Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbarali ni amejaa matusi

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbarali ni amejaa matusi

wwww

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
350
Reaction score
252
WanaJF mtanisamehe kuipost hii threat hapa, nataka watu wengi waione.

Ndugu zangu kama kawaida yangu, nilikuwa na mapunziko mafupi kwetu Ubaruku na kama kawaida kabla ya kufika Ubaruku lazima upite Rujewa makao makuu ya Wilaya.

Nilipofika Rujewa kama kawaida yangu lazima nionane na rafiki zangu hapa ambao baadhi ni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali. Jamaa hawa walinidokeza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hii ndg. ADAM I. MGOYI amekosa kabisa utawala bora kwani anawatukana watumishi kama MBWA ambao hawafai kabisa machoni pake.

Matusi na maneno ya kukejeli watumishi wenzake yamekidhili kiasi kwamba sasa hapati kabisa ushirikiano na Wakuu wa Idara katika Halmashauri hii. Jamaa huyu anasema kwakweli hali ni mbaya hasa ukizingatia wanaotukanwa ni watu wazima, na watu wenye heshima katika jamii. Ananidokeza kuwa Mkurugenzi huyu anafanya mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi kwa kufanya yafuatayo;

1. Amegauza IJUMAA ni siku yake ya kwenda MSIKITINI hivyo kama kuna vikao vimepangwa siku hiyo basi wakuu wa Idara watasubiri mpaka saa 11:00 jioni atakapotoka Msikitini na kupumzika ndipo waanze vikao ambavyo mara nyingi wanamaliza usiku.

2. Siku ya JUMAPILI ameigeuza ni siku ya kazi kwa Wakuu wa Idara, ambapo huwa mara nyingi wanafanya vikao kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi usiku.

Mbaya zaidi huyu bwana ananidokeza kuwa siku ya JUMAPILI tarehe 13.01.2013 alipokuwa kwenye kikao na Wakuu wa Idara aliwafedhehesha sana Wakuu wa Idara wawili Ndg. Mwaikambo (Idara ya Biashara) na Mtalika (Meneja wa Mamlaka ya Maji - Rujewa) kwa kuwatolea watusi mazito na ya aibu kwa watu wazima kama wale kutukanwa mbele ya kundi la watu.

Chanzo cha matusi dhidi ya Mtalika ilikuwa ni kuchelewa kuingia kwenye kikao kwa dakika tano ambapo inasemekana alikuwa chooni kabla ya kuanza kikao hicho, alitukanwa na kufukuzwa kwenye kikao bila kupewa muda wa kujitetea. Wakati Mwaikambo alitukanwa alipokuwa akimweleza Mkurugenzi huyo kwamba anashindwa kutekeleza majukumu yake ya kwenda kufuata taarifa ya utendaji wa Kata aliyopangiwa kama mlezi ya Ukwavila ambayo ipo km 70 (barabara ya vumbi) kutoka Ofisi za Halmashauri kutokana na kukosa usafiri wa kwenda huko. Naambiwa Mkurugenzi huyo alimmiminia matusi huyu mzee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 59 kama mbwa koko, huku akimwambia apende asipende akakwenda kwa gharama zake yeye anataka taarifa kila IJUMAA ya Kata aliyopangiwa ambayo ni nje ya fani yake ya biashara. Inasemekana kila Mkuu wa Idara amepangiwa kuwa mlezi wa Kata, akiratibu kazi zote zinazofanywa na uongozi wa Kata, kazi ambazo ziko nje ya fani zao na ambazo kisheria zinapaswa kufanywa na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji.


Swali la kujiuliza hapa ni je: Mkurugenzi Mtendaji ana haki kisheria ya kumtukana mtumishi hata kama mtumishi huyo yupo chini yake? na je watumishi wanaotukanwa kila siku wafanye nini ili kuondokana na udhalilishaji wanaofanyiwa na huyu bwana?

 
malalamiko haya yapelekwe ofisi ya waziri mkuu ili huyo mkurugenzi achukuliwe hatua muafaka maana hawezi kuwadhalilisha watu wazima.
 
