Mkutano wa CUF wa Maalim Seif wavamiwa na watu wenye "mask". Wanachama na waandishi wapata kipigo

"Akizungumza leo Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya amesema mlinzi huyo na wenzake walikwenda Mabibo kwa ajili ya kufanya doria" Chanzo: Mwananchi

Hivi inamaanisha CUF ya Lipumba ina mamlaka ya kipolisi ya kufanya doria? Au ndio maana wanapiga watu na hatua hazichukuliwi kwa sababu wanatambulika na vyombo husika vya kiusalama? (kauli hiyo ya msemaji huyo ikipita bila wahusika kuchukua hatua stahiki basi tena!!!)
Nimemsikia huyo jamaa tena bila woga anasema waliwatuma kufanya doria!ila walichokipata ndo dawa ila kwa bahati mbaya wananchi wenye hasira hawakuwa na hasira!
 
760651a9370b6f416686c409ce858d23.jpg

Hizi ndio taarifa nilizo zipata.
 
Ni hivyo. Sisi watanzania hatupaswi kuisema vibaya serekali yetu. Sababu ni kwamba, haisaidii bali itakupa kidonda cha moyo ufe mapema kabla ya wakati. Ipende tu na umuombee rais kama anavyosema. Serekali hii ipo na itaendelea kuwepo hadi siku tutakapo funguka akili zetu tufanye mapinduzi kwa kura sio kula. Nadhani utanielewa. Hakika narudia tena; Kuisema vibaya serekali hii kutakuletea ugonjwa wa moyo ufe mapema kabla ya wakati. Ipende tu ukijua siku hazigandi
Unafiki ni tabia ya mtu.
 
Nimemsikia huyo jamaa tena bila woga anasema waliwatuma kufanya doria!ila walichokipata ndo dawa ila kwa bahati mbaya wananchi wenye hasira hawakuwa na hasira!
Mkuu, sijui tunapelekwa wapi ikiwa vitendo vya kijambazi vinafanywa na watoto wapendwa wa wenye kumiliki utawala. Je usalama wetu uko wapi? Nani tumuamini?
 
Duh tumefikia huku
View attachment 499475 View attachment 499474

UVAMIZI : Inasemekana kwamba watu waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif ni kutoka upande unaomuunga mkono Prof Lipumba.

Walipovamia mkutano huo waliwashambulia wazungumzaji na baadhi ya waandishi habari waliokuwepo ndani ya chumba cha Mkutano. Pia waliwazuia kutoka nje hadi pale wananchi wa eneo hilo walipofahamu kinachoendelea na kuanza kupiga kelele.
Wavamizi walikimbia lakini mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa mmoja ( anayeonekana pichani ) wao amekamatwa na kushambuliwa na Wananchi wa eneo hilo.

Hii ndiyo shida ya kuwa na sheria mbili. Moja ya watu wa kawaida na moja watu wanaokingwa na serikali. Pamoja na mambo mazuri Rais Magufuli anayoyafanya, kosa kubwa la kuchaguwa sheria, double standard, kuwaadhibu watu na wengine kuwaacha kwa kosa like lile, hajisaidii. Inaifanya kazi yake iwe ngumu zaidi, na nchi kuharibu jina. Imekuwa ni kawaida watu kuvamia, na kuvunja sheria bila ya kuogopa, Sasa watu wameanza kuchukuwa sheria mikononi wao bila ya kujali sheria. Kama Rais Magufuli angemchukulia hatuwa Mkuu wa Mkowa kwa kuvamia clouds TV, raia wengine wangeogopa, lakini Sasa ina kuwa mbona Makonda kavamia na Hakuna kilichotokea. Nchi yeyote kukiwa na double standard, heshima ya kuheshimu sheria inapunguwa sana, Na hii ni hatari kwa biashara, wawekezaji na ni jina haya kwa Tanzania.
 
HICHO NDICHO KINAJENGWA KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA!!!!
 
Ni hivyo. Sisi watanzania hatupaswi kuisema vibaya serekali yetu. Sababu ni kwamba, haisaidii bali itakupa kidonda cha moyo ufe mapema kabla ya wakati. Ipende tu na umuombee rais kama anavyosema. Serekali hii ipo na itaendelea kuwepo hadi siku tutakapo funguka akili zetu tufanye mapinduzi kwa kura sio kula. Nadhani utanielewa. Hakika narudia tena; Kuisema vibaya serekali hii kutakuletea ugonjwa wa moyo ufe mapema kabla ya wakati. Ipende tu ukijua siku hazigandi
Naomba kutofautiana kidogo na wewe Mkuu...

Kutoisema vibaya wakati inafanya vibaya, ndiyo inaweza kupelekea tukapata ugonjwa wa moyo. Kwasababu sumu ya chuki na ghadhabu itakuwa inamwagikia ndani ya mwili...

Kuisema kunasaidia kutoa sumu isidhuru miili yetu wakati tukisubiri muda wa KUIKATAA kidemokrasia.

Lakini pia ni kwa kuisema kwetu kunaweza kuwasaidia wakafanya vema. Kama tulivyowasema kwa uamuzi wao wa kukurupuka kwa suala la madaktari wa Kenya.

Suala la kumuombea Rais kwa sababu ameomba tumuombee, huo kwa hakika ni upuuzi lakini pia ni kumdhihaki MUNGU. Haifai..

Mfalme Suleiman alipewa utawala ambao huyu Mtawala wetu hajaufikia hata kwa 0.0001%. Lakini hata MARA moja hakuwataka watu wake wamuombee... Lakini alikuwa Karine sana na MUNGU na aliridhiwa.. Huyu wetu vipi ???
 
....karibu sana na Mungu... "Not karine".
 
ae66604b2a6da98fd3328f6fb9a5f1d9.jpg

Huyu mtu alikamatwa baada ya kuvamia mkutano wa CUF wa ndani akiwa na wenzake tena wakiwa na bastola mchana kweupe.
Walipiga watu wakiwemo waandishi wa habari na viongozi wa CUF, ila polisi walishaanza kuonyesha namna fulani ya ajabu kuhusu kesi hiyo ya huyo jamaa na wenzake.
Jee hiyo kesi bado ipo au ilishajifia? Na kama ilijifia hiyo sio dalili za wazi kuwa watu watumiao silaha ni watu wanaotumwa na polisi au ni watu wao? Imani na jeshi hilo itatoka wapi kama ni hivyo?
 
Back
Top Bottom