Mkutano wa lala salama wa CHADEMA uko Igunga wafunika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa lala salama wa CHADEMA uko Igunga wafunika

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Omutwale, Oct 1, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Natuma salamu za pongezi kwa hatua na mafanikio yaliyofikiwa na Chama Cha CHADEMA katika uchaguzi wa Igunga. Hizi ni salamu za awali kwa yale matukio na mitihani mliyokwisha-ishinda kuelekea kilele cha ushindi hapo kesho.

  Kwa ukumbusho; CDM tayari mmeshinda propaganda ya kummwagia kijana wa ccm tindikali, kuchoma nyumba na ofisi za ccm na makada wao, kuingiza makomandoo kutoka nje ya nchi na mengine mengi. Na pia mmevuka mstari kwa kuweza kueleweka na kukubalika kwa kiasi kikubwa vijijini tofauti na chaguzi zilizopita. Mjini tayari mmekwishashinda.

  Ushindi wenu wa kesho una maana kubwa sana kwa Taifa hili. Maana zaidi ya ile ionekanayo machoni na labda pia itakayojulikana na wanaochukulia mambo kijuujuu. Ushindi wenu utamaanisha makubwa yafuatayo:
  • Kwamba Watanzania hawagawanyiki tena kwa misingi ya UDINI. Watanzania lao ni moja; siasa za kweli kutafuta haki na maendeleo
  • Kuwa Waumini wanajua misingi imara ya dini zao na hawakotayari kumuunga mkono mtu katika ukengeufu wake eti tu kwa sababu ni wa dini yao
  • Kifo cha mpango wa ccm kujivua Magamba (EL na AC watapona).
  • Dhana ya kwamba vyama vya upinzani vya kisanii na vile vya upinzani9 wa kweli visiposhirikiana basi basi ccm ndo inapata mwanya wa ushindi
  • Nguvu ya Dola kwa maana ya usalama wa Taifa na Polisi katika kung’ang’aniza matopkeo ya uchaguzi imefika kikomo.
  • Utamaanisha sasa, si kwamba mko tayari tu, bali ccm haiwezi tena kuwazuia kuingia Ikuli mwaka 2015
  Nimefurahishwa sana na intelijensia yenu CDM. Nimecheka sana kusikia kuwa ccm wamelishwa kasa nyingi na kuingia mitego yenu. Miongoni mwake ni huu wa kuwahonga mawakala feki 90 wa CHADEMA na kasha nyinyi kuleta 400 mliokuwa mmewaandaa vema toka awali wakitokea nje ya mkoa. Ccm walikwishapumua na kujua kazi imekwisha. Mpango huu umetumia muda na rasilimali nyingi kuuandaa na kuanza kuutekeleza. Ikumbukwe, mpango huu una-muunganisho na uingizwaji wa boksi na karatasi za kura ambazo tayari zilikuwa kwa Mkuu wa Wilaya. Hivyo kuuvuluga kwenu kumewavunja nguvu sana ccm maana hawategemei ushindi kwa njia ya kura bali mbinu ovu. Nimejulishwa mpalanganyiko ndani ya timu inayoongozwa na Januari akilalamika kuvuja kwa kila mikakati hata kabla ya kutoka nje ya vikao. Imefikia mahala wanahisi INVISIBLE ni mjumbe katika vikao vyao!

  Ila sijapendezwa na dau mnalotoa CDM kwa watu wa Usalama wa Taifa wanaowapigia simu na kuwapa taarifa za uhakika. Wakati nina taarifa za uhakika ccm kutumia zaidi ya bilioni 4 katika uchaguzi huu lazima pia tujue nanyi mmetumia ngapi na zinafadhiriuwa na nani? Za ccm tunafahamu ni za ufisadi na zinatolewa na magamba, zenu ninyi mnapewa na nani na zinatoka wapi?

  Kwa kila hali na kila jinsi hakuna wa kuzuia ushindi wenu hapo kesho. Hata kutangazwa kwenu hakuna wa kukuzuia. CCM tayari wanakiri kwa vitendo kulipoteza Jimbo la Igunga. Kila walifanyalo linaonyesha kuchanganyikiwa na kuishiwa kabisa mbinu. Wamebaki kulaumiana tu.
  Hapo kesho nitarudi hapa kuja kuweapongeza rasmi CHADEMA maana Ushindi Wenu ni Ushindi Sote Watanzania.

  Mungu aendelee kuwa nanyi katika kumalizia ngwe ya mwisho, Amen

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  Kama umati huu wote wanasifa za kupiga kura na wakapiga kura kesho basi jimbo hili chadema italichukua......
   
 2. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  hakika inatia faraja....tunausubiri ushindi kwa hamu sana..nguvu ya umma haiwezi shindwa kamwe!
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  May god be with us !
   
 4. M

  Msharika JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  May God stand for rightiousness
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  let Jah be blessed!
   
 6. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema wakishinda igunga nakunywa tindikali
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na mumeo salamu kama hizi umeisha mpa ?
   
 8. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Join Date : 27th September 2011
  Posts : 5

  Rep Power : 0
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Salam zimefika
   
 10. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  thanks for infor
   
 11. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Tutolee upupu wako hapa nenda kawaeleze vilaza wenzio huko.
   
 12. K

  Kinte Member

  #12
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mtu kama wewe ni bora unywe hiyo tindikali upotee, na majivu ya mifupa yako kabisa, huna faida kwa kizazi hiki wala kijacho!!
   
 13. N

  NANKY Member

  #13
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaman wengine mbona unatukana tu tumia hoja zenye maana kusaidia taifa
   
 14. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  weeeeeeeeeee!nina faida kubwa kwa nchi hii na chama changu cha mapinduzi labda kwenu nyie magwanda na hamshindi igunga!
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sumu aina gani?
   
 16. M

  Mwera JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema ikishinda igunga nitaihama tanzania.
   
 17. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa waraka wa CDM wa December 2010, 25% ya ruzuku hubaki makao makuu kwa ajili ya kukuza chama ikiwa ni pamoja na shughuli kama hizi. Hata hivyo, Tume ya uchaguzi inatoa fedha kwa ajili ya chaguzi.

  Quality
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Ninayo H2S04 98%, nitafute kesho jioni.
   
 19. Jidulamabambase

  Jidulamabambase Member

  #19
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna Mawaziri wa kutosha kule! Viongozi wa kuaminiwa (Wapiganaji wapya), Mapolisi na usalama wa taifa! Bado CHADEMA imekaba! CHADEMA ikishinda Igunga ni wazi CCM haipo 2015!
   
 20. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anza kuhama haraka. Ninyi ndo mlisemaa CHADEMA haiwezi kushinda jimbo hata moja. majimbo 25 yamechukuliwa, bado mpo!!
   
Loading...