Mkurugenzi wilaya ya Busega acha kutunyanyasa waalimu

Mwamgunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
247
48
Leo nimeingia ktk ofisi ya mkurugenzi wilaya ya Busega ili kuomba anipitishie fomu yangu ya kuongeza mkopo katika benki ya NMB majibu aliyonipa ni kuniamuru nitoke ndani ya ofisi yake vinginevyo atanifatilia ili ajue shule ninayofundisha na hatua za kinidhamu zichukuliwe juu yangu, anadai waalimu tumekuwa wasumbufu pia hawezi kupitisha fomu ya mtu ambae tayari ana mkopo mwingine benki.

Swali la kujiuliza hivi tangu lini mwajiri akampangia mwajiriwa kiasi cha mkopo wakati nitakaeulipa huo mkopo ni mimi mwajiriwa?

Waalimu wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu tumechoka kunyanyaswa na ipo cku tu tutashindwa kuvumilia manyanyaso haya!
 
mkomeshe kwa kumwandikia barua ya kuacha kazi masaa 24 yaani twenti foo notice of rizainesheni, jongea simba wa yuda wale watasha wanalipa kinoma.
 
Duuuuh hayo hakika ni manyanyaso, poleni sana walimu na huo unyanyasaji...
 
Ndio mjue hii nchi bila mtu anatazama tumbo Lake,ingekuwa yeye ndio amefanyiwa hivyo angefurahi?Nchi hii bwana,alafu lawama zote analaumiwa rais Kikwete,kumbe ni watendaji
 
Yani mkurugenzi ndio anapitisha mikopo, wilaya nyingine ukipitisha kwa mkuu wa idara yani afisa elimu, inaenda idara ya fedha, halafu afisa utumishi anasaini kwa niaba ya mkurugenzi.
 
mkuu kuna waraka wa utumishi kuhusu kiwango cha kukopa huenda ikawa umevuka mwalimu
 
Umesikia mwenzake wa Chato anawalazimisha watumishi wakimbie mchakamchaka au wajifunze ugambo. kule Bukoba kuna yule anaewacharaza walimu bakora. kuna yule anaetoa uwalim ukuu baada ya kulamba uroda. Poleni watu wa huko. CHADEMA kitawakomboa tu
 
mkuu kuna waraka wa utumishi kuhusu kiwango cha kukopa huenda ikawa umevuka mwalimu

Hapana mkuu, hilo nalifahamu. Pia kabla cjafika huko nimeanzia benki nikapigiwa hesabu ndio nikaenda huko!
 
Hivi serikali ilipowawekea watumishi kiwango maalumu cha kukopa Ilikuwa inamaanisha nn kama si unyanyasaji? Hivi ni sahihi kunipangia matumizi ya pesa za jasho langu? mkopo nakopa mimi kwa shida zangu, nalipa Mwenyewe halafu serikali inanilimit kiwango cha mkopo kana kwamba itanilipia.

UNYANYASAJI SERIKALI ACHENI UDHALIMU
 
mkomeshe kwa kumwandikia barua ya kuacha kazi masaa 24 yaani twenti foo notice of rizainesheni, jongea simba wa yuda wale watasha wanalipa kinoma.

Kweli kabisa mkuu, huku manyanyaso yamezidi.
 
Huyo kapata nafasi hiyo kwa upendeleo he belongs to ukoo wa panya ndo mana haogopi kitu anafanya anavyo taka ukawa tumaini letu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hawa wakurugenzi watendaji wana matatizo sana karibia kila halmashauri katika nchi hii wanalalamikiwa wao? halafu ukute wengine walishawahi kuwa walimu kabla ya kufika hapo walipo ila hawakumbuki walikotokea....
 
Mwalimu wa Tanzania ni kibonde cha kumkandamiza kwa kila kitu, si ajabu mwalimu huyu yuko kwenye orodha ya walimu wanao idai serikali madeni mbali mbali na anapo taka kujikwamua kwa kutumia mkopo
 
Walimu tulieni. Umeandaliwa mpango kabambe wa kumchomoa pale. tulieni siku si nyingi atachomoka. si ajabu akajiuzupu mwenyewe. Kamera zimeshaandaliwa kama cctv vile.
 
Back
Top Bottom