADA hii si ya KULAUMU mtu yeyote yule ni MADA ya kuonyesha CONCERN na uwajibikaji.

Na kama neno concern kwako ni LAWAMA then sijui nitakusaidiaje?
As per my Patriotism/Uzalendo. No question about that.
Siwezi kuanza kujitapa humu JF,

Tafadhali soma faida zake katika mada hii hii.
Post#168 hapo juu.
Nafikiri utasaidika mkuu.
 
Unaweza kuwa upo sahihi. Wakati mwingine sisi tunaosema itakuwa vibaya inaweza kuwa woga tu.
Mkuu woga wetu umetugharimu miaka mingi na kukosa maendeleo .Sababu ya HOFU.
Inashangaza wakati mtu anauliza vipi ndege ikitua popopote usalama wa nchi yetu uko wapi?
Jamani kwani ndege ni Daladala?

Katika makubaliano hayo kila ndege hutambulika kwa CODES zake na ni ya nchi gani INAPOINGIA katika anga yetu.Hivyo bado tu salama.

Jeshi letu la ANGA lina ujuzi sana kujua hii ni ndege ya aina gani na yawapi. Na wamepewa FlIGHT PLAN ipi.
Jamani kukosa ufahanmu kwa wengine wetu unatuumiza.
Mwingine anaogopa oh! tutafanyiwa ujasusi. Na NANI na KWA NINI?

Wataalamu wetu wana ujuzi wa hali ya juu sana kujua nini kinaendelea ANGANI.
Jambo moja Watanzania tuache WOGA WOGA usio na maana.
Nakubaliana nawe kabisa mkuu.
 
Lyamber ,
Mkuu,
Siwezi mkuu kuvuka mipaka ya mambo ya kujadili.

Ila tambua kuwa , serikali na States organs zote hawakurupuka kutoa uamuzi kama huo kwa kupiga chini hiyo proposal.
Mkuu mbona vitu vingi tu serikali inakurupuka kama upo Tanzania sina hata haja ya kukuelezea maana mikurupuko yote umeiona kwenye TV na magazeti na impact yake pia umeiona either directly or indirectly
 
Sina utaalamu na mambo ya anga....ila Tanzania ni nchi kubwa ambayo haina mikakati ya kutawala siasa na uchumi wa nchi jirani...

Badala yake wale ambao ilibidi tuwaendeshe wao ndio wanajaribu kutuendesha.

Nchi yetu tumejisahau sana... badala ya kuanzisha changamoto za EAC kazi yetu ni kupangua changamoto za nchi ndogo ambazo tumezilea wenyewe.

Hii unaonyesha tumejisahau au hatujui dira yetu ni ipi kwenye EAC, Africa na Dunia kwa ujumla.

Niliwahi soma sehemu kuwa Rwanda na Burundi wanatambulika kwa Anga la Tanzania...

Wajuvi mtujuze.

Kwani lazima uandike?
Nchi kubwa kuliko Misri, Ethiopia, South Africa etc?
 
Jawabu ni kwamba tunaendelea kuzama tu kidiplomasia na mahusiano. Kwa akili za viongozi tulionao, kila kitu ni tishio. Na suluhu ya haraka ya mtu asiyekuwa na fikra ni kusema no. Kwa sababu anaogopa hata kivuli chake.
hivyo hivyo hatumo katika nchi za Soko la COMESA ingawaje lina faida kubwa za kiuchumi na tuko hatuko Jumuiya ya Afrika Mashariki.....yote ni kukimbia kivuli chetu.
Kwa ufupi Tanzania imetandawa na ujinga na woga.
 
Weeweumeonaa Tanzania pekee Africa ZIKO ngapi..shidayako kumwona raisi AMA.kiongozi mikutanoni??nashaka NA...
 
Mkuu mbona vitu vingi tu serikali inakurupuka kama upo Tanzania sina hata haja ya kukuelezea maana mikurupuko yote umeiona kwenye TV na magazeti na impact yake pia umeiona either directly or indirectly
Nakuelewa fika.Hasa hutokea kunapokosekana wider consultation na ushauri kuzingatiwa.
Lakini katika hili, maomba usome FAIDA zake katika katika uzi huu huhu post# 168.

Katila hili tumekosea shabaha. Huenda tukajirudi.
Maana nakuelwwa sana. Kama huu msemo usemao:
mtu ALIYEJERUHIWA na Nyati akiona Ng'ombe HUKIMBIA.
Akifikiri ni Nyati pia.
 
Back
Top Bottom