Hapa nimeona
~ heshima ya kazi hakuna ( uswali ijumaa, ila waj2 hakuna kusali kikaoni) mbaya sana
~ nawasiwasi na elimu yake ( ya maccm bhana juzi kwenye mkutano wa mwingulu manzese kulikuwa na katibu wa wilaya kinondon yani ukimuona tu unacheka sanaaaa hajielewi kabisaaaaaaaaaa)
~ Msikilize tu, utekelezaji wa maagizo yake hakuna kutenda ( kwani ata ukipeleka Tamsemi ni kazi bure tu watalindana tu)
~ Na mwisho M4C inakuja subiri atanyooka tu.....
 
Hapa nimeona
~ heshima ya kazi hakuna ( uswali ijumaa, ila waj2 hakuna kusali kikaoni) mbaya sana
~ nawasiwasi na elimu yake ( ya maccm bhana juzi kwenye mkutano wa mwingulu manzese kulikuwa na katibu wa wilaya kinondon yani ukimuona tu unacheka sanaaaa hajielewi kabisaaaaaaaaaa)
~ Msikilize tu, utekelezaji wa maagizo yake hakuna kutenda ( kwani ata ukipeleka Tamsemi ni kazi bure tu watalindana tu)
~ Na mwisho M4C inakuja subiri atanyooka tu.....
Kwanza inaonekana hiyo halmashauri haina baraza la madiwani pili akikutukana ni wajibu wako kuhakikisha harudii hiyo tabia tia makofi kisawasawa maana au tukana na wewe hawezi kukufukuza kazi maana kazi za umma heshima ni muhimu sio kama kwa muhindi
 
Ningekuwa mimi ni miongoni mwa watumishi wa Halmashauri, ningemtia adabu zaaaamaaani sana huyo mswahilina. Kwa nini wanamlea hivyo!!! Lengo lake mbona naliona lipo very clear. Any way, ngoja jamaa fulani akamate nchi ndipo cha moto wakione watu mufilisi kama hao.
 
Hao watumishi wapeleke malalamiko yao kwa DC, RAS, na TAMISEMI kwa hatua zaidi.
 
hao wakurugenzi wanashindwa kumrekodi huyo mtu wakarusha matusi yake youtube?
Walishamripoti mkoani?
Halafu mtu anakutukana si wamshushie kichapo akili imkae sawa????

Halafu isije kuwa ni kuchafuana tu?
 
Wanamfuga tu. Si na wao wajipe off ijumaa. Wawe wanaingia saa kumi. Mie mtu anitukane kwenye kikao, wallah narusha kiti.
 
Hao watumishi wamebebwa nini?
Kwani wanshindwa kurekodi hayo Matusi na kumfikisha mahAkamani?
Au ndio Akili ndogo kuongoza Akili ndogo.
 
Hayo ni maneno ya uchochezi tena ni kinafki, tunaomba ushahidi ya hayo uliowasilisha, kwa mtazamo wangu hapo kuna Ukristo na Uislam tubadilike jamani tuachane na mambo ya udini tufanye kazi kwa maslahi ya Umma!
 
Watumishi wa umma wengi wanahitaji maombi ya kufunguliwa ufahamu,si mbarali tu sehemu nyingi hawajui wanalofanya wananidhamu za uoga na unafiki kitu ambacho hata Mungu hapendi,amesema watiini wenye mamraka lakini sio muwaogope,halafu ukitoka pembeni unaanza kuteta Mungu hapendi tubadilike,na kijana kwenye Halmashauri ukianza kusimama kwenye kweli kutafuta ukombozi wanasema huyu MCHADEMA,yaani naipenda CHADEMA unajua kwa nini kila unapofatilia haki,kweli watawala wanasema wewe ni MCDM,kumbe jamani CDM wanapenda haki na kweli,though tutapata shida lakini vijana tupigane
 
Jamaa inaonekana kalewa madaraka...kama vipi mripotini kwa ofisi ya waziri mkuu........
 
Uwasilishaji mzuri sana, lakini nina wasiwasi kidogo kwani; mosi mtoa habari inaonekana ameambiwa na si wa kushuhudia mwenyewe, na mbili habari ni ya upande moja zaidi. Nafikiri ushahidi zaidi u nahitajika, otherwise unaweza kuona tunacomment majungu tu, hili ni wazo langu tu wanjf..
 
Back
Top Bottom