Nilimkuta mke wangu anasoma kitabu, nikaichukua nikakutana na mstari moja unasema, ukiona unatukanwa usijibu, kwasababu lengo la aliyekutukana wewe ni kumjibu, sasa usipomjibu huwa anajisikia vibaya sana. Hivyo sina muda wa kuwajibu matusi yao nimeamua kuwapuuza.
Ndiyo maana akisimama Mnyika bungeni ni sawa na wabunge sitini wa ccm, akisimama Lissu mawaziri wote wanatetemeka, akisimama Lema wabunge wote wa ccm wanatamani kutoka nje ya bunge. Chadema tunacheza mpira wa kistaarabu.
Mwigulu kule igunga tulimfumania lakini hatutali kutumia karata hiyo kama kigezo cha kushinda.
Ccm wamebakiwa na karara moja ya kuwagawa watu kwa ukabila. Katika barabara mbovu arusha elerai inaongoza, tukamchagua bayo lakini akaingia kwenye mifuko ya wala rushwa tukamfukuza.
Cha kushangaza nguvu ya fedha ya ccm arusha inatoka kwa Lowassa, jana walikuwa wanavhangishana club afriko, sasa kama wanatimia ukabila kuwagawa watu mbona Lowassa ni mmeru na ni mbunge wa wamasai na amemwoa mrangi?