Mkurugenzi Manispaa Sumbawanga unatesa Wananchi

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,464
37,711
Jana Kwa mara nyingine nimebahatika kuitembelea Rukwa na Sasa Niko stendi mpya ya mkoa nasubiri usafiri nirejee kwenye makazi yangu.

Kazi yangu ya Uandishi wa habari hasa zinazohusu mazingira kwenye Maziwa na Mito Mikoa Nyanda za juu Kusini inanifanya mara nyingi nifike Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe.

Nimefika Rukwa tangu juzi jioni na jana nikasafiri kuelekea Kasanga ambako nilikuwa na wito maalum.

Habari za kilichonileta naziacha hapa, lakini kama Mwandishi nimekutana na jambo linalolalamikiwa Sana na Wananchi wa mkoa wa Rukwa Kwa Sasa nami naomba niliwasilishe hapa Jamvini ambapo naamini litafika sehemu husika na Mamlaka zitaona namna Bora ya kuwasaidia Wananchi hawa wanaoteseka.

Stendi mpya ya Mkoa Sumbawanga imejengwa katika kijiji cha Katumba Azimio umbali wa km 14 toka stendi ya zamani ambayo ilikuwa katikati ya mji.

Kijiji cha Katumba kiko barabara kuu ya Sumbawanga- Mbeya uelekeo wa Mbeya. Kwa jiografia hiyo Wananchi wanaotoka Wilaya za Kalambo na Nkasi ambao wanafuata bidhaa mbalimbali Sumbawanga mjini au wale wanaofuata Matibabu ya rufaa Hospitali ya mkoa wanashuka stendi ya zamani na kiuhalisia hawana haja ya kwenda Stendi mpya umbali wa km14.

Lakini cha kushangaza Mkurugenzi wa Manispaa Sumbawanga ameweka utaratibu àmbao unawalazimu Wananchi toka wilaya hizo mbili kulazimika kwenda Stendi ya Katumba km 14 uelekeo wa Mbeya àmbako ndiko mabasi Madogo na ya Kati yanayofanya safari.

Yamelazimishwa kuanzia safari na yakitoka huko hayaruhisiwi kabisa kupitia stendi ya zamani iliyoko katikati ya mji na hakuna mahali pengine wanapopakia isipokuwa kijiji cha pili toka mjini kwenda Kalambo au Nkasi ambako naambiwa Kwa Boda boda ni sh. 2000-3000 na Bajaji ni 1000-1500.

Hivi Kwa akili ya kawaida tu achana na akili ya "Kisomi" anayotumia Mkurugenzi mwananchi anatokaje katikati ya mji kuelekea Mbeya akifikisha km 14 ndo anapata gari ambalo linamrudisha tena mjini km 14 jumla 28 halafu anakwenda Matai umbali wa km 35? Hii akili ya wapi Jamani hata kama mmesoma Sana na Sisi wengine hatujui lolote?

Ni sahihi stendi mpya zinaleta maendeleo kwenye miji, lakini Kwa nini mabasi yanayofanya safari za ndani ya mkoa yasiruhusiwe kupakia abiria stendi ya zamani ambayo bado ni nzuri na inatumika Kwa Sasa kushusha peke yake?

Kweli Mkuu wa mkoa wa Rukwa rafiki yangu Mkirikiti Umeshindwa kuliona hili na kumwacha DED Sumbawanga atumie ubabe kutesa Wana Rukwa? Ni akili gani ya kawaida (logic) aliyotumia Mkurugenzi kulazimisha watu wote hata wasiotaka au wasiokuwa na sababu ya msingi kusafiri km 28 ambazo hazina sababu?

Nirudi Kwa Chama cha mapinduzi wilaya hizi mbili, nyie ndo mnaisimamia serikali kwenye maeneo yenu, mmeshindwa kulifikisha suala hili CCM mkoa nao wakalifikisha mamlaka husika likapata ufumbuzi?

