Mkubwa Fella amuonya Temba

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,236
2,000
Temba.jpg


Aliyekuwa Meneja wa Yamoto Band na Meneja wa Mkubwa na wanae, Said Fella 'Mkubwa Fella' amefunguka na kumuonya mmoja wa wasanii wake Mhe. Temba kuhusu aina ya nyimbo na tungo ambazo huwa anaziimba kwenye muziki wake.


Fella amesema hayo wakati akimpongeza Chege Chinguda kwa video yake mpya 'Kaitaba' ambayo imefikisha watazamaji milioni 1 kupitia mtandao wa YouTube, Said Fella amesema kuwa sasa Temba amemaliza chuo hivyo yupo tayari kwa ajili ya kuleta kazi nyingine ila amemuonya juu ya kuimba matusi na kusema akijaribu kufanya hivyo kipindi hiki basi atafungiwa.

"Mwanetu kamaliza chuo Mhe. Temba nae inabidi aje na ikibidi tuwambie wadau wafikishe ngoma town, wadau mbabe wa mdomo Temba washawasha anajiandaa akifika tunaomba support yenu muhimu sana naamini atabadilika na upepo ulipo kwa vijana na nimemwambia unajua muziki wa sasa awataki iyo iyo nini ipo apo down utafungiwa" alisema Fella

Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekuwa likifungia nyimbo pamoja na wasanii ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu kwa kutoa nyimbo ambazo wao wanaona ni kinyume na maadili na utamaduni wetu. Hivi karibuni zaidi ya nyimbo 10 zilifungiwa kutopigwa kwenye vituo vya Radio na TV.

Chanzo: EATV
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
9,125
2,000
Hahaaa temba bila matusi kweli? Ila kiukweli temba napenda sana nyimbo zake zinaamsha amsha ya kipekee!!
 

denoo49

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
6,107
2,000
Bwana Meneja aliishia wapi tena kwenye kutoa single zake, sambamaba na yule ajuza wao wa TMK?
 

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
10,256
2,000
Kweli elimu haina mwisho, Temba kamaliza chuo akiwa miaka 48! Ngoja na mimi nianze form one.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom