Mkutano wa 9 wa UVCCM, Dodoma: Rais Magufuli afuta bodi ya umoja wa Vijana! Awataka kutoogopa kujibu hoja za upinzani

Aiseee! Yaani leo Katambi anasema hakuna umuhimu wa kufuata demokrasia na kuzingatia haki za binadamu kwa kuwa ati “hakuna nchi inayofanya hivyo kwa asilimia 100”?

Mungu atupe nguvu watanzania. Maana, inasikitisha sana.
 
Vijana wa ccm wanajitahidi kuhakikisha "njia ya kwenda msalani haioti nyasi" (which is another way of saying "kuhakikisha mkono unaenda kinywani")
 
Mbona anawahusia sana kwa kutomchagua kiongozi wa vijana asiyewapa rushwa? Hii inaonyesha jinsi gani CCM inaongoza kwa kutoa rushwa. Yaani hata wenyewe kwa wenyewe hawa aminiani hii ni hatari.
 
Tangu nijiunge JF sijawahi kukimbia BAVICHA. Fuatilia thread zangu zote. Nikiingia tu hapa BAVICHA wanafyata mkia.
Mimi ni shock absorber na huwa nawatoa mapovu vijana wa BAVICHA kama hawana akili nzuri.
Kwa hiyo wewe ni damper?
 
Kuchukua hatua za kiutendaji kutokana na uwajibikaji mbovu wa wateule wake si frustrations,kiongozi makini hapaswi kuongozwa na hisia,anatakiwa kutenda haki,uki, iruhusu frustrations ziwe sehemu ya maamuzi yako kamwe hutoweza kuhukumu kwa haki.

Hakuna popote niliposhangilia,bali sikubaliani na sanaa za kiuongozi!Kusema umekamata vichwa vya treni visivyo na mwenyewe,baadae utuambie umekama magari yaliyoingizwa kwa anuani ya ofisi yako huku magari hayo yapo bandarini ksa zaidi ya miaka miwili hiyo ni sanaa inayovuka mipaka ya dunia hii!Ni sanaa zifanyikazo huko Jupiter.
Kwa comment yako ndiyo maana nilisema ulishangilia na bado unaendelea kushangilia kwa kuita ni SANAA
 
" Afadhali sana Shaka unajitahidi nasema haya toka kwenye nafsi ya moyo wangu unafanya kazi nzuri mungu atakusimamia" JPM mkutano mkuu wa 9 UVCCM Chuo cha Mipango Dodoma 10/12/2017
 

Attachments

  • VID-20171210-WA0810.mp4
    491.1 KB · Views: 38
Shaka aaminiki, kuna siku utamsikia aki idai CCM mabilioni ya hela kwa kumgeuza mtaji wao wa kisiasa.
 
Albert Msando aliomba nafasi kwa Rais Magufuli ili aweze kuwasema vijana wa CCM baada ya moja ya taarifa yao kusema wapo vijana wa CCM zaidi ya milioni sita jambo ambalo linapingana na taarifa zao wenyewe.

"Nimeazima taarifa ya utekelezaji na mpango mkakati naona mmesema kwamba UVCCM mpo milioni sita, je ni kweli? Kama vijana mtakuwa mnafanya mambo kama haya tutakuwa na nchi ya hovyo sana na chama cha hovyo sana, mmeandika takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya vijana wenye umri kati ya 14-35 ni asilimia 34 ya watu wote nchini. mara tu baada ya ukurasa wa nane, ukurasa wa tisa mmeandika kundi la vijana ni kubwa takwimu zinaonyesha sasa wamefikia asilimia 65 ya idadi ya watu nchini ina maana hatujijui tupo wangapi? alihoji Msando

Wakili Msomi Msando aliendelea kuonyesha mapungufu hayo ambayo yalikuwa na lengo la kumdanganya Rais John Pombe Magufuli

"Kwenye kitabu hiki mmemwambia Rais Magufuli kuwa vijana wa UVCCM mnafika milioni sita lakini kwenye jedwali la kweli mmeandika idadi ya vijana wa UVCCM kila mkoa 2013/2017 jumla walio hai ni milioni moja laki sita wasio hai ni laki nne sasa kwanini mumdanganye Rais? Tukafanye kazi na hizi ndiyo takwimu zenu sasa hivi mnamwambia Rais tunakaribia milioni sita mnataka Rais aondoke akiwa na picha ya kuwa mpo zaidi ya milioni sita wakati mpo milioni moja laki tano, jamani hatuendi hivyo tunakata CCM mpya ya vijana wachapa kazi, wanachama wote ambao hawapo hai warudi, tupate wanachama wapya" alisema Msando.
 
Back
Top Bottom