Hivi kweli 2024 na 25 mtarudi Kwa Wananchi hawa hawa wanaoteswa na maamuzi ya Mtu mmoja ambaye nyie mmeshindwa kumsimamia, muwaombe wawapigie Kura huku wakikumbuka gharama na mateso waliyoopitia Kwa miaka 4 nyuma?

Nanyi vyama pinzani mbali ya kunyimwa haki ya mikutano, mmeshindwa hata kutoa waraka kutetea watu wenu wanaowaunga mkono Kila siku?

Najua viongozi wa serikali na CCM mkoa hili haliwaumizi maana hamtumii usafiri wa Umma, lakini acheni ubinafsi mnatesa Wananchi.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wengine huwa wanafikiria na makalio sijui

Nafikiri stend ya zamani ya sumbawanga ingekua ni ya kushushia tu kwa mabasi makubwa na kupakia kwa mabasi madogo kwenda stendi mpya na kurudi stend ya zamani. Huwezi kumtoa mgojwa anayepelekwa hospital ya mkoa kumpeleka 14km halafu ndo arudishwe wakati hospital ipo 1km kutoka stend ya zamani sumbawanga. Huo ni unyanyasaji wa wananchi. Mfano mzuri ni stendi ya mbezi Dar watu wanaweza kushukia popote mjini gari inapopita ila lazima iingie mbezi stend.
 
Mambo hayo ni kero kwenye miji mingi mfano jiji la Dodoma na magari yanayotoka Mwanza kuelekea nyanda za juu kusini je kuna haja gani kwenda nanenane na kisha kurudi tena mjini na kuendelea na safari?kama ni ushuru wekeni utaratibu mzuri ila sio kusumbua wananchi bila sababu ya msingi
 
Bila shaka hujapandia gari Manispaa ya Songea stand kuu ni 28km kutoka mjini bodaboda ni elfu 14 au ikapungua kulingana na maelewano yenu, bajaji elfu 20.
Aisee..ndiyo kule shule ya tanga sijui?!.?
 
Jana Kwa mara nyingine nimebahatika kuitembelea Rukwa na Sasa Niko stendi mpya ya mkoa nasubiri usafiri nirejee kwenye makazi yangu.

Kazi yangu ya Uandishi wa habari hasa zinazohusu mazingira kwenye Maziwa na Mito Mikoa Nyanda za juu Kusini inanifanya mara nyingi nifike Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe.

Nimefika Rukwa tangu juzi jioni na jana nikasafiri kuelekea Kasanga ambako nilikuwa na wito maalum.

Habari za kilichonileta naziacha hapa, lakini kama Mwandishi nimekutana na jambo linalolalamikiwa Sana na Wananchi wa mkoa wa Rukwa Kwa Sasa nami naomba niliwasilishe hapa Jamvini ambapo naamini litafika sehemu husika na Mamlaka zitaona namna Bora ya kuwasaidia Wananchi hawa wanaoteseka.

Stendi mpya ya Mkoa Sumbawanga imejengwa katika kijiji cha Katumba Azimio umbali wa km 14 toka stendi ya zamani ambayo ilikuwa katikati ya mji.

Kijiji cha Katumba kiko barabara kuu ya Sumbawanga- Mbeya uelekeo wa Mbeya. Kwa jiografia hiyo Wananchi wanaotoka Wilaya za Kalambo na Nkasi ambao wanafuata bidhaa mbalimbali Sumbawanga mjini au wale wanaofuata Matibabu ya rufaa Hospitali ya mkoa wanashuka stendi ya zamani na kiuhalisia hawana haja ya kwenda Stendi mpya umbali wa km14.

Lakini cha kushangaza Mkurugenzi wa Manispaa Sumbawanga ameweka utaratibu àmbao unawalazimu Wananchi toka wilaya hizo mbili kulazimika kwenda Stendi ya Katumba km 14 uelekeo wa Mbeya àmbako ndiko mabasi Madogo na ya Kati yanayofanya safari.

