Siwezi kuzungumza/andika kwa kudhani Mkono ama yeyote wa siasa si lazima atoke chama kimoja kwenda kingine mwingine aweza kuamua kufanya shughuli zake binafsi, maadamu hajasema kuvaa gwanda basi tusimlishe maneno kwa taarifa za ukanjanja.
Serikali itoe tamko juu ya kifo cha mwalim kama ambavyo mh. Vicent alivyosema kwa niaba ya familia ya mwalimu... utata umezidi kutanda Pro Mwakyusa anaweza kutusaidia juu ya hili
Toa mfano wa aliyejivua gamba akabaki akifanya shughuli zake! Ukishaingia katika siasa ni kama umeshaingia kwenye wanga!! Huwezi kuacha kuwanga eti kwa sababu uko ugenini! Mkono ni peopleeeees!
Ni mbunge gani wa UDP aliyesaini azimio hilo?
Wabunge hao watatu waliungana na wabunge wa vyama vya upinzani vya Chadema, CUF, TLP na UDP kusaini azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Baada ya hatua hiyo, Serikali ililazimika kufanya mabadiliko makubwa kwenye Baraza la Mawaziri na mawaziri wanane na manaibu wawili kutupwa nje ya ulingo.
Hapo ndo napotofautiana nawe wa Mwitongo tusidhani kwa mazoea tu maadamu hajasema kwanini tusivute subira? kuliko kumpandisha imani?
movie bado linaendelea
mda sio mrefu yataibuka mengi yatakayopelekea wabunge wa CCM kupigana hadharani live
na kuanika uozo wa kila mmoja wao.
Mpaka 2015 tutakuwa tumeshudia mengi makubwa,lets wait and see!
Hapa mahali tulipofika sasa patamu kweli..