Mkurugenzi Meru azuia posho za madiwani wa CHADEMA, atoa kwa Diwani wa CCM tu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MKURUGENZI wa halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri, amezuia madiwani wa CHADEMA wasilipwe posho na kuruhusu diwani wa CCM, alipwe baada ya baraza la madiwani kujigeuza kama kamati kwa lengo la kumjadili Mkurugenzi huyo kwa tuhuma za ufisadi wa mali za halimashauri hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani wa Halimashauri hiyo lililofanyika katika ofisi za halimashauri hiyo zilizopo Usariver,Wilayani Arumeru,mkoani hapa.

Baada ya madiwani hao kujigeuza kama kamati Mkurugenzi huyo aliamua kususia kikao hicho na kutoka nje pamoja na wakuu wote wa idara na vitengo wa halimashauri hiyo na ndipo alipoelekea katika ofisi za malipo za halimashauri hiyo na kumwamuru mhasibu wa halmashauri hiyo kutowalipa madiwani wote wa CHADEMA.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo, Willy Njau, alisema kuwa kwa muda mrefu sasa Mkurugenzi huyo amekuwa akidharau na kulipuuza baraza hilo pamoja na madiwani wake katika maamuzi yote yanayofikiwa katika baraza hilo.

Alizitaja tuhuma za Mkurugenzi huyo kuwa ni kuamua kununua gari jipya la mkurugenzi wa halimashauri kwa gharama ya shilingi milioni 140 kinyume na makubaliano ya baraza hilo ya kukarabati gari lililopo kwa gharama ya shilingi milioni 25 na kutumia milioni 55 kununua pikipiki26 kwa ajili ya watendaji wa Kata kinyume na maazimio ya baraza hilo yaliyolenga watendaji wakopeshe pikipiki kwa dhamana ya halmashauri hiyo.
 
haija ni suprise hiyo maana kawaida yao kutumia pesa kuminya haki
 
awacheleweshe posho watie njaa kwanza kama watamjadili.


diwani ni mtu mdogo sana kwa mkurugenzi ingawa wao wanajiita kanso!
 
Magufuri lazima ampandishe cheo huyo mkurugenzi, ,,muda simrefu atakuwa RC
 
Chadema mnataka mkurugenzi afe kwa ajali ya gari bovu mseme ni albadir?
 
ccm chama kinachojipambanua kwa haki kinakumbatia upumbavu....tutaona mengi uongozi huu...
 
Back
Top Bottom