Mkopo wa Ujenzi-Nyumba za Biashara

Mkopo wa Ujenzi-Nyumba za Biashara

HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
3,926
Reaction score
6,671
Habari wadau.
Kwa mwenye idea na mikopo ya ujenzi wa nyumba za Biashara.. Naomba ushauri.

Nina eneo ambalo tayari kuna nyumba 2 ambazo kwa sasa zipo kwenye hatua za mwisho niingize wapangaji.

Nikiwa naendelea na hili nikapata wazo kama kuna bank inayo toa mikopo ya aina hii,kwa riba nafuu. Naombeni uzoefu wenu tafadhali.

Karibuni wadau kwa ushauri.
 
Angalizo tu

Angalia bank wasijeiishia kupiga mnada nyumba zako zote mikopo nayo ni ya kwenda nayo kwa akili
 
Nyumba za kupangisha ukiwa kwenye prime area zinalipa ila kwa jinsi uchumi wa katikati ulivyoyumba kipindi hiki , tafakari kwanza usije kujiingiza kwenye umasikini hohehahe
 
Shukrani
 
Kwa mfano Bank wakijiridhisha kiwanja chako na thamani ya jengo zinafika walau robo ya mkopo unaouhitaji...au la una chanzo kingine cha mapato kinachowahakikishia wao kupata pesa yao basi kazi haitokuwa ngumu.

Muhimu na la msingi kwao ni pesa yao kurudi na si ushawishi wako Mteja kuwa utapata M/Wapangaji ili ulipe mkopo.

Kuna jamaa yangu Mwaka juzi kapata milioni mia ya kuongeza/kukarabati nyumba ili apangishe coz alikidhi hivyo vigezo....kiwanja peke yake kilikuwa kinathaminika kwa 170m (prime area hata wakitaka kuuza hawatosumbuka)+nyumba+Kipato chake kwa mwezi.

Hivyo fanya tathmini kwa hayo kulingana na kiwango unachohitaji, ukiona unakaribia basi nenda Benki nao watakushauri.
 
Back
Top Bottom