Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Bi. Zaipuna akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
5,004
4,113

===
Viongozi wakuu wa Benki ya NMB PLC wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wake Bi. Ruth Zaipuna, wamekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, wamempongeza Mhe. Naibu Waziri Mkuu huyo kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo huku wakimuahidi ushirikiano katika juhudi za kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo endelevu na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yake hayo mapya makubwa.



Tunapozungumzia kasi kubwa ya maendeleo endelevu ya Tanzania na Watanzania ni ngumu sana kuitengenisha benki hii ya NMB na Benki nyingine na mafanikio hayo, toka vijijini mpaka mjini, toka kwa wafanyabiashara wadogo mpaka wale wakati na hata mabilionea.

Mwanzoni na baada ya kuasisiwa kwake Benki hii ilidhaniwa kuwa hakuna mtoto wa Kitanzania anayeweza kuiongoza kwa tija na ndio kisa cha wazungu kuweka wazungu wenzao kwa kipindi kirefu.

Uthubuti mkubwa wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hii chini ya Mwenyekiti wake Dkt Edwin Mhede wa kumteua Mwanamama wa Kitanzania Bi. Ruth Zaipuna pamoja na Wasaidizi wake ambao pia ni wazawa imekuwa ni chachu ya mafanikio makubwa na yaharaka ambayo hata wazungu ambao ndio wenye hisa nyingi katika Benki hiyo naamini hawakuyatarajia,

Leo,baada ya safari ndefu ya Benki hii chini ya Uongozi wa wageni leo tunashuhudia watoto wa Kitanzania yaani Bi. Ruth Zaipuna na Dkt Dotto Biteko wakijadili na kupanga namna bora ya kulisaidia Taifa lao kwa pamoja ili Kila Mtanzania mwenye hitaji la Biashara na mwenye Sifa stahiki apewe mkopo kwa haraka na kwa riba nafuu.


...........Kazi iendelee..........
 
Uteuzi wa Dotto ni Uteuzi sahihi sana
 
Nahisi tu huyu dada atakuwa fiti kwenye brain
 
Benki kwa Tanzania ni NMB tuache maneno maneno. Mimi naipenda sana japo bado Sina pesa bado
 
Benki kwa Tanzania ni NMB tuache maneno maneno. Mimi naipenda sana japo bado Sina pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…