Mkurugenzi Gaming Board atabadilishwa lini?

Mkurugenzi Gaming Board atabadilishwa lini?

hotstoryg

Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
18
Reaction score
14
Tangia mwwka 1996 Mkurugenzi wa gaming board Mr. Abbas Tarimba ni huyo huyo je ni kwanba hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kuwa Wakurugenzi! Mbaya zaidi Makampuni ya casino yanaleta wafanyakazi kutoka nje na kulipwa mishahara mikubwa kuliko wazawa kwa kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya, huku wazawa wakifanya kazi bila kuwa na Mikataba ya kazi mfano mzuri ni pale Princess Casino IT Plaza.

Mtanzania anafanya kazi kwa miaka miwili bila kupewa mkataba, je huyu mkurugenzi hayaoni hayo, hakuna chombo maalum cha ukaguzi wa mashine zao kama ifanyikavyo nchi za nje wanaset kwa kuwaibia watanzania bila kuwa monitored!

Tunaomba Magufuri aliangalie hili kwa manufaa ya watanzania na nchi upande wa kodi.
 
1989 alikuwa pale (wakati huo Bahati Nasibu ya Taifa) akiwa msaidizi wa mzee Mussa (RIP)... Duu! Mpaka leo kweli amebobea ..
 
Kwanza hiyo ni kamali na Abbas ni muislamu hivyo ni haram kuongoza .
 
Taasisi imekuwa kama mali yake binafsi..anachagua nani amwajiri na nani asimwajiri..Ukifuatilia kwa karibu udini,ujamaa,urafiki,u yanga na undugu vimetawala mno....

GBT haina tofauti na NSSF.Yasemekana pia Ndugu Tarimba alikwishastaafu kwa mujibu wa sheria ila kwa sababu za pengo kutozibika ikiwa angeondoka kurudi uraiani Mh.Prof wa Msoga alimwongezea muda tena kwa msingi kuwa hakuna kama yeye...

Ni wakati mwafaka kurekebisha mfumo mzima wa uteuzi na usimamizi wa taasisi za umma..zinageuzwa taasisi binafsi za wakurugenzi wakuu hasa wanapokaa kwa muda mrefu..wanageuka miungu watu..bodi zinakuwa vibogoyo sababu ya maslahi na posho za kifisadi...

JPM katika ubora wako fungua macho na choma mchwa wa ubinafsi,undugu,ujamaa,urafiki ktk usimamiaji wa rasilimali za taifa...
 
Huyu naye ni jipu linasubiri kutumbuliwa. Pale kumejaa waislamu sababu yake. Hizi betting shops zote sidhani kama wanazifuatilia
 
Mkurugenzi abadilishwe au hyo bodi ifutwe kabisa,kwan ina faida gani kwa mtanzania wa kawaida aliyeko kule butuguri musoma?
 
Tangia mwwka 1996 Mkurugenzi wa gaming board Mr. Abbas Tarimba ni huyo huyo je ni kwanba hakuna watanzania wengine wenye sifa ya kuwa Wakurugenzi! Mbaya zaidi Makampuni ya casino yanaleta wafanyakazi kutoka nje na kulipwa mishahara mikubwa kuliko wazawa kwa kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya, huku wazawa wakifanya kazi bila kuwa na Mikataba ya kazi mfano mzuri ni pale Princess Casino IT Plaza.

Mtanzania anafanya kazi kwa miaka miwili bila kupewa mkataba, je huyu mkurugenzi hayaoni hayo, hakuna chombo maalum cha ukaguzi wa mashine zao kama ifanyikavyo nchi za nje wanaset kwa kuwaibia watanzania bila kuwa monitored!

Tunaomba Magufuri aliangalie hili kwa manufaa ya watanzania na nchi upande wa kodi.

Huwezi kumtoa mtu kama hana kosa.Chini ya tarimba michezo ya kubahatisha imekua ikiongeza pato la taifa kila mwaka hasa kupitia vat.
Suala la kuajiri wageni kwenye casino sio la Tarimba,peleka malalamiko kwa lamishna wa kazi ndie anaidhinisha uhamiaji kutoa vibali
 
Huyu naye ni jipu linasubiri kutumbuliwa. Pale kumejaa waislamu sababu yake. Hizi betting shops zote sidhani kama wanazifuatilia
Kama wana sifa sioni tatizo.ushazoea kuona wachaga tpa na tra sasa wamefutulanya
 
Mkurugenzi abadilishwe au hyo bodi ifutwe kabisa,kwan ina faida gani kwa mtanzania wa kawaida aliyeko kule butuguri musoma?

Mkuu hela ya bahati nasibu inatumika sana kuokoa jahazi wakati wa maafa.shirika hili lipo chini ya wizara ya fedha na muda wote lina pesa ya makusanyo ya kamari
 
Huyu naye ni jipu linasubiri kutumbuliwa. Pale kumejaa waislamu sababu yake. Hizi betting shops zote sidhani kama wanazifuatilia
We maku waislam sio watu? Ndio maana nyie wagalatia msio na akili mkarogwa
 
Ninyi mnafikiri pesa za Uchaguzi wa CCM zinatoka wapi? ... Acheni kucheza Kamari ...
 
