Mkutano wa CCM wilaya ya Mpanda

Mkutano wa CCM wilaya ya Mpanda

kamanda ahsante sana sana kwa kusaidia sana kuutangaza mkutano wetu wa mpanda, lakini pia ahsante kwa kuhudhuria. Umefanya uzalendo mkubwa kwa ccm kwa kazi nzuri ya kuutangaza mkutano wetu.

Ulipochemka ni kidogo sana hasa unapojaribu kupotosha ukweli wa kilichotokea, sina haja ya kusema waliohudhuria wanajua kilichotokea na vyombo vingine vitaroti ukweli, na ndo itakuwa aibu yako. Kwa kifupi nawashukuru sana wananchi wa mpanda kwa mapenzi yao makubwa kwa chama cha mapinduzi.




Ote=stk one;4242679]hadi sasa hakuna ambacho kinaendelea, pamoja na matangazo ya mbwembwe nyingi, lakini hadi hivi sasa hakuna chochote ambacho kinaendelea. Pamoja na madai kuwa kutakuwa na mawaziri watano, lakini tetesi zinasema kuwa hakuna mawaziri isipokuwa waziri magembe tu na manaibu wengine kama malima, na agrey mwanry. Wengine ni makada wa chama kama nape na mwigulu.

View attachment 58857View attachment 58859View attachment 58860

hizi ni baadhi ya picha na hali halisi katika ofisi za makao makuu ya ccm wilaya ya mpanda.

Nitaendelea kuwa updates. Ila picha siyo nzuri sana kamchina kangu siyo kazuri!!!! Tuvumiliane wadau.

Up dates.....!!!!!


Naona ofisi inaanza kuchangamka, na magari yanaanza kuingia, akina mama wanajiandaa na matarumbeta yanaanza kusikika. Bila shaka wageni watakuwa wanakaribia kuingia. Nitaendelea kuwajuza!!!!


Up dates.....
Naona jamaa ndiyo wanaingia hapa ofisi za ccm wilaya. Ngoja nichukue picha halafu nitawajuza mkutano ukianza....be patient please!!!!!!!


Up dates....picha za waliofika kwenye mkutano wa ccm mpanda...


View attachment 58868 View attachment 58869
nape na mwigulu


up dates.....

Sikuwa hewani kwa muda kutokana na shamra shamra za maandamano kutoka ofisini kwenda kwenye viwanja vya kashaulili ambako mkutano unafanyika....

Sasa hivi nape anaongea na kutoa shukrani. Watu siyo wengi kama ilivyotarajiwa....uwanja umepwaya sana....nape anasema kidumu chama cha mapinduzi, watu hawamjibu.....anaanza majigambo...kuwa yeye ndiye msemaji wa chama bora cha ccm tz....

Up date......

Anaanza matusi ya reja reja....eti waliotoka bungeni wakati jk anahutubia walikuwa wapambe.....anazungumzia wakati cdm wanakwenda kumuona jk ikulu kwa ajili ya katiba mpya....

Ameanzisha nyimbo ya tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote......nape huyo...

Up dates.....

Anazungumzia mkutano wa jana wa ndago na mauaji ya kijana wa ccm.....!!! Ameanza matusi...eti wabunge wa cdm akili zao hazina akili....anasema mkutano wa cdm ulikuwa wa wahuni na waliohutubiwa walikuwa magaidi na wahuni wasioitakia mema tz....ccm inalaani sana mauaji haya...anasema kwa kuwa wao wako madarakanik wanaagiza vyombo vyote vya ulinzi na amani viwashughulikie wote waliohusika......anamwagiza msajili wa vyama vya siasa akiangalie chama ambacho kinaleta fujo....ananukuuu biblian na kurani...habari ya mfalem suleimani na wale wana mama wawili wenye watoto na maamuzi ya mfalme suleima kuhusu maamuzi aliyoyachukua kuhusu yule mtoto ambaye alitaka kugawanywa......

Up dates.....

Anatoa mfano wa kenya...na uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi......wameanzisha nambari one ya komba......




Anaanza kuwatambulisha mawaziri na mwigulu nchemba.....!!!!

Anamdharau dr slaa eti ni babu....kazi kweli leo...watu hawaongezeki....nitawarushia picha baadaye kidogo...!!!

Up datess.....
Mwigulu ameanza kuongea....anazungumzia kupanda kwa maisha na hali ngumu ya uchumi....anaanza kuchambua bajeti ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.....


Up dates......!!!
Ameanza matusi...anasema kuna siku wapinzani watakana jinsia zao....siyo matusi haya?????


