Mkutano wa CUF wa Maalim Seif wavamiwa na watu wenye "mask". Wanachama na waandishi wapata kipigo

Are you sayong rais wako mtukufu ndiyo alivaa kinonja kuvuruga mkutano? Mbona unaruka mbali kiasi hivyo? Wache polisi wapeleleze utakuta ni vijaba wa kijiweni wamepewa mbau mbau kwenda kufanya fujo, wamelipwa na blue guards wa Bara waliotemwa huko Zenj
Baraka zinatoka kwake TISS hawawezi fanya chochote bila baraka WA mzee broken fent ford au sizonje au komwe Kama Leo kikao cha Mtulia kilichopigwa marufuku..mungu niweke niione nchi ya ahadi inshallah...
 

Kama ni kweli matukio haya yamefanywa na mtu ambas watanzania wengi walimuamini na kutaka kumpa nchi ili atuondolee umaskini kwa professa wake sasa naona kama chai kaitia chumvi
na amejiharibia Kwa watanzania walomuheshim

LIPUMBA NI KUWADI..
 
hizi ni figisu tu ili chama kionekane kimemwaga sana damu matokeo yake chama kitakuja kufutwa na msajili mkuu wa vyama vya siasa Tanzania then upinzani unapungua mwisho wa siku uchaguzi kipo chama kimoja hata ikiwa kura 1 bhado knapita
 
Waswahili wanasema "USIPOZIBA UFA, UTAJENGA UKUTA!"
Naona kwa tukio hili la bastola kuoneshwa kila siku na kutochukuliwa hatua wahusika, Wananchi watawaonesha wanaozimiliki na mabwana zao ni wapi bastola hizo zagavu zilipaswa kutunzwa wapi. Tunapowalea majambazi kama hao Mungiki je wakishakubuhu hatujiulizi watakuwa nani?
 
Kwani wanasiasa wengine wanajitofautishaje na Lipumba?

Tulioko nje ya siasa tunaona wote tabia zenu zipo hivyo hakuna jipya.

tofauti ni aina ya vituko mnavyofanya.


Kama ni kweli matukio haya yamefanywa na mtu ambas watanzania wengi walimuamini na kutaka kumpa nchi ili atuondolee umaskini kwa professa wake sasa naona kama chai kaitia chumvi
na amejiharibia Kwa watanzania walomuheshim
 
Wote tunajua kuna mgogoro. Ni wote pia tunajua kuwa Rais ni mkubwa kuliko waziri na Meja mkubwa kuliko Luteni. Je, hujui kuwa Mwenyekiti (Lipumba) atakuwa mkubwa kuliko Katibu (wake)? Imegawanyika, akili ya kawaida inatutuma tumfuate Mwenyekiti, si Katibu; tumfuate Captain, si winga. Hayo ni 9 la 10 ni kuwa hapa tuna mwamuzi anaitwa Msajili. Msajili yuko upande gani ebu tuambie. WM
Kama ni mweyekiti basi tutamfuata Mtatiro si Lipumba huyu jamaa si mweyekiti wa Cuf bali ni mvurugaji kupitia ofisi hiyo uliyoitaja hapo juu na ndo maana imefika mahali nae kakwama na kesi ipo mahakamani.
 
Yawezekana ni sahihi sababu yeye alimtaka wakae wapate suluhu lakini cha kustaajabisha yeye seif muislam anajuwa sheria ya kislam kwa nini akatae kukaa na kupata suluhu... yaonyesha wazi kuwa seif Anakiburi na kiburi ni sifa ya Mungu na si mwanadamu...
Asante sana mkuu, yule bwana anaejiita mwenyekiti aliacha mwenyewe kwa ridhaa yake tena wakati wa uchaguzi sasa leo uchaguzi umeisha unakuja kusema kuwa yeye bado ni mw/kiti, wa wapi?. Kama ni mwenyekiti wa cuf basi ni Mtatiro si vinginevo Lipumba ni mvurugaji tu na kadri kunavyokucha heshima inazidi kushuka kulingana na matendo yake na hapa ndo tunathibitisha kwamba kumbe unaweza ukawa msomi na una akili nyingi sana laini busara huna.
 
Watu 8 waliovalia ninja wamevamia mkutano wa chama cha CUF na kujeruhi baadhi ya waandishi wa habari na wafuasi wa chama hicho Mabibo Dar Es Salaam
View attachment 499461

Kuna hiyo picha niliyoambatanisha hapo inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huyo aliyezungushiwa duara ndiye aliyepigwa siku ya tukio. Kuna ukweli wowote? Yeyote anayemfahamu huyo atuthibitishie?


Wakuu kulikuwa na mkutano wa CUF ya upande wa Maalim Seif,ulipangwa kufanyika katika hotel ya Vina-Mabibo.

Ghafla wakavamia watu waliovaa mask usoni na kuanza kutembeza kichapo kwa waandishi wa habari na wanachama waliokuwepo eneo la tukio.

