digalangosha
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 1,574
- 2,295
Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma mji umekushinda mkuu. Naomba kuonesha interest mimi ni mdau wa usafirishaji.
Tuanze na ishu ya stendi kuu ya mabasi ya kwenda mikoani, mh. Rais huyu mkurugenzi ndugu kunambi toka umetuletea Dodoma alianza mgogoro na shirika la reli ambao ndio wamiliki wa eneo ilipojengwa stendi, lakini kutokana na ukilitimba wa huyu mkurugenzi kunambi amesababisha mahusiano ya TRL na manispaa kuvunjika na hivo TRL kudai eneo lao na hivo kupelekea kuvunja stendi na baadhi ya biashara zilizokua zimezunguka eneo hilo.
Pili, mkurugenzi huyo huyo ameisababishia serikali hasara kubwa kutokana na kujenga ukuta na jengo la maofisi stendi hapo ambalo leo hii ni useless kutokana TRL kuchukua eneo lao.
Tatu, mkurugenzi huyu huyu anayejiita magufuli mdogo kutokana na kuaminika kuwa na uhusiano mzuri na Rais amesababisha hasara kwa kuvunja bar ya chako ni chako kimakosa na sasa serikali inalazimika kulipa fidia.
Nne, mkurugenzi huyu alikataza mabasi ya mikoani kutokupakia abiria katika stendi binafsi hisipokua stendi mpya ya nane nane, lakini katika kampuni zoteee kampuni ya mabasi ya mbunge wa gairo ndugu SHABIBY mabasi yake yanapakia abiria mjini na hakuna mamlaka inayomgusa wala kunambi kuongelea swala hilo. Je kuna nini kati ya shabiby na mkurugenzi...?
Tano, kunambi anajitapa kwa kusema hata RC wala DC hawana uwezo kama aliokua nao kutokana na kujuana na Rais.
Sita, serikali ilirekebisha viwanja vya mashujaa pale mjini kwa gharama hili maadhimisho ya siku ya mashujaa yawe yanafanyikia hapo, leo hii pamefungwa kutokana na eneo kuwa chini ya railway.
Saba, stendi anayosema mpya hiyo ya nane nane hakuna hata jengo la abiria hata la kujengwa kwa makuti tu, choo ni shidaa, hakuna umeme na analazimisha mabasi yalale hapo, hakuna maji..
Nane, mhe. Rais najua umeenda Dodoma jana nimepishana na wewe ihumwa naomba ukiwa unaenda mjini ingia hapo nane nane usikie kero kuliko huyu mkurugenzi hawe anakuletea report iliyopikwa.
Mh. Rais kama unapitia JF au watu wako wa karibu naomba uangalie mwenendo wa mkurugenzi huyu maana kuna tetesi za wenye mabasi kufanya mgomo soon na huyu mkurugenzi hana nia yakuingilia kati.