Up dates....
Anazungumzia upandaji wa maisha na sababu zake.....
1. Anasema ni kupanda kwa gharama za mafuta eti kwa sababu kuna vita mashariki ya kati....
Anasema kuwa hakuna mtu ambaye atakuwa kijana milele.....sijui hata anamaanisha nini!!!!!!
Anamtukana mbowe eti....mpigisha disco......!!!!
Anazumzia udom....eti asiyeona kuwa jakaya hajafanya chochote, hana akili!!!!

Up dates....
Anazungumzia habari za mbowe na kuchukua gari la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni....
Anagusia habari za mbowe kumlipia mtoto wake chekechea mil 15.....
Anasema kuwa hakuna hata kiongozi mmoja wa upinzania mwenye lengo la kuikomboa nchi hii.....!!!!

Up dates.....
Anazungumzia urafiki wa cdm na chama cha cameroon...eti kwa kuwa cameroon anataka ndoa za jinsia moja, anasema cdm wataleta ndoa za jinsia moja......

Nape amezingua campaign nyingine eti ahadi ni deni....amempandisha j. Magembe...eti ataeleza utekelezaji wa ilani ya ccm kwenye maji.....anadai vigelegele kwa magembe....

Magembe anabisha hodi katavi na anawaomba watu wanyooshe mikono juu kuonesha kama kweli wamemkaribisha.....anawasifia akina dhaifu na liwalo na liwe.....

Up dates....
Akina mama hapa kando yangu wanasema hata jiwe likisimama kugombea dhidi ya jk katika jimbo la mpanda mjini, jiwe litashinda....nimefurahi sana...huku kwetu akina mama wanatupa raha kweli, wako againsta ccm kabisa....raha kweli....

Up dates....
Magembe amepunguza bei ya maji kutoka kutoka 25 hadi 30.....anadai amepunguza, lakini akina mama hapa wananiambia bei ya maji ni shilingi 25 kwa ndoo...yeye kadai kuwa amepunguza hadi shilingi 30...jamani...kazi kweli sijui amepunguza au ameongeza....!!!

Up dates....
Watu wanaanza kuondoka....hakuna cha maana ambacho kinaongelewa....hata mimi wanaanza kuniboa!!!!

Up dates....
Amenza mzee wa wake za watu na smg...adam malima....anasema kikwete atakabidhi km 16000 za bara bara tz nzima....

Up dates....
Watu wanaondoka.....anaongea sasa naibu waziri wa mifugo....sijui jamaa ni mmasai....kiswahili kigumu kweli kake...jamani watu wanazidi kuisha kwenye mkutano.....

View attachment 58871View attachment 58874 View attachment 58875

hii ndiyo hali halisi, nape asije akaanza kujisifu...uwanjani watu ndiyo hawa...tena wanazidi kupungua kwa sababu hakuna ambacho wanaongea kikaeleweka.....aibu tupu....

Up dates.....
Anaongea naibu waziri wa uchukunzi.....hali ni mbaya....jamani watu wanaisha uwanjani na mimi ni miongoni mwao....hakuna cha maana hapa, anasema watu watakuwa na masikio lakini hawataona.....sijui masikio yanaona siku hizi....bange hizi.....!!!!! Me naondoka...asanteni wote ambao mmenifuatilia tangu jana nilipotoa taarifa za mkutano hadi leo ambapo mkutano hauna mvuto wala mashiko...hakuna cha maana hapa tchaooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
[/quote]


mdogo wangu nape
hivi ni lini wewe na chama chako mtakuwa wakweli inaonekana huko chamani kwenu ni mwendo wa uongo na uzandiki tu
1. Uliwahi kukana id yako kuhusu wewe kuripoti matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa igunga hata kabla ya kutangwazwa
2. Mlibisha kuhusu vijana wenu kuhusika na mauaji ya nduguyetu mbwambo arusha (waliokamatwa ni wakina nani)
3. Ulikataa kuwa hujawataja kwa majina mafisadi na wala hujatoa ahadi ya siku 90 juu ya mafisadi hao (edo, chenge na rostam) kujivua gamba..... Kumeishia wapi kujivua gamba
4. Wakati dokta slaa alipotaja ile orodha ya mafisadi 11 pale mwembe yanga mlimshambulia sana.. Leo nanyi mnaimba wimbo wa ufisadi mpaka cag katika lipoti yake ameonyesha wzi anzia wizarani mpaka katika halmashauri (baraza la mawaziri limeshavunjwa mara ngapi tangu jk aingie,,, sababu hasa ni zipi)????

