Mkurugenzi wa Kituo cha Usaidizi wa Kisheria cha Everlasting Legal Foundation (ELAF), Dkt. Hamis Masoud, amelaani vikali lugha za uchochezi wa kidini, akisisitiza kuwa kama tunakwenda kwenye hatua ya maridhiano hatupaswi kutengeneza vita mpya ya migogoro ya kidini, akisisitiza kuwa Watanzania wanasimama kama taifa, wenye dini na wasio na dini wanaunganishwa na undugu ambao ni ubinaadamu
Akizungumza na waandishi wa habari, jana Novemba 23, 2025 katika makao ya Ofisi hizo jijini Dar es Salaam, Dkt. Masoud amesema mijadala ya Kitaifa inapaswa kuheshimu imani za watu wote, na si sahihi kutumia dini kama silaha ya kuudhalilisha au kuchochea migawanyiko katika jamii.
Amekemea matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa dini na wahadhiri ambayo yamekuwa yakihamasisha vurugu, ikiwemo vitisho vya mashambulizi kwenye nyumba za ibada
Amesema vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi, hususan sheria za makosa ya jinai, hivyo hatua kali zinapaswa kuchukuliwa mara moja ili kuzuia madhara makubwa kwa ajili ya amani ya taifa.
Dkt. Masoud ametahadharisha kuwa taifa linaweza kuingia katika migogoro ya udini endapo hatua za kisheria hazitachukuliwa kwa wakati, akisisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Aidha, ameitaka sekta ya umma kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia maslahi ya taifa, akibainisha kuwa mamlaka wanazoshikilia viongozi zinatokana na wananchi na lazima zitumike kwa uadilifu.
Amesisitiza kuwa lengo la kauli zake ni kulinda umoja, mshikamano na amani ya taifa, huku akiwakumbusha viongozi wote kwamba mamlaka hutoka kwa Mungu na yanapaswa kutumiwa kwa uangalifu mkubwa.
Dkt. Masoud amelitaka tena Jeshi la Polisi kuchukua hatua dhidi ya wote wanaotoa matamshi ya uchochezi wa kidini, akisema kuwa endapo Jeshi la Polisi halitachukua hatua stahiki, watamshauri Rais kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa usalama wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao