( Mkutano wa FOCAC Dakar) Fursa Mpya za Ushirikiano kati ya China na Afrika (2): uchumi wa kidigitali watazamiwa kuwa sekta mpya ya kuvutia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
265
250
1638240256465.png


Kampuni ya China Telecom inasaidia utoaji elimu kwenye mtandao wa internet kupitia mikonga ya mawasiliano iliyojenga barani Afrika
Hivi sasa, uchumi wa kidigitali umetajwa na nchi nyingi za Afrika kama sekta muhimu ya kufufua uchumi, kutafuta maendeleo ya ubunifu na kuboresha maisha ya watu. Kwa mujibu wa Ripoti ya Uchumi wa Kidigitali wa Afrika kwa Mwaka 2020 iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IFC la Benki ya Dunia na kampuni ya Google, hadi kufikia mwaka 2025, thamani ya uchumi wa kidigitali barani Afrika inatarajiwa kufikia dola za kimarekani bilioni 180, na kuchukua asilimia 5.2 ya pato la jumla la bara hilo. Hata hivyo Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD imesema nchi za Afrika zimehamasisha uvumbuzi, uchumi wa kidigitali unakua kwa kasi, lakini kutokuwa na mpango kabambe wa kimkakati kumekwamisha maendeleo ya uchumi wa kidigitali.Takwimu zimeonesha kuwa mwaka 2019, uchumi wa kidigitali ulichukua asilimia 36.2 ya pato la taifa la China, na kuchangia asilimia 67.7 ya ongezeko la pato hilo. China imefanikiwa kuwezesha teknolojia mpya kuhudumia ukuaji wa uchumi, jambo ambalo linastahiki kuigwa na nchi za Afrika. Kwenye ufunguzi wa mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Dakar, Senegal, rais Xi Jinping wa China amesema China na Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchumi wa kidigitali na kujenga miradi ya uvumbuzi wa kidigitali.Kwa miaka mingi, China imeisaidia Afrika kupata maendeleo makubwa katika miundombinu ya digitali. Kwa mfano, mradi wa mtandao huru wa biashara wa kwanza wa 5G barani Afrika uliojengwa kwa pamoja na makampuni ya China na Afrika Kusini ulikamilika mwaka jana; Kituo cha Data cha taifa cha Senegal kilichojengwa kwa msaada wa China kitazinduliwa mwaka huu; kampuni ya mawasiliano ya simu ya China, China Telecom ambayo imezindua mikonga 14 ya chini ya bahari barani Afrika na kutoa huduma za mtandao wa internet karibu kila pembe ya Afrika kupitia kushirikiana na kampuni za mawasiliano za nchi za huko, itawekeza zaidi kwenye huduma za mawasiliano ya simu baada ya kupata wawekezaji kama Mfuko wa Maendeleo wa China na Afrika; na kongamano la ushirikiano wa Mfumo wa Uongozaji Safari wa Beidou kati ya China na Afrika lililofanyika Beijing mwezi uliopita limetoa msaada wa programu muhimu za ubunifu kwa ushirikiano wa kidigitali kati ya China na Afrika. Katika miaka mitatu ijayo, China itaisaidia Afrika kutekeleza miradi 10 ya uchumi wa kidigitali, kikiwemo kituo cha ushirikiano wa matumizi ya satilaiti ya kutambua kutoka mbali.

1638240302792.png

Mkurugenzi wa ofisi ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wu Peng akizindua “Msimu wa Kuhimiza Biashara ya Bidhaa za Afrika kwenye Mtandao wa Internet”