Ushauri wangu wewe bado ni mdogo sana... Angalia mbele uongo hudumu kwa muda mchache sana.. Angalia utakosa pa kujificha.... Hivi unajua shida zinazowakumba watanzania chanzo chake ni nii?? Huyo mwenyekiti wako hata hajui kwanini nchi anayoingoza ni maskin... Shame on you guyzzz...... Siku zenu zinahesabika,...... Manadhani mtaongoza milele.... Hahaaaaaaaaaaaaaaaa pole sana..... Imekufa kanu sembuse nyinyi mazinzi, wezi, wauaji.... Na walafi wa rasilimali za watanzania... Mmeifanya tanzania kama mali yenu.... Mtatueleza ....siku moja.... Endelea kujipa moyo....
 
Mambo tunayoyaona yakiipata CCM hayatokei kwa bahati mbaya bali ni Mpango wa Mungu kuwa katika meza yake kilio cha maskini wa kitanzania kimemfikia na ameamua kuwajibu waja wake kwa njia ya kukitoa madarakani CCM. anajaribu kuwaonyesha ishara nyiki zikiwamo za kutokubalika ili waanze kuji-adjust wasipate pressure 2015. Wao wameamua kuifanya mioyo yao migumu licha ya hizi dalili. Vitabu vitakatifu vinasema aishupazaye shingo yake na asione na kusikia atavunjika ghafla. Na hiki ndicho kinakwenda kuipata CCM na viongozi wake lets wait and see.
 
Nikiona hii sura na Hii rangi sijisikii vizuri tumbo linashikwa kuarisha ghafla

avatar11941_3.gif
 
Mwigulu Nchemba awe makini anapofunguwa mdomo wake otherwise atailetea serikali yake ya CCM kama ili iliyoletwa na Sophia Simba na Membe. Mwigulu anasema serikali ya Uingereza inaitumua CHADEMA kuleta ushoga nchini! Kama CHADEMA kuwa na urafiki na chama cha conservative ni tatizo, tuseme kuhusu serikali ya CCM inayopewa hela na serikali hiyo hiyo ya Uingereza chini ya chama cha Conservative? Nchemba anaweza kusema 25% ya bajeti ya serikali ya Tanzania inatoka wapi? Na serikali ya CCM wanapokea hela ili kueneza ushoga?

Mchumi class A hawezi kuwa insensitive kiasi hicho. The guy is senseless kwani ushabiki umemwondolea hata fahamu kidogo tu za kuelewa athari za maneno yake kwa JK ambaye anajidai kumpa support.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
We,jamaa ni muongo sana halafu unaweka post kwa kuongeza chumvi hata picha zako ulizoweka ziko Biased kiasi kwamba unaeneza propaganda kwa upenzi wako.Mi nilikuwepo na watu walikuwa wengi tu.Picha uliyopiga umechagua maeneo ambayo watu hawkupenda kukaa kwa vile kuna jua kali.Mbona hukupiga wale waliokuwa wamekaa kwenye yale matent?Pia sijaona uptodates zako aliyosema Aggrey Mwanri na umeamua kuyapotezea kwa makusudi kwa ajili ya Unazi wako.Mengine umesema sahihi kabisa yote aliyosema Mwigulu,Nape ingawa mengine ume-paraphrase.Jifunze kuongea ukweli na usidanaganye maana mi nilikuwepo kwenye mkutano na sina chama nilikuwepo hapo kusikia siasa ili niweze kuchuja na mengine ninayosikia.
 
We,jamaa ni muongo sana halafu unaweka post kwa kuongeza chumvi hata picha zako ulizoweka ziko Biased kiasi kwamba unaeneza propaganda kwa upenzi wako.Mi nilikuwepo na watu walikuwa wengi tu.Picha uliyopiga umechagua maeneo ambayo watu hawkupenda kukaa kwa vile kuna jua kali.Mbona hukupiga wale waliokuwa wamekaa kwenye yale matent?Pia sijaona uptodates zako aliyosema Aggrey Mwanri na umeamua kuyapotezea kwa makusudi kwa ajili ya Unazi wako.Mengine umesema sahihi kabisa yote aliyosema Mwigulu,Nape ingawa mengine ume-paraphrase.Jifunze kuongea ukweli na usidanaganye maana mi nilikuwepo kwenye mkutano na sina chama nilikuwepo hapo kusikia siasa ili niweze kuchuja na mengine ninayosikia.

mkuu, no research no right to speak. mwaga data na mapicha ili umprove skt one wrong na sisi ambao hatukuwepo mpanda tipate kufanya comparison. kusema tu jamaa ripoti yakeni biased hakusaidii kitu. lete hizdn picha za kwenye matent tuzione na nondo alizoongea mwanry.
 
Ahsante kwa update nzuri, umeelezea mpaka nimejiona kama nilikuwepo vile..
 
Back
Top Bottom