Wavamizi hao walikuwa na mapanga,marungu na mmoja akiwa na bastora.

Hali iliyosababisha mkutano kusambaratika na watu kukimbia hovyo,nina mtu katika eneo la tukio,ananipa habari kuwa kichapo kimetokea na baadhi ya watu kujeruhiwa.

Picha hii juu ni mmoja wa wavamizi,ambaye wakati anataka kutoroka,wananchi walimdhibiti na kumpa kichapo.
More News to come.....

MUNGIKI WA LIPUMBA WAVAMIA “PRESS” YA CUF, WAPIGA WAANDISHI WA HABARI NA VIONGOZI, MUNGIKI MMOJA AJERUHIWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

(Imetolewa na Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front - CUF) 22 April 2017.

Ndugu zangu, Leo, Jumamosi, 22 Aprili 2017, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Juma Mkumbi (ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa) alikuwa anazungumza na vyombo vya habari katika Hotel ya VINA iliyoko Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni (jijini Dar Es Salaam), juu ya masuala mbalimbali yanayohusu wilaya yake.

Akiwa anaelekea kumaliza mazungumzo na wanahabari, ghafla, watu waliovalia KININJA/VINYAGO walipaki magari mawili karibu na hoteli na kuvamia ukumbi wa PRESS ya Mhe. Juma Mkumbi.

Wavamizi hao maarufu kama MUNGIKI, (ambao hutumwa na Prof. Lipumba) leo wakiwa na BASTOLA MOJA na MAPANGA walianza kuwapiga viongozi wa CUF akiwemo Juma Mkumbi na kuwasababishia majeraha kadhaa.

Watu waliopigwa zaidi kwenye kadhia hiyo ni waandishi wa Habari, wengi wao wameporwa simu zao na vitendea kazi mbalimbali. Hata hivyo, juhudi za wasamaria wema na wananchi wa eneo hilo zilifanyika na wananchi wakapandisha ghorofani baada ya kusikia kelele za kuomba msaada, MUNGIKI wa Lipumba wakazidiwa nguvu na kukimbilia kwenye magari yao, wakatokomea kusikojulikana.

Katika kadhia hiyo, baadhi ya MUNGIKI hao walichelewa kuwahi magari waliyokuja nayo na inasemekana walianza kukimbilia vichochoroni ambako wananchi walishakusanyika, mifukuzano ikaanza. Tunaambiwa kuwa baadhi ya MUNGIKI hao, ( akiwemo huyu pichani) wamejeruhiwa vibaya na wananchi.

The Civic United Front (CUF) tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo za kusikitisha, kughadhibisha na kutia aibu katika nchi yetu. Iweje leo katika nchi hii watu wavamiwe na makundi ya wahuni na kupigwa na kuumizwa? Iweje leo waandishi wa habari wazuiwe kuchukua habari za mambo muhimu ilimradi tu kuna genge la wahuni limeachwa lifanye litakavyo? Iweje leo, vyombo vya dola viendelee kulikumbatia kundi hili la Lipumba ambalo linaajita “MUNGIKI” huku likiachwa tu lijiite hivyo na kutenda hivyo.

Tukio hili la leo la Mabibo linanifanya niwakumbushe matukio mengine kadhaa ambayo MUNGIKI wa Lipumba wameyasimamia tena wakisaidia na POLISI ama wakati wa matukio hayo, au wakati wako chini ya vyombo vya Ulinzi na Usalama. Nitawakumbusha baadhi ya matukio hayo:

1. TUKIO LA KWANZA
Tukio la kutekwa kwa mhe. Joran Bashange (Kaimu Naibu Katibu Mkuu - Bara na Mkurugenzi wa Fedha wa chama). Watekaji walifanya tukio hilo majira ya saa 1.30 asubuhi tarehe 16/08/2016 mtaa wa Madenge, Buguruni wakiwa na PINGU na gari aina ya Noah yenye namba za Usajili T 670 CEX. Walimbeba Mhe. Bashange mzobemzobe na kumuingiza kwenye gari.

Bashange aliokolewa na wananchi waliolizunguka gari hilo na kuliwekea magogo, kisha wakawataka watekaji wajisalimishe na Polisi wakaitwa wakawakamata kwenye eneo la tukio wakawakuta na PINGU za Polisi, mikanda ya kijeshi n.k. Watekaji hao wanafahamika kwa majina ya Samweli Richard, Ramadhan Said na Shaibu Issa (Maarufu Mrangi) na walipohojiwa wakakiri kuwa wametumwa na Prof. Lipumba.

