mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,548
Leo kuanzia mida ya saa kumi jioni kulikuwa na mkutano mkubwa uliofanyika katika viwanja vya bima katikati kabisa mwa mji wa Mtwara. Mkutano huo ulioandaliwa na CUF ulihudhuriwa na Bwana Katani Katani ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo. Bwana Katani aligombea ubunge katika wilaya ya Tandahimba na kushindwa kwa mizengwe na Ndugu Njwayo wa CCM, alivalia pensi na Tshirt aliushangaza umati huo kwa mavazi yake lakini alipoanza kutoa hoja wananchi hao walisahau mavazi yake hayo.
Hoja
Wengi wa wazungumzaji walishikilia msimamo ule ule "Gesi haitoki ikiwa Ghafi" huku kauli mbiu nyingine ikiibuka na kusema "Gesi kusini kwanza Dar Baadae". Moja ya hoja ni kuwa ni lazima gesi ichakatwe hapa mkoani Mtwara na plant ya umeme ianzishwe hapa Mtwara na kisha usafirishwe kunufaisha watanzania wengine. Mmoja wa wazungumzaji alisema Wanamtwara wamechoka kuwa vipofu wa kushikwa mkono wakati wa kula ugali na sasa wanaona na wanataka kula ugali huo bila kushikwa tena mkono.
Wananchi wengi walikuwa wanajibu maswali wanayoulizwa kwa hamasa kubwa...Mfano swali moja liliuliza "wangapi wapo tayari kufa ili gesi isitoke Mtwara?" wananchi karibu wote waliokuwepo pale walinyoosha mikono..(Mtaona picha hizo kwenye magazeti na blog mbalimbali...kwani niliona waandishi wengi wa habari...binafsi sikufanikiwa kupiga picha)
Wazungumzaji wengi waliwashutumu Mh Ghasia kwa kufananisha jina lake na neno "FUJO" huku Mkuchika akianikwa hadharani kuwa ni mnafiki namba moja na kwamba mawaziri hao kwa sasa hawawezi kutembea tena Mchana wakiwa Mtwara na wamekuwa wakiingia kimya kimya tena usiku kuepuka dhahma kutoka kwa wananchi hao.
Roma Mkatoloki, Kalapina Na Kundambanda Kupamba Mkutano
Mgeni rasmi aliutaarifu umma kuwa tarehe kumi na tisa ya mwezi huu kutakuwa na maandamano na mkutano mkubwa mwingine wa kupinga suala la gesi na kusema Mkutano huo utahudhuriwa na Wasanii Roma Mkatoliki, Kalapina na Kundambanda. Alisema wameshindwa kumualika "Diamond" kwa kuwa suala hilo si la burudani bali la kiharakati zaidi ndio maana amewaalika wasanii wanaharakati.
Wacha niishie hapa...kwa jinsi nilivyoona Wananchi waliopo mkutanoni......Kuna haja ya Serikali kukutana na Wanaanchi kupata muafaka wa suala hili....vinginevyo tunapoelekea si kuzuri...