Mkurugenzi HESLB apata kigugumizi kuitambua barua inayosambaa mitandoni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,849
Kufutia kusambaa kwa barua inayodaiwa kuwa ni ya kutoka Bodi ya Mikopo inayohusu Bodi hiyo kusitisha ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nje ya nchi(China), gazeti la Mtanzania lilimtafuta Mkurugenzi wa Bodi hiy ili atoe ufafanuzi wa jambo hilo.

Hii hapa chini ni sehemu ndogo ya habari hiyo kama ilivyoandikwa na gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 29/12/2016:

MTANZANIA lilimtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa HSELB, Badru ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hilo.

“Siwezi kusema ndiyo ni ya kwetu au hapana kwa sababu barua hiyo sijaiona, kwanza bodi haina utaratibu wa kuweka barua kwenye mitandao ya kijamii.

“Kama ina taarifa yoyote inataka kuitoa huwa inatumia utaratibu wa kawaida wa utoaji taarifa na kama kuna umuhimu kuweka kwenye mitandao ya kijamii ndipo huweka,” alisema Badru.

Chanzo: Mtanzania
 
Huyu mtafiti wa malaria alie kazini ana shida sana!! Subiri tuone mwisho wa episode hii nayo.......!!! Ameingia na jazba zake tuone mwisho wake Utafikia wapi!! Wa Kitengo kazini
 
Iko wapi hiyo barua tuidadavue?
Huna uwezo huo!

Haya jana niliyasema kule kwenye uzi wenyewe kwamba mamamanina haya hayachelewi kuja kukanusha hapa na nikatao muda mpaka kufikia leo mchana tutakuwa tumepata kanusho, sasa yako wapi?
 
Back
Top Bottom