Bashange alipewa PF3 kwani aliumizwa kwenye zile purukushani, akapata matibabu kisha jalada ya upelelezi la kesi ya jinai la RB Namba BUG/IR/5937/2016 likafunguliwa. Baada ya siku chache watuhumiwa wote wakaachiwa, chama chetu kikaripoti suala hilo kwenye ofisi ya ZCO Dar Es Salaam, akamuamuru OCD wa Buguruni awafikishe watuhumiwa hao kwa ZCO. Watuhumiwa hao walipelekwa kwa ZCO na tokeo hapo hakuna kilichoendelea, walishaachiwa huru na hawakuwahi kufunguliwa mashtaka yoyote.
__________________________

2. TUKIO LA PILI
Tukio la Lipumba na kundi la MUNGIKI likisaidiwa, likilindwa na kuongozwa na POLISI lilipovamia, kupiga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF mwezi Agosti 2016, kusababisha uharibifu mkubwa Blue Pearl Hotel, kusababisha Mkutano Mkuu wa CUF uhairishwe kwa sababu za kiusalama kabla ya kukamilisha ajenda ya pili ya mkutano ambayo ilikuwa imeanza, ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa. Uhuni huo wa Mungiki na Lipumba ulikisababishia chama kulipa Shs Milioni 8.5 kwa Hotel ya Blue Pearl ili kufidia hasara ya uharibifu wa samani mbalimbali, lakini pia likakisababishia chama hasara ya Shs Milioni 800 ambazo ziliandaa Mkutano Mkuu huo maalum.

Tukio hili la uvamizi na upigwaji na uumizwaji wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu liliripotiwa Kituo cha Polisi Magombeni na kupewa RB Namba MG/RB/9072/2016 ya 22/8/2016, maelezo ya walipigwa na kujeruhiwa yalichukuliwa, wakapewa PF3 wakapata matibabu, Jeshi la Polisi likapewa CD za tukio zima likionesha picha za video za MUNGIKI waliovamia na kujeruhi watu pamoja na majina yao, lakini hadi leo hajakamatwa wala kufunguliwa mashtaka yeyote kati yao.
__________________________

3. TUKIO LA TATU
Tukio la Lipumba na MUNGIKI kuvamia Ofisi Kuu ya CUF Buguruni tarehe 24/09/2017. Katika uvamizi huo, walinzi wa ofisi na walinzi maalum wa kampuni ya Ionsides Security Company walipigwa na kunyang’anywa Bunduki moja (ambayo baadaye MUNGIKI waliikabidhi kwa jeshi la Polisi). Jambo la kusikitisha ni kuwa, MUNGIKI na LIPUMBA walikuwa wanaongozwa na kusaidiwa na maafisa wa Jeshi la polisi na Askari Kanzu ambapo Polisi walikuwa na gari mbili wakiwa na silaha za moto, LIVE bila chenga!

Uvamizi huo ulihusisha kupiga na kuumiza vibaya walinzi wa zamu, na walinzi maalum wa Ironsides Security, kubomoa milango na mageti ya Ofisi kuu na kuharibu mali za chama (kwa kusindikizwa na kusaidiwa na Polisi). Chama kiliripoti suala hili Kituo Kikuu cha Buguruni (kwa ajili ya kutimiza matakwa ya kisheria – kesi ya nyani kwa ngedere) na likafunguliwa jalada la uchunguzi kupitia RB Namba BUG/RB/8741/2016 ya tarehe 24/9/2016. Hadi leo hii hakuna uchunguzi uliofanywa wala hatua zilizochukuliwa.
__________________________

4. TUKIO LA NNE
Tukio la kutekwa mwanachama wa CUF Mohamed Said, ambalo lilitokea tarehe 10/11/2016 katika eneo la Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Polisi, baada ya kundi la MUNGIKI kuendesha vurugu kubwa huku Polisi wakishuhudia. Hii ilikuwa mojawapo ya siku ambazo kesi ya Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya Lipumba, Msajili wa Vyama na wenzao, ilikuwa inatajwa.

Baada ya Mohd Said kutekwa, alipelekwa hadi Ofisi Kuu ya CUF Buguruni akaingizwa ofisini kwa Lipumba akahojiwa na Lipumba kisha baadaye wakamuacha. Vipigo alivyopewa kwenye utekaji huo vilipelekea apate majeraha makubwa usoni na mdomoni.

Bwana Mohamed Said aliripoti Kituo cha Kati (Central Police) akapewa PF3 na kwenda kupata matibabu ikiwemo kushonwa nyuzi kadhaa na jalada la uchunguzi wa kijinai likafunguliwa kupitia RB Namba CD/CID/PE/88/2016.

Watekaji wale wanajulikana, polisi walipewa picha zao halisi za video na mnato, tangu wakati wanamkamata Bwana Mohd Said hadi wanamuingiza kwenye magari na kuondoka naye, bila ridhaa yake, tena mbele ya Polisi waliokuwa wamtanda mahakamani ili kulinda hali ya usalama. Lakini hadi leo hii, hakuna MUNGIKI aliyekamatwa wala kuhojiwa.
__________________________

5. TUKIO LA TANO
Tukio la kutekwa mhe. Joran Bashange (kwa mara ya pili) lililotokea tarehe 14/12/2016 kata ya Buguruni mkabala ya Shule ya Msingi Hekima. Kundi la MUNGIKI wa Lipumba zaidi ya 30 likajitokeza na kuanza kumshambulia likimlazimisha aingie kwenye gari ambayo haikujulikana (kwani ikimbia na baadhi ya watekaji waliotoroka).

