Mkono wa buriani wa mama Sykes kwangu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
MKONO WA BURIANI WA MAMA SYKES KWANGU

Hii picha nimepiga na mama Bi. Zainab Sykes tarehe 12 January 2021 nyumbani Mbezi.

Nilikuwa natoka kufanya kipindi cha Mapinduzi ya Zanzibar, Studio za Clouds Plus, nikaona kheri nimpitie Mama Sykes kumwamkia.

Nimemkuta ameshika mashafu yake anasoma ambayo ndiyo hiyo kwenye picha kaishika kwa mikono yake miwili.

Alikuwapo na mama mdogo Bi. Hawa tukazungumza kiasi cha kuzungumza na kama kawaida mama akanitembeza Memory Lane akinikumbusha mumewe Bwana Ally Sykes na kunichekesha.

Siku ile mvua kubwa ilikuwa imenyesha.

Nikaagana na mama na akaniombea dua na kunikumbusha nisipotee sana.
Ndiyo ilikuwa buriani.

1613053450060.png
 
Jitahidi uitembelee na familia ya shujaa John Okelo
Lupwelo,
Famili ya Okello iko wapi?

Litakuwa jambo zuri kwangu mimi kupata fursa ya kuzungumza na jamaa zake.

Ninaweza kupata fursa ya kuandika kitabu.
Ikiwa una "contact" zao tafadhali nipatie.
 
kaka mkubwa pole sana kwa kuindokewa na mama,Mungu amfanyie wepesi huko aliko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom