Mkutano wa CCM wilaya ya Mpanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa CCM wilaya ya Mpanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Jul 15, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hadi sasa hakuna ambacho kinaendelea, pamoja na matangazo ya mbwembwe nyingi, lakini hadi hivi sasa hakuna chochote ambacho kinaendelea. Pamoja na madai kuwa kutakuwa na mawaziri watano, lakini tetesi zinasema kuwa hakuna mawaziri isipokuwa waziri magembe tu na manaibu wengine kama Malima, na Agrey Mwanry. Wengine ni makada wa chama kama Nape na Mwigulu.

  IMG0055A.jpg IMG0053A.jpg IMG0052A.jpg

  Hizi ni baadhi ya picha na hali halisi katika ofisi za makao makuu ya ccm wilaya ya mpanda.

  Nitaendelea kuwa UPDATES. ILA PICHA SIYO NZURI SANA KAMCHINA KANGU SIYO KAZURI!!!! TUVUMILIANE WADAU.

  UP DATES.....!!!!!


  Naona ofisi inaanza kuchangamka, na magari yanaanza kuingia, akina mama wanajiandaa na matarumbeta yanaanza kusikika. Bila shaka wageni watakuwa wanakaribia kuingia. Nitaendelea kuwajuza!!!!


  UP DATES.....
  naona jamaa ndiyo wanaingia hapa ofisi za ccm wilaya. Ngoja nichukue picha halafu nitawajuza mkutano ukianza....be patient please!!!!!!!


  UP DATES....picha za waliofika kwenye mkutano wa ccm mpanda...


  IMG0058A.jpg IMG0059A.jpg
  NAPE NA MWIGULU


  UP DATES.....

  Sikuwa hewani kwa muda kutokana na shamra shamra za maandamano kutoka ofisini kwenda kwenye viwanja vya KASHAULILI Ambako mkutano unafanyika....

  sasa hivi NAPE Anaongea na kutoa shukrani. Watu siyo wengi kama ilivyotarajiwa....uwanja umepwaya sana....Nape anasema kidumu chama cha mapinduzi, watu hawamjibu.....anaanza majigambo...kuwa yeye ndiye msemaji wa chama bora cha ccm tz....

  UP DATE......

  Anaanza matusi ya reja reja....eti waliotoka bungeni wakati jk anahutubia walikuwa wapambe.....anazungumzia wakati cdm wanakwenda kumuona jk ikulu kwa ajili ya katiba mpya....

  Ameanzisha nyimbo ya TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE......NAPE HUYO...

  UP DATES.....

  Anazungumzia mkutano wa jana wa Ndago na mauaji ya kijana wa ccm.....!!! Ameanza matusi...eti wabunge wa cdm akili zao hazina akili....anasema mkutano wa cdm ulikuwa wa wahuni na waliohutubiwa walikuwa magaidi na wahuni wasioitakia mema tz....ccm inalaani sana mauaji haya...anasema kwa kuwa wao wako madarakanik wanaagiza vyombo vyote vya ulinzi na amani viwashughulikie wote waliohusika......anamwagiza msajili wa vyama vya siasa akiangalie chama ambacho kinaleta fujo....ananukuuu biblian na kurani...habari ya mfalem suleimani na wale wana mama wawili wenye watoto na maamuzi ya mfalme suleima kuhusu maamuzi aliyoyachukua kuhusu yule mtoto ambaye alitaka kugawanywa......

  UP DATES.....

  Anatoa mfano wa Kenya...na uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi......wameanzisha nambari one ya Komba......
  anaanza kuwatambulisha mawaziri na Mwigulu Nchemba.....!!!!

  anamdharau dr slaa eti ni babu....kazi kweli leo...watu hawaongezeki....nitawarushia picha baadaye kidogo...!!!

  UP DATESS.....
  Mwigulu ameanza kuongea....anazungumzia kupanda kwa maisha na hali ngumu ya uchumi....anaanza kuchambua bajeti ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.....


  UP DATES......!!!
  Ameanza matusi...anasema kuna siku wapinzani watakana jinsia zao....siyo matusi haya?????


  UP DATES....
  Anazungumzia upandaji wa maisha na sababu zake.....
  1. anasema ni kupanda kwa gharama za mafuta eti kwa sababu kuna vita mashariki ya kati....
  anasema kuwa hakuna mtu ambaye atakuwa kijana milele.....sijui hata anamaanisha nini!!!!!!
  Anamtukana mbowe eti....mpigisha disco......!!!!
  anazumzia UDOM....Eti asiyeona kuwa jakaya hajafanya chochote, hana akili!!!!

  UP DATES....
  anazungumzia habari za Mbowe na kuchukua gari la Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni....
  anagusia habari za mbowe kumlipia mtoto wake chekechea mil 15.....
  anasema kuwa hakuna hata kiongozi mmoja wa upinzania mwenye lengo la kuikomboa nchi hii.....!!!!

  UP DATES.....
  anazungumzia urafiki wa CDM na chama cha Cameroon...eti kwa kuwa Cameroon anataka ndoa za jinsia moja, anasema CDM wataleta ndoa za jinsia moja......

  NAPE AMEZINGUA CAMPAIGN nyingine eti AHADI NI DENI....amempandisha J. Magembe...eti ataeleza utekelezaji wa ilani ya ccm kwenye maji.....anadai vigelegele kwa magembe....