Mbali na miundombinu, biashara ya mtandao wa Internet pia imekuwa chombo muhimu cha kufufua uchumi wa nchi za Afrika. Mwezi Septemba mwaka huu, siku ya biashara ya moja kwa moja kwenye mtandao wa internet ilifanyika kwenye kituo cha kuandaa biashara ya moja kwa moja kwenye mtandao wa internet kati ya China na Afrika mjini Changsha, China. Ndani ya siku tatu, shughuli 55 za kuuza bidhaa za Afrika zilifanyika kwa njia ya moja kwenye mtandao wa internet, zikitazamwa na watu milioni 23.27, na kufikia biashara yenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 4. Imefahamika kuwa katika mwaka mmoja uliopita tangu kituo hicho kizinduliwe, matangazo 4,200 ya moja kwa moja ya bidhaa za Afrika yamefanyika na thamani ya biashara kufikia dola milioni 86. Kahawa ya Ethiopia, ufuta wa Tanzania, pilipili kavu ya Rwanda, pilipili manga nyeupe ya Cameroon, mvinyo wa Afrika Kusini na bidhaa nyingine bora za kilimo za Afrika zimeingia kwenye nyumba za wachina wa kawaida kupitia biashara ya mtandao wa internet. Katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya bidhaa zilizoagizwa na China kutoka Afrika iliongezeka kwa asilimia 46.3 na kufikia dola za kimarekani bilioni 59.3, kiasi ambacho ni kikubwa kuliko kiwango cha ongezeko la biashara ya jumla kati ya pande hizo mbili. Katika siku za baadaye, China itashirikiana na Afrika kupanua biashara ya mtandaoni, kuandaa sikukuu za kuuza bidhaa za Afrika mtandaoni na shughuli za kutangaza utalii, na kufanya thamani ya jumla ya bidhaa zitakazoagizwa na China kutoka Afrika ifikie dola za kimarekani bilioni 300 katika miaka mitatu ijayo.Uchumi wa kidigitali umekuwa moja ya sekta zenye uhai na nguvu ambayo haijatumiwa ipasavyo katika uchumi wa Afrika, na utatoa fursa kwa Afrika “kuwapiku wengine kiuchumi”. Kwa kutegemea Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” BRI, China na Afrika zitatumia fursa zilizopo kujenga kwa pamoja njia ya digitali, na kufungua ukurasa mpya wa jumuiya ya mtandao wa internet yenye hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili.
 

Miki123

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
282
500
Mwenye hii ID bila Shaka ni mchina au kibaraka WA wachina kila nyuzi ni China. Wezi kama wazungu Tu.
 

castieltsar

JF-Expert Member
Jun 3, 2016
1,234
2,000
Mwenye hii ID bila Shaka ni mchina au kibaraka WA wachina kila nyuzi ni China. Wezi kama wazungu Tu.
Ile nadharia ya kwamba Kila maskini akimwona tajiri anamwita mwizi .....anyway Africa tumelala/tumepoa Sana hatuna malengo yeyote Yale na bara letu .....ivi Kuna nchii duniani Sasa hivi inaweza ikimbia China kweli?Kwanza angalau yeye ndo kaichangamsha Africa kidogo Ila ndo ivyo tunawaza pafupi Sana
 

Miki123

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
282
500
Ile nadharia ya kwamba Kila maskini akimwona tajiri anamwita mwizi .....anyway Africa tumelala/tumepoa Sana hatuna malengo yeyote Yale na bara letu .....ivi Kuna nchii duniani Sasa hivi inaweza ikimbia China kweli?Kwanza angalau yeye ndo kaichangamsha Africa kidogo Ila ndo ivyo tunawaza pafupi Sana
Kaichangamshi au anainyonya sababu ya kuzubaa Kwa viongozi wapuuzi WA afrika mfano wa Zambia na DRC. Migodi ya Cobalt ya Congo kipindi inamilikiwa na wamerikani maisha ya wafanyakazi na watu wanaozunguka hiyo migodi ilikuwa Bora kuliko hivi sasa ambapo wachina ndio wanaimiliki na kupiga pesa nyingi na hawazingatii Sheria za mazingira.

Kiuharisia kila nchi ina maslahi binafsi kama nchi itashindwa kung'amua vizuri maslahi yake mfano wa nchi za kiafrika, wachina wataendelea kujichukulia Mali za Africa kila uchao.

Mikataba ya WA China ni ya kiraghai inayonufaisha upande mmoja zaidi, fuatilia Exim Bank of China na China development Bank pamoja na Sera zao za export promotion, utaelewa namaanisha nini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom