Mkurugenzi feki wa TAKUKURU jijini Mwanza atiwa mbaroni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU ) mkoani Mwanza imemkamata mkazi wa nyakato national jijini Mwanza Simon Jumbe kwa kosa la kujifanya Mkurugenzi wa taasisi hiyo mkoani humo na kujipatia zaidi ya shilingi milioni 4 kutoka kwa watu mbalimbali kati ya mwaka 2008 hadi kufikia aprili 8 mwaka huu.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale, amesema mtuhumiwa huyo maarufu kama Simon Chomba ni mara yake ya tatu kukamatwa na maafisa wa TAKUKURU kwa kosa la kuwatapeli watu 13 aliokuwa akiwahaidi ajira ndani ya taasisi hiyo pamoja na kujifanya mtumishi wa TAKUKURU, jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 36 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mbali na matukio ya kuchukua fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 4 laki mbili na themanini na nne elfu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu,makale amesema chomba pia amekuwa akitumia cheo hicho cha Mkurugenzi wa TAKUKURU mkoa kujipatia huduma ya bure zikiwemo za kunyoa kwenye saloon, kitoweo cha samaki kutoka kwa wafanyabiashara na sehemu nyingine nyingi zinazotoa huduma kwa jamii.

Mtuhumiwa alikamatwa aprili 8 mwaka huu na maafisa wa TAKUKURU baada ya kuomba pesa kutoka kwa wananchi wawili kiasi cha jumla ya shilingi laki saba na elfu thelathini ili aweze kuwapatia kazi akijifanya kuwa ni Mkurugenzi wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza, ambapo mtego uliandaliwa mtego wa shilingi 100,000 ambao ndio ulifanikisha kukamatwa kwake.

Mtuhumiwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi na kupewa kesi namba 75 ya mwaka 2017 iliyopo mbele ya Hakimu Chuma. Mshitakiwa amesomewa mashitaka 13 na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Meela Mwema, hata hivyo amekosa dhamana na amerudishwa rumande hadi Aprili 19 mwaka huu kesi hiyo itapotajwa tena.

Chanzo: ITV
 
Regional TAKUKURU director unapiga rungu mpaka kwenye kitoweo, salons.
Hao waliotapeliwa na huyo mtu kama wametunukiwa shahada wapokonywe, maana akili yao haiendani na vyeti vyao.
Mkurugenzi wa TAKUKURU MKOA hulipwa si chini ya milioni 3 iweje ashindwe kulipia samaki badala yake anapiga rungu.
Bodaboda tu hawezi kujishusha mpaka atake kunyolewa bure.
 
Na hao waliokuwa wanatoa fedha wakamatwe...wanaonyesha dalili zote za kushiriki kutoa rushwa! Kwa sababu, hakuna utaratibu unaotaka anayehitaji kujiunga huko kutoa fedha tena bila hata kudai risiti ya serikali ya malipo halali
 
Ni regional bureau chief/RBC na si mkurugenzi kwa mikoani yaan kamanda wa takukuru mkoa
 
Ni regional bureau chief/RBC na si mkurugenzi kwa mikoani yaan kamanda wa takukuru mkoa
 
Hahaaaaa nchi ngumu hii. Jamaa anapiga hadi Vitoweo? Kweli mkurugenzi wa PCCB
 
Back
Top Bottom