Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo George Nyatenga (Pichani chini).
Pia amewasimamisha kazi Wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.
Prof. Ndalichako amemwagiza Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali ahakiki maelezo na Nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.
Amewateua wafuatao ku Kaimu nafasi; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mteule ni Bw. Jerry Sabi kutoka Mzumbe University na Kaimu Mhasibu Mkuu mteule ni Bw. Daniel Mafie kutoka NECTA