Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Nimekumbuka alipokuwa akizungumza bungeni wakati akitoa hutuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17, kwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage, alisema mwaka 1961, Tanzania ilirithi viwanda 125 tu.
Waziri huyo mwenye jukumu la kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli, ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, aliweka wazi kuwa idadi hiyo ya viwanda vilivyorithiwa kutoka Serikali ya Kikoloni ni kidogo ikilinganishwa na viwanda vya sasa.
Mpaka mwaka 2005, wakati Serikali ya Awamu ya Nne ilipokuwa ikiingia madarakani, Mwijage alisema tayari viwanda vilikuwa vimeongezeka na kufikia 5,153.
Kwa mujibu wa takwimu hizo kuanzia mwaka 2005, kasi ya kuongezeka kwa viwanda nchini ilikuwa kubwa kuliko wakati wowote katika historia ya nchi, ambapo mpaka kufikia mwaka 2013, viwanda viliongezeka na kufikia 49,243.
Vilivyokufa
Akizungumzia viwanda vilivyokufa ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakivitumia kujenga hoja zao za kisiasa kuhusu ajira, Mwijage alisema viko 37 tu.
Alisema Serikali ilifanya tathmini katika viwanda vyote vilivyobinafsishwa ambavyo ni 106 na matokeo ya tathmini hiyo, yalibaini kuwa viwanda 45 vinafanya kazi vizuri; 24 vinasuasua na 37 tu ndio vimefungwa.
Ajira inayotolewa
Waziri Mwijage alisema kati ya viwanda hivyo 49,243, vikubwa ambavyo vimekuwa vikitoa ajira kuanzia watu 100 na kuendelea vipo 247.
“Viwanda vya kati vinaajiri kati ya watu 50 na 99 ni 170, viwanda vidogo vinavyoajiri kati ya watu watano na 49 ni 6,907 na viwanda vidogo sana vinavyoajiri chini ya watu watano ni 41,919,” alisema Mwijage.
Katika kuhakikisha JF inakuwa chanzo cha habari unapewa mwaliko wa kutaja mkoa wako una viwanda vingapi na kwa asilimia kubwa ni vile vinavyoajiri zaidi ya watu 100 au ni vile vya watu 5?