Mkutano wa CHADEMA Sombetini

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
Wakuu,
Mkutano wa kampeni wa chadema sombetini ndiyo umefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Kata ya Sombetini Kamanda Madava ndiyo amefungua rasmi, lakini amegusia suala la utulivu, kwamba tunaombe tuwe watulivu kwa kipindi hiki cha kampeni, tuwe wapole, wavumilivu, lakini tusiwe wanyonge. Amesema tusimguse wala kumchokoza mtu, lakini tukiguswa tusimwache....

Diwani wa Ngarenaro Doita anawasalimia wananchi, anasema maendeleo yanayoonekana Arusha ni kwasababu ya chadema, wakati hatupo hawakuthubutu, lakini tulipoingia tukikohoa wanafanya..... chezea chadema.

More Updates::

Nanyaro anasema tutahakikisha kikao cha bajeti kwenye baraza la halmashauri kabla ya uchaguzi wa sombetini. baada ya bananga kuingia kwenye baraza la madiwani chadema wataongoza kamati zote na maendeleo lazima yaje kwa kasi


Mawazo;
pamoja na matatizo yote niliyowahi kupata, nakiri kuwa kama kuna wakati naona kuna raha ni wakati huu wa kupigania ukombozi wa watu maskini.......


Mawazo;
Kanda ya ziwa nimeivuruga ccm kote, nimefanya mikutano 400 kwa mwaka katika majimbo 38, na hatafuti utukufu bali kukomboa watu maskini kama mimi ambao wameteswa mateso mengi.....





Lema,
Bananga anafanya kazi nzuri kwenye chama, amekisaidia chama lindi na mtwara, leo tuna wenyeviti wa serikali za mitaa kule yote ni kwasababu ya kazi ya Bananga.

Lema;
Uchaguzi wa Sombetini, akipigwa moja wetu, tunaacha kampeni, tunakwenda kumsaidia mwenzetu. Hatuwezi kuvumilia upumbavu wowote na hili polisi na usalama wa taifa wasikie


Lema,
Nilipokuwa bungeni majuzi nilimwambia Ole Medeye kuwa Kikwete akikurudisha uwaziri utakuwa chizi.
Tumesikia jamaa amempiga chini.
Ole Medeye anahubiri ukabila wakati ameoa mchaga mpuuzi kweli

Lema,
Kesho kutwa tunaanza operations nchi nzima, helcopter tano kwa siku kumi, agenda kuu ni rasimu ya katiba na kupanda kwa gharama za umeme na gesi. Kazi ya sombetini tunawaachia BAVICHA wakapambane na hawa ndondocha





.........................................................................................................................................................................
.........................................................................................................................................................................



 
Peoplezzzzzzzz😛eace😛owerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Arusha Glory anawasalimia wananchi, anasema hatujaja kufanya kampeni, bali kuja kuwashukuru wapiga kura...... Bananga ni diwani anayesubiri kuapishwa
 
Mweka hazina wa chama wilaya ya Arusha kamanda Nsajigwa Mwakatobe anawasalimia wananchi, anasema wao wana hela sisi tuna watu tusiogope tutashinda
 
Makamanda mnatisha!!!!!!!

Mimi natafuta tenda ya kusomba watu kwa malori yangu...magamba naombeni mnipatie tenda malori yangu yamepaki hayana kazi
 
Wakuu,
Diwani wa Ngarenaro Doita anawasalimia wananchi, anasema maendeleo yanayoonekana Arusha ni kwasababu ya chadema, wakati hatupo hawakuthubutu, lakini tulipoingia tukikohoa wanafanya..... chezea chadema

Hizi porojo ndio zinasababisha nisifike kwenye mikutano ya CHADEMA, sikuzoea kudanganywa!
 
Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Arusha Noel Olevaroya anasema yeye ni mmasai na yupo chadema, nimeshangaa ccm wanahubiri ukabila kwa kuwaambia wamasai wasichague wagombea wachaga, anasema hii ni dhana na fikra mfu, kwasababu kitendo hicho cha ukabila ikiendelea ni sawa na kuwaambia wachaga wasiwachague wamasai.
Anasema vijana hatuko tayari kuonewa na polisi kwa uhuni wa ccm.......
 
Mbunge wa Simanjiro Kamanda James Ole Milya anasema wamsai ni wastaarabu sana, na hatuko tayari kugawanywa kwa ukabila..............
 
Nawatakia ufunguzi mwema, amani itawale kipindi chote cha kampeni
 
Vipi wakuu Kamanda Mawazo hakualikwa kwenye huo ufunguzi?
 
Mbunge wa Simanjiro Kamanda James Ole Milya anasema wamsai ni wastaarabu sana, na hatuko tayari kugawanywa kwa ukabila..............

Huu uchaguzi ulifanyikia geto gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…