Yamelazimishwa kuanzia safari na yakitoka huko hayaruhisiwi kabisa kupitia stendi ya zamani iliyoko katikati ya mji na hakuna mahali pengine wanapopakia isipokuwa kijiji cha pili toka mjini kwenda Kalambo au Nkasi ambako naambiwa Kwa Boda boda ni sh. 2000-3000 na Bajaji ni 1000-1500.

Hivi Kwa akili ya kawaida tu achana na akili ya "Kisomi" anayotumia Mkurugenzi mwananchi anatokaje katikati ya mji kuelekea Mbeya akifikisha km 14 ndo anapata gari ambalo linamrudisha tena mjini km 14 jumla 28 halafu anakwenda Matai umbali wa km 35? Hii akili ya wapi Jamani hata kama mmesoma Sana na Sisi wengine hatujui lolote?

Ni sahihi stendi mpya zinaleta maendeleo kwenye miji, lakini Kwa nini mabasi yanayofanya safari za ndani ya mkoa yasiruhusiwe kupakia abiria stendi ya zamani ambayo bado ni nzuri na inatumika Kwa Sasa kushusha peke yake?

Kweli Mkuu wa mkoa wa Rukwa rafiki yangu Mkirikiti Umeshindwa kuliona hili na kumwacha DED Sumbawanga atumie ubabe kutesa Wana Rukwa? Ni akili gani ya kawaida (logic) aliyotumia Mkurugenzi kulazimisha watu wote hata wasiotaka au wasiokuwa na sababu ya msingi kusafiri km 28 ambazo hazina sababu?

Nirudi Kwa Chama cha mapinduzi wilaya hizi mbili, nyie ndo mnaisimamia serikali kwenye maeneo yenu, mmeshindwa kulifikisha suala hili CCM mkoa nao wakalifikisha mamlaka husika likapata ufumbuzi?

Hivi kweli 2024 na 25 mtarudi Kwa Wananchi hawa hawa wanaoteswa na maamuzi ya Mtu mmoja ambaye nyie mmeshindwa kumsimamia, muwaombe wawapigie Kura huku wakikumbuka gharama na mateso waliyoopitia Kwa miaka 4 nyuma?

Nanyi vyama pinzani mbali ya kunyimwa haki ya mikutano, mmeshindwa hata kutoa waraka kutetea watu wenu wanaowaunga mkono Kila siku?

Najua viongozi wa serikali na CCM mkoa hili haliwaumizi maana hamtumii usafiri wa Umma, lakini acheni ubinafsi mnatesa Wananchi.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Umeiandika Kishabiki. Baada ya malalamiko ya Wananchi ulimuona Mkurugenzi kumuulinza kuhusu hili ili kubalansi story yako??
 
Umeandika kitu Cha msingi sana kwa kasi ndogo ya ukuaji ya mji wa Sumbawanga hakukuwa ulazima wa kutanua stendi kupeleka nje ya mji.
NB.Mkoa wa Rukwa haujawahi kupata viongozi wenye nia ya dhati ya kupigania maendeleo Kila kitu hovyohovyo tu elimu hatufanyi vizuri,RC umeshindwa kusimamia ipasavyo kumalizia ujenzi wa chuo cha VETA huko Katuma.
Wakazi wa Rukwa nanyi mmezidi upole mno huu ujinga huwezi kuukuta mikoa km Arusha na Kilimanjaro.
 
Bora useme wewe, hata ile ya Kanondo ni taka taka kabisa, mkurugenzi mwenyewe ukimuona kama upstairs hamna kitu
 
Kwakweli stand kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Rukwa iko mbali na pili bado hakuja andaliwa utaratibu wa uhakika wa usafiri kama unahitaji kwenda stand hasa kama una safari Alfajiri. Unakuta daladala hakuna na bajaji mida hiyo hakuna, unalazimika ulale stand ili usiachwe na mabasi. Kuna usumbufu mkubwa sana
 
Wamiliki wa mabasi ndio wanapashwa kujiongeza ili wasismbue abiria..

Hawana budi kuwa na private parking zao ktkt ya mji ili kuepusha adha hiyo ...

Iringa , Dar, Ruvuma na miji mingine wanafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom