Tangia mwwka 1996 Mkurugenzi wa gaming board Mr. Abbas Tarimba ni huyo huyo je ni kwanba hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kuwa Wakurugenzi! Mbaya zaidi Makampuni ya casino yanaleta wafanyakazi kutoka nje na kulipwa mishahara mikubwa kuliko wazawa kwa kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya, huku wazawa wakifanya kazi bila kuwa na Mikataba ya kazi mfano mzuri ni pale Princess Casino IT Plaza.
Mtanzania anafanya kazi kwa miaka miwili bila kupewa mkataba, je huyu mkurugenzi hayaoni hayo, hakuna chombo maalum cha ukaguzi wa mashine zao kama ifanyikavyo nchi za nje wanaset kwa kuwaibia watanzania bila kuwa monitored!
Tunaomba Magufuri aliangalie hili kwa manufaa ya watanzania na nchi upande wa kodi.