Bashange akapiga kelele na mayowe ndipo wananchi waliokuwa karibu wakawadhibiti watekaji, wengine wakakimbia. Watekaji kadhaa waliowekwa chini ya ulinzi na wananchi wakakamatwa na POLISI baada ya wananchi kuomba msaada kwa njia ya simu. Walipohojiwa POLISI Kituo cha Buguruni wakadai wametumwa na Prof. Lipumba.

Baadhi ya waliokamatwa kwenye eneo la tukio na kufikishwa Kituoni wanajulikana kwa majina ya Twaha Ngozoma, Miraji Mtwibiliko. Jalada la upelelezi lenye RB Namba BUG/PE/116/2016 lilifunguliwa katika Kituo cha Polisi Buguruni siku hiyo hiyo.

Watuhumiwa hao (MUNGIKI) wakiwa bado rumande alifika Prof. Lipumba na kufanya mazungumzo na OCD kisha mmoja akaachiwa na mwingine akaachiwa kesho yake. Hadi leo tuongeavyo, hakuna mtuhumiwa aliyefikishwa mahakamani kutokana na tukio hilo la jinai.
__________________________

6. TUKIO LA SITA
Tukio la kuchomwa kisu mwanachama aitwaye Robert Samsoni eneo la shingo, lililotokea tarehe 14/12/2016 eneo la Mahakama Kuu ya Tanzania, mbele ya Polisi! Tukio hili lilifanywa na MUNGIKI wa Lipumba mbele ya kamera za waandishi wa habari wakiwepo na waliripoti hadi kwa picha za VIDEO, wachomaji na mchomwaji wako dhahiri kwenye video hizo.

Tukio hili lilianza baada ya MUNGIKI na Lipumba kuanza kupiga wanachama wa CUF waliohudhuria mahakamani katika kesi ya Bodhi ya Wadhamini wa CUF dhidi ya Lipumba na wenzake, ambapo mkakati wao ni kuhakikisha kwamba wananchama wanaogopeshwa ili wao tu (Mungiki) na Lipumba ndiyo wahudhurie mahakamani.

Tukio likaripotiwa Kituo cha Polisi Kati (Central Police) na PF3 ikatolewa, majeruhi akashonwa nyuzi takribani 12 (jeraha kubwa sana), majina ya MUNGIKI waliompiga na kumchoma kisu yakawasilishwa polisi, picha zao, makazi yao n.k.

Polisi wakafungua majalada ya uchunguzi namba CD/RB/12671/2016 na CD/IR/4567/2016 yote ya tarehe 14/12/2016. Hadi hivi leo tuzungumzavyo, hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa wala kuhojiwa, sembuse kufikishwa mahakamani.

______________________________

Matukio yote haya ni ushahidi tosha kwamba, Vyombo vya Dola ndivyo vinalilea, kulipa mbinu na kuliendekeza hili kundi la Lipumba, na kwamba vinashirikiana nalo kuleta vurugu, kuumiza watu na kutisha wananchi kwa kutumia mgongo wa kile kinachoitwa "Mgogoro wa Uongozi ndani ya CUF."

Mathalini, Katibu wa CUF wa wilaya ya Kinondoni, hivi karibuni yeye na mtu mwingine aitwaye Ali Makwiro, waliongea na vyombo vya habari wilayani Kinondoni na kusisitiza kuwa wao wawili wanamuunga mkono Lipumba na harakati zake za sasa. Chama chetu na uongozi wake (Mimi na Kamati ya Uongozi ya chama, Katibu Mkuu Maalim Seif, Baraza Kuu, Kamati ya utendaji ya Taifa, Bodi ya Wadhamini), hata siku moja hatukuwahi kukaa na kufikiria achilia mbali hata kupanga HUJUMA zozote juu ya wanachama wachache wanaomuunga mkono Lipumba, au viongozi wachache wanaomuunga mkono, bali hata kuombea jambo hilo litokee.

Pamoja na Usaliti alioufanya Lipumba kwa chama, pamoja na kuungwa mkono na dola ili akivuruge chama, pamoja na upuuzi na ujinga wote aliousimamia tangu alipotangaza kuwa anarejea kuwa Mwenyekiti kwa lazima, sisi viongozi wa chama tunaotambulika na vikao vyote halali vya chama, hatukuwa kufikiria ku OPT njia ya mapambano na umwagani damu kama namna ya kumshinda Lipumba na genge lake.

Mara zote tumekuwa tunawasisitiza wanachama wetu kuwa watulivu na wasijihusishe na vitendo vya matumizi ya nguvu na vurugu. Hata wabunge wetu na wanachama wa Dar Es Salaam walipopanga tarehe ya kwenda kuipokonya Ofisi Kuu ya Buguruni kutoka kwa Lipumba, nilijitokeza hadharani na kuzuia zoezi hilo na mnakumbuka nilisisitiza kuwa siko tayari kuona damu ya hata mwanachama mmoja wa CUF inamwagika ati kwa sababu sisi ni wengi na tunataka kutumia wingi wetu kumtoa Lipumba na kigenge chake pale Buguruni.

