Kasheshe
Tatizo siyo Mkulo, tatizo ni JK. Mwezi Februari wabunge walimwambia awateme Dr. Mponda na Dr. Nkya, akasema NO.
Sakata la Jairo mpaka leo hii hakieleweki, wabunge wake hao hao wa CCM ndio walipeleka hoja, wakachunguza na kutoa maazimio, je, amefanyia kazi hayo maazimio mpaka leo?
Madudu makubwa kama hayo, Mkulo hawezi kuyafanya bila nod kutoka kwa Ikulu. Pia haiwezekani kuwe na ufisadi wote halafu Ikulu iwe kimya. Report aliyokuwa nayo Deo Filikunjombe iko mezani kwa JK siku nyingi sana.
Hapa kuna maswali mengi sana yanayoibuka. Kwanini JK anakuwa na kigugumizi cha kuwang'oa? Mwezi Februari walisema kwamba Dr. Mponda aliandika barua ya kujiuzulu, lakini JK hakukubali.
Hili sakata linanikumbusha sakata ya Richmond, watendaji wa serikalini ambao walitakiwa kuchukuliwa hatua wote waliondoka kwa amani na wengine bado wako serikalini wanadunda. Ukishaona hivyo, maana yake ni kwamba Ikulu nayo ilihusika na wanaogopa wakichukua hatua yoyote ile kwa wahusika inaweza ku-backfire.