Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,639
- 22,490
Idara ya Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa tangazo la ajabu sana. Inasema kuna raia wa kigeni wanafanya kazi bila vibali vilivyotolewa kwa kufuata utaratibu.
Idara ya Kazi inasahau kwamba vibali hivyo vimetolewa na Idara ya serikali ya Tanzania, sio waajiri au waajiriwa wamejipa vibali. Sasa iweje Idara ya Uhamiaji itoe vibali bila kuzingatia taratibu, halafu serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu) iwalaumu waajiri kuajiri watu wa nje bila vibali vilivyofuata taratibu?
Pili, ni usumbufu mkubwa kutoa amri kwamba waajiriwa wote wa nje wanapewa siku 30 kufikisha vibali vyao, vilivyotolewa na serikali, kwa ajili ya ukaguzi. Hii ni kusababisha vurugu za kipuuzi zisizo na msingi hasa kwa watu wenye vibali vilivyofuata taratibu. Wazungu wanasema "poor management on your part should not constitute my crisis".
Vibali vya kazi kwa watu wa nje vinatakiwa viwe vya miaka miwili au mitatu, na kuwa renewed ikibidi. Kama Idara ya Uhamiaji wamefanya madudu kutoa vibali, walipaswa kutoa the benefit of doubt kwa hao waajiriwa na kufanya uhakiki pale wanapokwenda kurenew vibali vyao, sio kuleta emergency measures sizizo na pua wala mdomo kwa sababu ya uzembe wenu watu wa Idara ya Uhamiaji.
Hii mikurupuko ya serikali, hasa ofisi kubwa kama ya Waziri Mkuu inatia aibu. Kama kuna madudu yamefanyika watumbueni walioyafanya sio kusumbua watu waliofadika na uzembe wa serikali.
Hivi nyie watu wa Idara ya Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu mnajua hata ni watu gani nchini wanafanya kazi kwa vibali nchini, au mnajitamkia tu amri?
Mnamtia aibu Waziri Mkuu Kassim Majariwa ambaye tunamjua kuwa mtendaji makini sana.
NB: Suala la vibali vinahusu watu wengi sana katika nyanja nyingi sana - kuanzia kampuni za kutafuta gesi na mafuta kama Statoil; vyuo vikuu; mapailoti; aircraft engineers kutia ndani na hawa wanaowakilisha bombardier kama bado wapo; foreign investment projects; viwanda kama Dangote; mahoteli; mainjinia wa miradi ya serikali; mahospitali; taasisi za kidini; taasisi za misaada kama GIZ, DANIDA, SIDA, JICA, EU nk; Benki ya Dunia; EU Commission; idara za Umoja wa Mataifa; Idara za TV na Radio kama BBC and DW; Ofisi za Ubalozi; miradi ya ujenzi wa barabara; ma-ajenti wa kuuza magari; International schools, Mawakala wa clearing wa nchi kama Malawi, etc; Wasafirishaji kampuni za kigeni; Makampuni ya mafuta kama Engen; International NGOs, kampuni za meli, kampuni za ndege kama KLM, SAA, Turkish Airlines, Kenya Airways nk, wachezaji mpira, makocha, nk.