MartinDavid
JF-Expert Member
- May 22, 2009
- 874
- 144
Push-Up Anniversary! Ubishi Unaendelea.Sasa Leo Warudi hapa...!
Leo ni Mwaka Mmoja Tangu mgombea Urais wa CCM John Pombe Magufuli alipoongeza nguvu katika kampeni zake za Urais kwa kuaminisha watanzania kuwa Misingi ya Urais ni "Push-ups".Mimi nilikataa na nikatoa sababu nilipojibizana na Dr.Hamis Kigwangalla na January Makamba kwenye Makala za RaiaMwema.
Niliwatahadharisha kuwa tunatafuta Rais aliyetuna kwenye Brain na sio kwenye mishipa.Kijembe hicho kiliwaingia kisawasawa.Nikawaambia sisi UKAWA hatuwezi kuwajibu kwa Push-ups kwa kuwa hatumtafuti Sungusungu wa Taifa bali Rais wa Nchi hivyo tutajibu kwa hoja kuanisha sera na maono yetu kwa Tanzania Mpya. Natamani leo akina January na Dr.Kigwangallah waandike tena tufanye Tathmini leo .
Je,Urais ule uliotafutwa hadi kwa Push-ups umeweza kutoa suluhisho kwa matatizo na changamoto zinazolikabili Taifa? Kila siku huwa ninasema Maandishi Yanaishi.Kalamu ina nguvu kuliko Risasi
Baadae au Kesho nitaiweka makala ile hapa.
Sasa ni wakati wa kujitathmini
-Kwa ushupavu ule wa Push-ups za kampeni tumeweza kuanzisha au kusaini mikataba mingapi ya kujenga viwanda?
-Je tumeweza kugawa milioni 50 kila kijiji kama ilivyohubiriwa kwa nguvu za Push-ups?
-Akiba ya Fedha za kigeni inatosha?
-Demokrasia na Uhuru wa Maoni au Vyombo vya Habari umestawi au umesinyaa?
-Utawala wa Sheria imeshamiri?
-Umoja wetu kitaifa umeimarika kiasi gani?
-Hali ya Maisha na mzunguko wa fedha mitaani ukoje?
-Wanafunzi wanapewa elimu bora ?Vyuoni wanapewa mkopo wa kutosha na kwa wakati?
-Huduma za Afya zikoje?Hakuna wagonjwa wanaolala chini?
-Bandarini kuna mizigo ya kutosha na biashara zinaendelea vizuri? Taifa bado linapata mapato?
-Wafanyakazi walipunguziwa Kodi je punguzo lile lina unafuu wowote wakati gharama za maisha zipo juu?
-Uhusiano wetu na majirani zetu ukoje?
-Demokrasia imeshamiri kwa kiasi gani?
-Wanyonge waliokuwa wakiambiwa kwamba wamempata Rais wao hali zao za maisha zikoje?
-Hakuna wanaokandamizwa na kunyanyaswa?
-Maafa yale ya Kagera(Kulekule alikozindulia Pushups akishangiliwa) Serikali yake ilisimama na wananchi kwa haraka kiasi gani kuonesha faida za Ushupavu alioaminisha wa Push-ups? Alionesha huruma na utu kiasi gani kwa watu hawa kuonesha matunda ya maandalizi yake ya Push-ups ya kuutafuta Urais ?
-Tanzania katika Ramani ya Kimataifa tumesaidiwa kwa lolote na mchango wa Push-ups zile? Zimeweza kuvuta wawekezaji?
Nilitahadharisha kwamba misingi ya Urais sio Push-ups bali Falsafa,Itikadi,Sera ,Dira na Maono sahihi
Rais Bora hupatikana kwa kuegemea katika Misingi hiyo na atakua Rais Bora kitaifa na Kimataifa
Wiki iliyopita nilizua mjadala wa kumshauri na kumshinikiza Rais ahudhurie baadhi ya mikutano muhimu ya kimataifa.
Nikasema Mkutano huu wa Umoja wa Mataifa ni wa Muhimu sana kwani ndipo Rais angejipambanua kimataifa
Sera ya ndani(Domestic Policy) hufafanuliwa vizuri na kujenga haiba ya Taifa na Misimamo yake kimataifa katika sera(Foreign Policy) kupitia Balozi za nje na Mkuu wa Nchi anapokua katika mikutano kama hii
Nikasema ndio muda wa Tanzania kujadili suala la wakimbizi(Tunao Wakaimbizi kutoka Burundi), Agenda 2030 na Masuala Mengine
Sasa Rais wa Nigeria Muhhammaddu Buhari amehutubia Dunia kupitia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UNGA71) na katika Hotuba yake amefanya jambo tulilomshauri Magufuli juzi akafanye kule UN
Rais Buhari amejenga hoja kuwa katika kupambana na ufisadi kule Nigeria yeye na wananchi wa Nigeria wanazitaka nchi wanachama wa Umoja wa mataifa zitie saini mkataba wa umoja wa mataifa wa kupambana na Rushwa(UN Convention against Corruption) kwani bila hivyo Umaskini utaendelea kushamiri duniani kuwa fedha za maendeleo zinakwapuliwa na kufichwa nje ya nchi tena kwenye nchi ambazo zimetunga sheria zinazozuia wamiliki kutajwa au kuzuia fedha zao kurudishwa nchini kwao hivyo Wala Rushwa kulindwa
Akawaambia Wakuu wa Nchi na Serikali kuwa bila kufanya hivyo Umoja wa Mataifa hautafikia malengo yake miaka 14 Ijayo yaani agenda 2030
Niruhusuni nimnukuu kwenye nondo za Rais Buhari "Nigeria Will Continue to advocate for the facilitation of the recovery of illicit financial Assets.The Sustainable Development Goals underscore the imperative for our collective will towards finding enduring and sustainable solutions to addressing a global disparities.Corruption freezes development,thereby undermining the achievement of Sustainable Development Goals"
Hoja zake zimejengwa kifalsafa,Kiitikadi,Kisera na Kimaono
Kwenye Kampeni zake kule Nigeria alijenga hoja.Hakuzisindikiza kwa Pushups
Wakati Rais Buhari akihutubia kule New York City huku kwetu Rais Magufuli alifanya ziara za kushtukiza na kujikitita katika mjadala wa kujadili Chuma Chakavu kule ofisi ndogo za CCM Lumumba
Ni kweli Mtambo wa Kuchapa Magazeti ya Uhuru aliambiwa Uliuzwa kama Chuma Chakavu. Aliujadili,Sijamzushia
Tuendelee na Mjadala kwa Upole na Tumlindie Heshima Rais Wetu
A Luta Continua,Victory Ascerta.....