Mkutano wa CHADEMA Arusha - Nov 29, 2013

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
Mkutano wa chadema umeanza muda katika uwanja wa Ngarenaro, amezungumza Diwani Doita
anasema;
Halmashauri ya arusha imekuwa ikifanya mambo sivyo, kwa kuwa sasa ni katibu wa elimu na afya atashughulikia swala la rushwa hospitali, na michango mashuleni kwani kuna mil 900 iko haina kazi na sasa amemshauri mkurugenzi zika nunue madawati, yeye kama mwenyekiti hataki michango mashuleni, na wazazi msikubali kupitisha michango mbalimbali.

Doita anasema Sisi kama wanasiasa siyo kwamba tunaingilia walimu wakuu ila kwa hawa wanaokuja na njaa njaa zao tutapigana nao

Updates;
Anazungumza James Ole Milya, anasema chama kibaki kwa wananchi, hatuwezi kutaka magugu ndani ya ccm yatolewe wakati kwetu kuna magugu, tunatoa kwanza kwetu.

Milya anasema Simbachawene ni mpumba anaposema tutumie kibatari je computer, viwanda navyo vitumie vibatari, hili ni tatizo la kuweka waziri ambaye hata jimboni kwake hana umeme na hana uelewa anajua umeme ni kwaajili ya kuwasha taa..
Milya anasema sijutii kuondoka ccm, ninaomba kamati kuu tukaamshe vijijini..nina hasira na ccm na tukiwachekea watatumaliza, Mulongo ameendelea kuwa muongo, anasema baada ya div 5 wataenda mpaka div 7...

Ally Bananga anasema mfungwa anatamani kurudi gerezani, hawa mabwege wanafanya mabaya sana, ccm wajue wakitengeneza picha wajue watazanzania wanataka maji. Elimu bora,ajira kwa vijana..

 
Updates
Mh Nanyaro anawashukuru wana wa Arusha kwa kuwaongezea madiwani, hivi sasa maamuzi mengi halmashauri, yanafanywa na Cdm, sasa wameweza kujenga madarasa 52 kwa hela za halmashauri,
Anamtambulisha naibu meya Msofe na kusema hadi sasa hakuna muafaka na ccm kuhusu meya ila kuna naibu meya aliyechaguliwa na vyama vyote
 
Chadema Daima
Suala la Viongozi watimuliwa nalo pia litolewe ufafanuzi ili kukanusha habar ziziso za kweli.
 
Watu kila siku wanachangia harusi halafu anakuja mwanasiasa anawakataza kuchagia elimu!

Hivi elimu na harusi kipi muhimu?

Chadema sifuri kabisa...
 
...

....magugu toa shambani choma moto!!!!

pamoja sana niko njiani...
 
Watu kila siku wanachangia harusi halafu anakuja mwanasiasa anawakataza kuchagia elimu!

Hivi elimu na harusi kipi muhimu?

Chadema sifuri kabisa...

Hapa hadanganywi mtu.
Kodi wananchi wanatoa kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa,Na sio kila siku michango Sifuri ni ccm haijui kuchambua sera.
 
Bananga Anasema kama tuko kwenye mtungi halafu mwenzetu kwa kuwa ana kiu anaamua kutoboa mtumbwi ili amwenye maji, uki maliza maji si mtubwi utazama sasa sisi hatukubali atazama mwenyewe..
 
Nanyaro anazungumza anasema yeye anajikita kwenye matatu..hakuna mtoto atakae baki nyumbani eti madarasa yamejaa, tumejenga madarasa 51, hakuna mzazi kuchangishwa, 2. Natangaza hivi arusha mjini tuna naibu meya alie chaguliwa na vyama vyote
 
Nanyaro;
Hatuna mwafaka na ccm yaani na hatuwezi kuingia na mwafaka na meya fake ambaye amekali kiti chenye damu..hivyo kuanzia sasa naibu meya ndiyo meya wetu, na kwa muda mchache na usimamizi tulioufanya kwenye barabara mpaka pesa ikabaki hivyo wafadhili wamefurahi na wametuongeza bilion 20 na pesa hizi zitajenga brbr ya ungaltd mpaka dampo, sombetini, njiro, kaloleni..jiji liko chini ya chadema maana tumewazi hata huyo meya fake juzi alishindwa kuongea kiingereza...
 
Nanyaro;
Uwanja ulioko karibu na shoprite unarudishwa kwa wananchi kuanzia mwakani tutafanyia mikutano pale..wrong parking akiendelea kutuzingua tutamng'o..
 
Tunaomba uwakumbushe kutolea ufafanuzi mambo yafuatayo.

Chama kina kopesha wana chama wake?

Wanao kopeshwa wanarudisha na riba?

Ni lini chama kitajenga makao makuu na kuondokana na swala la kupangisha.

Ni kipengele kipi kwenye katiba ya chadema kina ruhusu mwanachama kumpiga tofali la kichwa mwanachama mwenzie anapo kosea?

Pesa wanazo changa wananchi zina kwenda wapi mbona huko mikoani hakuna ofisi?

Chama kipo tayari kuendelea kutonywa kinapo taka kufanyiwa ukaguzi wa pesa za wananchi?

cc Godbless J Lema
Henry Kilewo
Joshua nasary
 
Last edited by a moderator:
Nanyaro;
Wafanyabiashara wanatakiwa kutozwa usafi katikati ya mji ni 500 na siyo 10,000/=
 
Cha muhimu cdm waimarishe chama chao kuanzia ngazi za chini kabisa,malumbano yasipewe nafasi
 
Hakikisheni wasaliti wote Yuda Iskaryote tupa kule waende kwa masisiem yanayowatuma kuvuruga chama.
 
Watu kila siku wanachangia harusi halafu anakuja mwanasiasa anawakataza kuchagia elimu!

Hivi elimu na harusi kipi muhimu?

Chadema sifuri kabisa...

Kuna diwani mmoja wa upinzani mjinga sana kule morogoro alipanda majukwaani na kubabaika hivyohivyo @ wazazi msilipe michango yeyote na mwisho akasusiwa mashule yote ya kata yake kama sio mkuu wa wilaya kuingilia kati wale wanafunzi na wazazi wao waliodanganywa wangejuta sana. Watu hawa ni wa kuwapuuza tu.
 

Wao si wako safi sasa wanalialia kutonywa ili kuficha mvunguni madhaifu gani kama sio ulaghai huu.
 
Last edited by a moderator:
Watu kila siku wanachangia harusi halafu anakuja mwanasiasa anawakataza kuchagia elimu!

Hivi elimu na harusi kipi muhimu?

Chadema sifuri kabisa...

kuna milioni 900 hazina kazi pale manispaa, zitachangia elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…