Mkurugenzi manispaa ya Kinondoni ajipange

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,754
7,091
Leo ni siku ya wafanyakazi na kwa utaratibu uliozoeleka wafanyakazi wa kada zote hukutana pamoja kwa maandamano na hotuba mbalimbali.

Ili kufanikisha hili wakurugenzi hutoa nauli au usafiri kwa wafanyakazi kwenda eneo lililopangwa kukutana.

Leo hii mkurugenzi huyu kakataa kutoa usafiri au nauli kwa washiriki kiasi kwamba hakuna aliyekwenda kwani ni mbali na makazi yao.

Niulizieni, hivi ni nini anachowatafuta wafanyakazi walio chini yake?
 
Anabana matumizi...muache mkurugenzi afanye majukum yake kwa weledi na si ushabiki...
Kubana huko ni kwa manufaa ya nani? Na kama alilijua hilo ni kwanini basi awahamasishe wafanyakazi kwenda uwanja wa taifa?
Ni kwanini pia abane matumizi yeye peke yake ilihali manispaa nyingine wametoa nauli kwa wafanyakazi? Huku ni kujupendekeza kulikopitiliza.
 
Kwani ni kinondoni tu haijapeleka wawakilishi??

Mbona hata ofisi yetu haijapeleka mtu, je na sisi tumwajibishe boss wetu????
 
Kubana huko ni kwa manufaa ya nani? Na kama alilijua hilo ni kwanini basi awahamasishe wafanyakazi kwenda uwanja wa taifa?
Ni kwanini pia abane matumizi yeye peke yake ilihali manispaa nyingine wametoa nauli kwa wafanyakazi? Huku ni kujupendekeza kulikopitiliza.
Utakua na matatizo ww
Nahis haukuwa well informed..mara wawakilish mara taifa..whats yo point mkuu..au kun mishe zako zimefel nn..maana kwa povu hilo si kawaida
 
Si afadhali huyo amewaambia ukweli mapema. Kuna wenzenu walisafiri kutoka ruvuma hadi shinyanga kwenye sherehe za mwenge waliofika aliambiwa ageuze na waliomabararani waaliambiwa wa U-turn haraka kwa gharama zao.
 
Utakua na matatizo ww
Nahis haukuwa well informed..mara wawakilish mara taifa..whats yo point mkuu..au kun mishe zako zimefel nn..maana kwa povu hilo si kawaida
Binadamu kuwa na matatizo ni nature na binafsi siwezi kushindana nayo. Pia binafsi kuna mambo ambayo siwezi kuyaona kama binadamu bali binadamu wenzangu wanaweza kuyaona. Nakushukuru kwa kuyaona matatizo yangu lakini ukweli ni kuwa kuna utamaduni wa mwajiri kuwasafirisha wafanyakazi wake kwenda kwenye sherehe za mei mosi kila mwaka.
Kusema natoa povu ni kunikosea adabu na nademand kuombwa msamaha.
Kuwatetea wakurugenzi wa aina hii ni kuwakosea wafanyakazi walionyimwa nauli. Nakuuliza tena, ni kwanini abane matumizi peke yake ilihali manispaa nyingine wametoa nauli na maji ya kunywa?
 
Back
Top Bottom