As long as, Makao Makuu ya chama (Headquarter) yanayotambulika kikatiba yako Zanzibar, niliwaambia wanachama kuwa tumuachie Ofisi Kuu (Main Office) ili yeye atambe kwa kusaidiwa na dola na nikasema mimi ntafanyia shughuli zangu na Kamati ya Uongozi kutokea Makao Makuu na nikatoa mfano kwamba mbona CCM wanaendesha chama chao kutokea Dodoma? Msimamo huu ndiyo pia msimamo wa Katibu Mkuu wa CUF.
_______________________

Sisi ambao tunatambuliwa na vikao vya chama tumeamua kutumia njia sahihi kutatua mgogoro huu wa kutengenezwa, kwa nini upande huu unaoungwa mkono na vyombo vya dola, na serikali na chama kinachoongoza dola, unatumia njia za hatari namna hii katika kumpigania Lipumba waliyemtengeneza?

Kwa nini basi Mkutano wa Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni (anayeunga mkono chama na kumpinga Lipumba) uvamiwe na kuhujumiwa na watu waliotumwa na Lipumba huku nchi yetu ina vyombo vya dola? Mbona ule wa Katibu wa Kinondoni (anayemuunga mkono Lipumba) sisi hatukutuma wahuni wauvamie? Kwani sisi hatuwezi kufanya hivyo? Kwani kazi ya vyombo vya dola ni kusimamia wavaa vinyago na wabeba silaha za moto na baridi ili kuvamia shughuli halali za vyama au utoaji wa maoni?

Chama chetu kinasikitishwa sana na vitendo hivi vya watu kuvamiwa na MUNGIKI wanaoongozwa na Lipumba, kupigwa, kuchomwa visu, kutekwa n.k. ambapo kwenye masuala yote hayo, vyombo vya dola vimeendelea kumlinda Lipumba na genge lake dhidi ya chama na viongozi wake.

Kubwa kuliko yote, tumesikitishwa mno na kitendo cha hatari sana cha leo ambapo waandishi wa habari na viongozi wa chama wakiongoza na Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni, wavamiwa na kupigwa na kundi hili la Lipumba lijiitalo “MUNGIKI’ (kama ilivyotokea leo Mabibo). Je, tukio hili lina maana gani? Lina maana kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuripoti habari za Lipumba tu, na kuhudhuria mikutano yake - na kwamba wasithubutu kusogelea mikutano ya viongozi halali wa chama (kama ilivyokuwa Mkutano huu wa leo wa Mkt wa CUF Kinondoni). Je, watanzania wanaona hali hii ni sawa tu? Je tukae kimya tu?

Je, dola, hata kama imewekeza nguvu kubwa kabisa kwenye mpango wa kuisambaratisha CUF kwa kumtumia Lipumba, na kwamba nguvu hiyo inawauma na lazima wamtumie wawezavyo hadi mwisho, kwa nini basi zisitumike mbinu za hujuma za kawaida kuliko hizi za kuteka viongozi, kuwapiga, kuwajeruhi, kuwavamia, kuwachoma visu na kuzuia shughuli zao?

Kwani usalama wa Taifa, ambao wanampangia Lipumba hujuma za namna hii hawana mbinu mbadala za kukimaliza chama cha siasa kisichotakiwa bila kutumia nguvu hii na makundi yenye mapanga na silaha za moto? Hivi unapotaka kukiua chama fulani cha siasa, ni lazima utumie nguvu za kijinga namna hii, zinazoweza kupelekea umwagaji damu bila sababu?

Natoa wito kwa IGP Mangu, Kamishna Sirro wa kanda maalum na ZCO wa Dar Es Salaam, kwamba haya yanayoendelea hivi sasa hadi viongozi wa juu wa CUF na waandishi wa habari kuanza kuvamiwa na mapanga na silaha za moto, kupigwa na kujeruhiwa, kutekwa, kuchomwa visu na kuumizwa, ni matunda ya JESHI LA POLISI ya kulilea kundi linalojiita MUNGIKI, lililoasisiwa na Lipumba na ambalo huenda linapata msaada mkubwa sana wa kiutendaji kutoka SERIKALINI!

Ndiyo maana mtu anaweza kushangaa, iweje kundi hilo litende mambo yote hayo, mpaka haya ya leo na hakuna MUNGIKI hata mmoja ambaye amewahi kufikishwa mahakamani. Mtanzania wa kawaida anaweza kujiuliza, MUNGIKI hawa wa Lipumba wanapata wapi Bastola za kutumia kuvamia mikutano halali kabisa? Dola inadhani kuwa tumeshasahau kitendo cha Nape Nauye kutolewa bastola na Ofisa wa Usalama wa Taifa?