Duu 2007 pilika za maisha nilikuwa na kibali cha kufanya kaz casino Hapo m n mtz na kilitolewa mwenyekit akiwa huyo jamaa kumbe had Leo nishaachana na hizo mishe yeye bado mwenyekit,wammilikishe tu hiyo bodi kama Hashimu lundenga na miss Tanzania iwe yake moja kwa moja ,maana hata Dr lick angetufaa hapo kama tff imeshindwa kumtumia
 
Tukilejea historia yake,Je alipokuwa Rais wa Club ya Yanga alifanikiwa?Je ktk kiti cha Udiwani pale Kinondoni Hananasif amefanikiwa kwa kiwango gani?Je amefanikiwa kwa kiwango gani akiwa mweka hazina wa CCM Dar es salaam na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM?..na ni kweli ana weredi wa kutosha kuendesha sekta husika ktk mazingira ya utandawazi na Changamoto lukuki za Utakatishaji fedha haramu kupitia Casino?Kaupata wapi na lini?Je tuhuma za kuifanya taasisi kama mali yake binafsi ni za kweli?..
 
Mkurugenzi abadilishwe au hyo bodi ifutwe kabisa,kwan ina faida gani kwa mtanzania wa kawaida aliyeko kule butuguri musoma?

We Ni taahira, nimepitia michango yangu huku jamvin nkaona uwezo wako ulivyomdogo...kalume kenge
 
Baada ya kufuatilia kwa kina juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nimekutana na yafuatayo:

Licha ya umri mkubwa ndugu Tarimba Abbas ni mtendaji anaejituma/anaejitoa kujenga taasisi imara na endelevu na yenye tija kwa taifa;Amekuwa akijiendeleza kimasomo mara kwa mara ndani na nje ya nchi kwa vipindi tofauti hivyo kuhitimu shahada kadhaa mfano Degree ya Sheria,n.k;Amejitahidi sana kusimamia maadili na weredi wa majukumu ya taasisi husika kwa kiwango cha kuzuia ubabaishaji na ukiritimba ktk michezo ya kubahatisha..

Mfano:Alisimama kidete nyakati za Jackpot Bingo kwa kusimamia taratibu na sheria hivyo kutoyumbishwa na ukwasi au hadhi za wahusika,N.k .

Mapungufu:Kwa wakati mmoja au mwingine Kujihusisha kwake na masuala ya kisiasa na michezo hasa mpira wa miguu kumemfanya ajigawe hivyo kupwaya upande mmoja kwa namna moja au nyingine hivyo kushindwa kutimiza malengo mahsusi kitaasisi.Kutokana na faida kadhaa zitokanazo na vyeo na madaraka Katika siasa na michezo kuna uadui mwingi unaohusisha kupigania fulsa za madaraka/vyeo hivyo kujikuta akiandamwa na mahasimu wa kimadaraka ktk utumishi wa umma,siasa na michezo.
Mapungufu mengine ya kiutendaji ni ya kimfumo kitaifa zaidi kama ambavyo yanaonekana ktk taasisi nyingi ambapo viongozi wakuu wa taasisi za umma wamekuwa na madaraka makubwa sana kiutendaji hivyo kuwa na uwezo wa kuingilia idara zote chini yao na kutoa dira ya maamuzi kiutekelezaji {Ajira,Manunuzi,fedha,n.k}.Upatikanaji wa katiba mpya yenye tunu ya miiko,maadiri na uwajibikaji wa viongozi ni suruhisho la kudumu kuondoa mfumo uozo wenye nidhamu ya kulindana,kubebana,kufumbiana macho.

Waendesha na wacheza michezo ya kubahatisha {Gaming,Casino,kubet} duniani kote ni watu wenye ukwasi mkubwa sana japo hata wa kipato cha chini wamekuwa wakishiriki japo si kwa kiwango tegemezi kimapato.Mfano mzuri ni Las vegas,Macau ambako ni kiini cha michezo ya kisasa ya bahati nasibu au kamari..kwa msingi huo sekta husika inahitaji ueredi kwa kina,uzoefu,umakini na kutoyumbishwa na waomba leseni za kuendesha michezo husika sababu wimbi la utakatishaji fedha haramu {madawa ya kulevya/mauzo ya siraha/ufisadi ktk mataifa maskini} limekuwa likishamili kupitia michezo husika.

USHAURI:Watumishi wa Umma waandamizi wawe na utaratibu wa kuwa groom /kuwakuza/kuwajenga/kuwalea viongozi watalajiwa ama wa baadae ktk taasisi zao mapema ili kuepuka kukosa viongozi makini mara baada ya walio ktk madaraka vipindi vyao kukoma..Mfano kiongozi au mtendaji aliebakisha miezi sita hapaswi kupekekwa kwenye training ya Capacity Building au Strategic Sensitization yenye lengo la kimatokeo baada ya miaka 2..

Bodi za wakurugenzi za mashirika ya umma zitengenezewe mfuko maalum wa kusimamia posho na stahiki zingine hivyo zisilipwe posho tokea ktk mashirika husika kuepusha upofushaji wa macho yenye rutuba kiufahamu na usimamizi

Hitimisho:
Tusiwe tunapost thread zenye chembe chembe za chuki binafsi baina yetu na walengwa wa thread husika..tutafiti kwa kina,tutathmini kwa kina na kuwa na ushahidi juu ya chechote tunachotupia..Platform hii inagusa wengi na mengi kutendewa kazi kijamii,kitaifa na kimataifa
 
Back
Top Bottom