Mkoa wa Njombe wafanya vizuri zoezi la Vitambulisho vya Taifa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa NIDA imeendelea na zoezi la usajili na utambuzi nchini ambalo linafanyika kwa awamu. Awamu ya kwanza imejumuisha mikoa 12 ikiwemo mkoa wa Njombe. Akizungumza afisa msajili wa Mkoa wa Njombe Bw. Odoyo Albetus amesema mpaka sasa wamefanikiwa kusajili kata za Njombe mjini hivyo wamejipanga vyema kuendelea na usajili maeneo yote ya mkoa wa Njombe. Hivi sasa tayari amefanya mafunzo kwa viongozi wa kata na vijiji/mitaa kwenye Halmashauri ya Mji wa Makambako ili kuwajengea uwezo kuhusu maswala muhimu wakati wa usajili. Bw. Odoyo anasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha zoezi hilo.

Ili kusajiliwa ni lazima Mwananchi awe na umri wa miaka 18 na kuendelea pia afike na nakala (copy) ya nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

1.JPG

Pichani: Afisa msajili NIDA mkoa wa Njombe Odoyo Albetus akitoa mafunzo kwa Maafisa watendaji wa kata na mitaa/vijiji (WEO/VEO) wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako

2.JPG

Pichani: Maafisa watendaji wa kata na mitaa/vijiji (WEO/VEO) wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako wakiwa katika mafunzo ya usajili na utambuzi zoezi la vitambulisho vya Taifa.


Wananchi wanaweza kuwasiliana na NIDA kwa kupiga simu huduma kwa mteja namba 0673333444/0687416666. Au kuwaandikia S.L.P 12324, barua pepe nida.tanzania@nida.go.tz na kutembelea tovuti www.nida.go.tz ama mitandao ya kijamii. facebook; Nidatanzania, Twitter; @NIDA_Tanzania, Instagram; nidatanzania, Chaneli Youtube; Nida Tanzania.
 
Back
Top Bottom