Dola inadhani kuwa tumeshapoteza kumbukumbu kuwa watekaji wa msanii ‘Roma Mkatoliki’ na wenzake waliwatishia kwa Bastola kabla ya kuwatoa Tongwe Records. Hizi bastola ambazo sasa viongozi wa CUF na waandishi wa habari wanatishiwa na kundi la “Lipumba na Mungiki” tena hadharani mchana kweupe, wamepewa na nani? Hawaogopi dola?

Siku kundi hili la MUNGIKI litakapoendesha MAUAJI ntasikitika sana ntajapoona IGP na wenzake wakijitokeza kulaumu mauaji hayo na kudai kuwa wanawasaka wauaji. Nimeshaeleza huko awali kuwa wauaji huanza polepole, huanza kuvamia wakalindwana dola; hupiga na kuumiza wengine wakalindwa na dola; huteka, kutisha, kuchoma watu visu na wakalindwa na dola, huvamia mikutano halali na bastola na mapanga na kuumiza watu na wakalindwa na dola, na mwisho huanza kuua.

Tusubiri kundi hili la Lipumba lianze uuaji ndipo tubane pua kuwa tunalisaka! Na ifahamike kuwa chokochoko hizi ambazo zimefanywa na kundi la MUNGIKI tangu Agosti mwaka 2016 hadi leo bila kuchukuliwa hatua, ni uthibitisho mwingine dhahiri kuwa DOLA, POLISI n.k. wana HISA za kutosha kwenye kila kinachoitwa "Mgogoro wa Ndani ya CUF".

Mwisho, kwa niaba ya The Civic United Front (CUF) napenda kutoa pole zangu za dhati kwa waandishi wote wa habari waliopigwa katika kadhia hiyo, kunyang’anywa simu zao, vitendea kazi na fedha. Nawaomba waandishi wa habari na majukwaa yao tushikamane pamoja kuvibana vyombo vya dola vichukue hatua kali dhidi ya wahuni na MUNGIKI wote waliopanga njama na kutekeleza tukio la leo.

Naviomba pia vyombo vya habari vitathmini kama ipo haja ya kuendelea kutangaza habari za kundi hili la IBRAHIM LIPUMBA ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kundi hili la MUNGIKI. Lakini Ofisi ya Katibu na sisi Kamati ya Uongozi tutatoa ushirikiano wote ambao unahitajika kwa viongozi wa vyombo vya habari na majukwaa yao katika kuhakikisha kwamba wahuni hawa wanaofugwa na Lipumba na dola, wanafika mwisho wao.

Nampa pole Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni, Mhe, Juma Mkumbi, yeye na viongozi na wanachama wa CUF TAASISI walioko Kinondoni. Nameshawapigia simu na kuwataka waweke kumbukumbu sahihi za matukio yote yaliyotokea leo ikiwa ni pamoja na kusaidiana na Ofisi ya Katibu Mkuu kuyaripoti kwa IGP Mangu na wenzake ili kuweka rekodi sahihi bila kujali kuwa jeshi la Polisi litachukua hatua zozote au la!

(Pichani, ni mmoja wa MUNGIKI akiwa ameumizwa na mamia ya wananchi wenye hasira kali ambao walijitokeza kuwaokoa viongozi wa CUF na waandishi wa habari dhidi ya uvamizi. Nimejulishwa kuwa pia, wananchi hao wamepasua na kuharibu magari mawili yaliyokuwa yakitumiwa na MUNGIKI na kwamba MUNGIKI wengine walifanikiwa kutoroka, akiwemo yule aliyekuwa na BASTOLA. Kijana huyu anayeonekana pichani huonekana akimlinda LIPUMBA sehemu nyingi aendazo).

Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
22/04/2017.

===========

DAKIKA 10 ZILIVYOTUMIKA KUMWAGA DAMU CUF
cuf-300x186.jpg

VURUGU: Mmoja wa watu (kushoto) wanaodaiwa kuvamia mkutano wa viongozi wa CUF na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Vina, Manzese, Dar es Salaam jana, akijitetea kujinasua kwenye mikono ya Wananchi. PICHA NDOGO ni baada ya kujeruhiwa.

Na ASHA BANI – Dar es Salaam

VURUGU kubwa zimetokea katika mkutano wa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam baada ya kuvamiwa na genge la watu wanane waliokuwa na silaha za moto.

Watu hao waliingia ndani ya chumba cha mkutano huo na kuwapiga viongozi wa CUF na waandishi wa habari.

Tukio hilo lilitokea jana saa 5:10 asubuhi katika Hoteli ya Niva iliyopo Mabibo, wakati Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni, Juma Nkumbi, alipokuwa akielezea matukio yanayoendelea wilayani kwake, huku akidai kuwa ni kinyume na katiba ya chama hicho.

Akiwa katikati ya mkutano huo, ghafla waliingia watu wanane wakiwa wameziba nyuso kwa vitambaa usoni na walivamia meza kuu waliyokuwa wamekaa viongozi hao na kuanza kuwashambulia kwa mapanga na mikanda, huku mmoja wao akiwanyooshea bastola.