  Magembe anabisha hodi Katavi na anawaomba watu wanyooshe mikono juu kuonesha kama kweli wamemkaribisha.....anawasifia akina DHAIFU NA LIWALO NA LIWE.....

  UP DATES....
  akina mama hapa kando yangu wanasema hata jiwe likisimama kugombea dhidi ya JK katika jimbo la mpanda mjini, jiwe litashinda....nimefurahi sana...huku kwetu akina mama wanatupa raha kweli, wako againsta ccm kabisa....raha kweli....

  UP DATES....
  Magembe amepunguza bei ya maji kutoka kutoka 25 hadi 30.....anadai amepunguza, lakini akina mama hapa wananiambia bei ya maji ni shilingi 25 kwa ndoo...yeye kadai kuwa amepunguza hadi shilingi 30...jamani...kazi kweli sijui amepunguza au ameongeza....!!!

  Up DATES....
  Watu wanaanza kuondoka....hakuna cha maana ambacho kinaongelewa....hata mimi wanaanza kuniboa!!!!

  UP DATES....
  Amenza mzee wa wake za watu na smg...adam Malima....anasema Kikwete atakabidhi km 16000 za bara bara tz nzima....

  UP DATES....
  Watu wanaondoka.....anaongea sasa naibu waziri wa mifugo....sijui jamaa ni mmasai....kiswahili kigumu kweli kake...jamani watu wanazidi kuisha kwenye mkutano.....

  IMG0086A.jpg IMG0082A.jpg IMG0083A.jpg

  Hii ndiyo hali halisi, nape asije akaanza kujisifu...uwanjani watu ndiyo hawa...tena wanazidi kupungua kwa sababu hakuna ambacho wanaongea kikaeleweka.....aibu tupu....

  UP DATES.....
  Anaongea naibu waziri wa uchukunzi.....hali ni mbaya....jamani watu wanaisha uwanjani na mimi ni miongoni mwao....hakuna cha maana hapa, anasema watu watakuwa na masikio lakini hawataona.....sijui masikio yanaona siku hizi....bange hizi.....!!!!! Me naondoka...asanteni wote ambao mmenifuatilia tangu jana nilipotoa taarifa za mkutano hadi leo ambapo mkutano hauna mvuto wala mashiko...hakuna cha maana hapa TCHAOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   

  Attached Files:

 2. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  malori ya kusomba watu vipi hayajawekewa mafuta?
   
 3. Rogate

  Rogate JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Keep us Posted
   
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali mbaya, limepita moja hapa kubwa, lakini lina watu kama kumi na watano hivi, naona watu wamechoka kubebwa bure!! Hali mbaya kweli hapa, nasikia nyimbo za komba, lakini watu sura zimeshuka chini, kazi kweli kweli.
   
 5. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dont wory brother, I will try my level best.
   
 6. s

  sangija Senior Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado dawa haijawaingia sawasawa!!!! Kenge kujitambua kuwa kapokea kipigo lazima aone damu zinatoka maskioni!!!!
   
 7. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ndiyo uzuri wa JF tupo kila mahali..tunasubiri update zako,vp hawajatoa mgao kama kawaida yao?
   
 8. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona gari lenye nyimbo za komba bado linazunguka mji, lakini hakuna wafuasi! Naona watu wanaondoka ofisini mmoja baada ya mwingine, sijui kama kuna mkutano leo, dalili zinazidi kupungua.
   
 9. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,382
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Mkutupe update basi....
  Kama hali ikiwa hivyo mi ndo nafurahiiiiiiiii!!!!
   
 10. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona meneja wa Tanesco ni mdau wa cdm, umeme upo.
   
 11. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Liwalo na Liwe yupo?
   
 12. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  I mean elfu tano na ubwabwa ili wananchi wahudhurie...
   
 13. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nitahakikisha kila ambacho kipo ndani ya uwezo wangu kinaingia JF. Dont wory brother!!!
   
 14. s

  sangija Senior Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari kama hizi zinaleta faraja kubwa kwa wenye uchungu na hii nchi na wazalendo wa kweli,naomba mungu atuweke salama hadi 2015! watakimbia vivuli vyao! believe me!!!!
   
 15. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hali mbaya, bila shaka leo hakuna wali, naona watu wanatawanyika kutafuta ridhiki kila mmoja kivyake. Kuhusu elfu tano, sina uhakika, watu ni wachache sana, labda mkutano ukianza wataongezeka.
   
 16. G

  Gongerfasil Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 25
  safi saaaaaaaaaaaana ngugu endelea kutujuza mpka hawa jaamaaa waondoke
   
 17. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anajua joto la mpanda, hawezi kuhudhuria mikutano ya hivi, aliondoka hivi juzi alikuwa kwenye msiba wa shemeji yake.
   
 18. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna shida, nitawajuza kila kitu.
   
 19. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kwetu sisi komba nikimnyama kidogo chenye tabia yakunywa mnazi na kikshalewa kinaanguka kutoka juu ya mnazi adi chini.
   
 20. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu tunashukuru kwa picha. Nappe hakawii kuja humu na IDs mchanganyiko kujitapa kwamba alijaza watu.!
   
Loading...