Hata hivyo, bastola hiyo ilipokonywa na kuangushwa chini na mwanachama mmoja anayemuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Maalim Seif waliumizwa kwa kupigwa na wavamizi hao, huku waandishi wa habari licha ya kujitetea, lakini nao waliambulia kipigo.

Waandishi wa habari waliojeruhiwa ni Fred Mwanjala wa Channel Ten ambaye pia aliharibiwa kamera yake, Merry Geofrey (Nipashe) aliyeumia sehemu ya mkono na kushonwa nyuzi mbili, Rachel Chizoza (Clouds Fm), Kalunde Jamal (Mwananchi), Henry Mwang’onde (The Guardian), Mariam Mziwanda (Uhuru), Estherbella Malisa (Azam TV) na mwandishi wa habari hii.

Baada ya kundi hilo kuwapiga viongozi hao kwa takriban dakika 10, huku wengine wakikimbia kujiokoa, ndipo wananchi waliokuwapo nje ya hoteli hiyo walianza kurushia mawe magari mawili waliyokuja nayo.

Magari hayo aina ya Prado yalipigwa mawe na kupasuka vioo vyote, huku mmoja kati ya watu wa kundi hilo, akitajwa kwa jina moja la Kaduguda, alikatwa kifundo cha mguu na kuachwa kikining’inia.

Mtu huyo alianza kulia na kulalamika akiomba kuachiwa, huku akisema yeye alibebwa bila ya kujua, huku akidai kuwa alitumwa na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Jamani nisameheni, mimi nimetumwa na Lipumba, naombeni mnisamehe jamani,” alilalamika huku akiendelea kulia.

Tukio hilo lililokuwa kama filamu ya mapigano liliwashtua wananchi wa eneo hilo waliokimbilia hotelini hapo, kila mmoja akisema lake, huku wengi wao wakidhani kundi hilo lililovamia ni majambazi kutokana na magari kukimbia na watu hao wakiwa wamejifunika sura zao.

Baadaye saa 5:25, askari polisi wa Kituo cha Magomeni wakiongozwa na Inspekta wa Polisi, Ahobokile Mwakabosi, walifika eneo la tukio na askari wengine kwa gari mbili.

Gari moja lilimchukua mtu aliyekatwa kifundo na kumpeleka Kituo cha Magomeni na askari wengine walichukua maelezo kwa waliojeruhiwa, wakiwamo waandishi wa habari.

Katika hatua nyingine, uharibifu umefanyika katika hoteli hiyo, ikiwamo kupasuka vioo, kuvunjwa kwa viti na kuumizwa kwa baadhi ya wafanyakazi, akiwamo mlinzi wa getini.

Godfrey Sombi aliyewahi kuwa mgombea udiwani wa Kata ya Mburahati, aliyeumizwa kichwani, alisema jambo hilo si la kunyamaziwa kimya.

Alisema vitendo vya uvamizi vimeendelea kutokea siku hadi siku kwa watu kutekwa na kupelekwa kusikojulikana na wengine kujeruhiwa na kama Serikali haitatoa tamko, kunaweza kusababisha mauaji yasiyo ya lazima.

Mlinzi wa getini katika hoteli hiyo, Mandrit Luanda, alisema wavamizi hao walifika wakiwa na magari yakiwa na bendera za CUF na hakuwa na wasiwasi nao.

Alisema waliingia licha ya kuanza kuwatilia shaka kutokana na kuwa na miili mikubwa, lakini baada ya muda mfupi alianza kusikia mapigano yakiendelea ndani ya hoteli hiyo.

“Baada ya dakika 10 walitoka na kukimbia huku wenzao watatu wakijeruhiwa na vioo vya magari waliyokuwa wamepanda vikivunjwa,” alisema.



MKUTANO

Awali kabla ya mkutano huo kuvamiwa, Nkumbi, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Mohamed Mkandu na Ally Makwilo wanajiita viongozi wa Wilaya ya Ubungo ilhali wakijua wanafanya hivyo kinyume na katiba ya chama hicho.

Alisema katika mkutano wao waliofanya Aprili 16, mwaka huu, walitoa matamko makali kwamba ni marufuku kwa kiongozi yeyote kutofautiana na Lipumba na yeyote atakayefanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Nkumbi alisema kuwa hatambui uongozi wa muda wa Ubungo kwa kuwa hakuna kikao chochote halali kilichotoa mwongozo wa uundwaji wa uongozi wa muda wa wilaya hiyo mpya.

Aliwataka wanachama wa Kinondoni wasitoe ushirikiano wowote kwa hao viongozi aliowaita kuwa ni feki.

Pia alisema anaunga mkono tamko lililotolewa na wanachama wa matawi 20 ya Dar es Salaam la kumkataa Lipumba na kumtaka kuondoka katika ofisi Kuu za Buguruni mara moja.

Aliwataka wanachama wa chama hicho waliopo wilaya hiyo kuungana pamoja kuwakataa Lipumba na lile aliloliita kuwa ni genge lake wanaotaka kuua chama na upinzani kwa ujumla.



BAADA YA TUKIO

Taarifa kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi, Uhusiano na Umma wa CUF, Mbarara Maharagande, ilisema wanalaani vikali kitendo hicho alichokiita si cha kiungwana na hakiashirii nia njema, uvumilivu na uendeshaji wa siasa za kistaarabu.

Alisema kama Jumatano wiki hii, Katibu wa Wilaya ya Kinondoni, Mohamed Mkandu, alifanya mkutano kama huo kwa amani bila bughudha na Watanzania walisikia alichokizungumza, iweje Nkumbi afanyiwe vurugu hizo?

Kwa niaba ya chama hicho, alitoa pole kwa waandishi wa habari waliojeruhiwa katika tukio hilo na kwamba wataendelea kuwa nao pamoja katika kuhakikisha kuwa wanarejea katika hali yao ya afya ili kutekeleza majukumu ya kuwatumikia Watanzania.

“Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuwakamata wahusika wote wa tukio hilo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa kuwa matukio kama haya yanayofanywa na kundi linalojulikana yamekuwa yakijirudia mara kwa mara, ikiwamo jaribio la utekaji kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Joran Bashange mbali na wahusika wanne kukamatwa eneo la tukio,’’ alisema.

Maharagande alisema inasikitisha kuona polisi wamekalia mashtaka hayo na kushindwa kuchukua hatua za kisheria.



MATUKIO YALIYOWAHI KUTOKEA

Maharagande alisema matukio kama hayo ni mwendelezo wa matukio mbalimbali yaliyowahi kutokea na kusababisha vurugu zisizokuwa za lazima katika mkutano Mkuu Maalumu wa CUF Taifa uliofanyika Agosti 21, mwaka jana.

Alisema tukio la pili ni la utekaji wa wanachama na viongozi wa chama hicho lililotokea Septemba 16, mwaka jana baada ya Bashange kutekwa akitoka nyumbani kwake Mtaa wa Madenge, Buguruni, Wilaya ya Ilala na kupewa RB namba BUG/IR/5937/2016.

Tukio la tatu alisema lilitokea Ofisi Kuu ya chama hicho iliyopo Buguruni, Dar es Salaam, Septemba 24, mwaka jana baada ya Lipumba na wafuasi wake kuvamia ofisi hiyo, kuvunja mageti na milango ya ofisi, kuwapiga walinzi binafsi wa Kampuni ya Ironsides Security Guard waliokuwa wakilinda hapo na Jeshi la Polisi likatoa RB Na.BUG/RB/8741/2016.

Alilitaja tukio la nne ni la uvamizi na kuvunja ofisi za Wilaya ya Bagamoyo na Mkuranga lilitokea Novemba 4, mwaka jana na Lipumba na wafuasi wake wakilindwa na polisi walikwenda katika ofisi hizo.

Alisema tukio la tano ni la wabunge na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi kuzuiliwa kufanya mikutano na kukamatwa huko Nachingwea.

Alilitaja tukio la sita kuwa lilitokea Oktoba 10, mwaka jana baada mkutano kuzuiliwa kufanyika mkoani Tanga.

Chanzo: Mtanzania
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2017-04-23 at 20.13.24.jpeg
    WhatsApp Image 2017-04-23 at 20.13.24.jpeg
    24.7 KB · Views: 39
Wapinzani kuchukua Nchi bado sana labda 2055. AAcha wajifunze kwanza kuongoza Nchi maana hakuna namna. Hatuwezi kuweka Nchi rehani kwa kuifanyia majaribio ya Uongozi!!
Siasa za nchi hii ziliisha elekea kubaya siku nyingi, tokea wakati ule wa mauaji ya Mwembechai. Ni CUF hii hii ambayo serikali inaiogopa. Polisi walishatumika mno kujaribu kukiangamiza chama hiki hadi mkuu wa polisi wakati ule (Mahita) akaapa kwamba CUF haiwezi kuchukua dola. Akasema kama wao ni ngangari yeye ni ngunguri. Ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka juzi ndo kabisaa yalitonesha kidonda, mkuu wa nchi aliudhi watu wengi baada ya kusema Jecha anastahili tuzo.
Tujiombee kama taifa, lakini siasa za nchi hii hazielekei kuzuri.
 
Inashangaza viongozi eti wanainamisha vichwa kwa viongozi WA kiroho wapewe baraka. Mungu hadhihakiwi jamani ili wewe usalie madarakani kwa kuzuru wengine
 
juzi juzi tu askari polisi 8 wameuwawa lakini nguvu yote imeelekezwa kwingine badala ya kuwasaka wauaji

hii sirikali inatumia mkono mmoja huo huo kula chakula na kuokota takataka bila kunawa.. what do you expect kama sio kuugua bila kupona?
 
Back
Top Bottom