Mkoa wa Mbeya mtavurugwa

Mkoa wa Mbeya mtavurugwa

SHADI JUMA

New Member
Joined
Jan 21, 2020
Posts
0
Reaction score
7
Mimi sio mwanasiasa bali ni mtumishi hapa Mbeya. Nimekuja mbeya sasa ni mwaka wa 4. Kuna jambo linaendelea mbeya na wao hawataki kulikemea.

Mkoa wa Mbeya wasipoangalia kufikia mwaka 2025 watatawaliwa na wanyakyusa. Nikupe takwimu Mbunge wa Chunya, Kyela, Rungwe na Busokelo ni Wanyakyusa. Mbeya Mjini, Mbalali na Mbeya vijijini si Wanyakyusa. Mwaka huu nilikutana na rafiki yangu jana Uyole akaniambia mjini wameshakaa lazima Tulia ashinde na sasa wanaangalia kati ya Mbalali na Mbeya vijijini nako wawe na mtu wao mwenye asili ya unyakyusa.

Aliniambia eti Rais amesema Tulia atakuwa Spika na 2025 ndiye atakuwa Rais. Mkakati wa kufanikisha Wanyakyusa eti unaratibiwa na wafanyabiashara wakubwa wa kinyakyusa.

Ombi langu kwa watu wa Mbeya kama mmemchoka Sugu tafuteni mtu mwingine. Tulia atawapeleka jehanamu. Hivi hamujiulizi anatoa wapi hela zote anazotoa kila siku ambazo hazifanani na mshahara wake? Hamjui kama anatumia ofisi yake vibaya kuomba mahela kwa wafanyabiashara ili kuja kuwanunua? Anaposema atakuwa Spika kwani Ndugai hagombei?

Sisi Tanga tunampenda Ummy lakini hajatuhonga ila matendo yake yanatufanya hata wapinzani tumpende.
 
Unajiegemeza katika ukabila kweli umefilisika kisera na mwisho wa kufikiri umekufika shame on you man, leo umeanza na kabila kesho udini na mlishaanza na ukanda hii ni TZ simeni majira.
Hoja yako ya kumwogopa tulia ni dhaifu sana
 
hii nukuu yako nzito;

"Tulia atakuwa Spika na 2025 atakuwa Rais"

kama huo ndio ukweli wa mambo basi hakuna wakumzuia huyo dada, na sio hao wafanyabiashara tu, bali atachotewa pesa hata hazina ilimradi tu ashinde hilo jimbo, na jinsi mkuu anavyompenda mpaka akamzawadia u Naibu Spika sina shaka na hilo.

Sugu itabidi ajipange kweli kweli hapo Mbeya Mjini, kuna nguvu ya moja kwa moja toka ikulu inamsaidia huyo dada, hayo mapesa yote anayatoa wapi?!

Ndugai na kujipeleka kote ikulu/dsm kwenye kila hafla ajiandae kutafuta kazi nyingine, au kama bado anapenda kuonekana kwenye viwanja vya bunge, itabidi arudi kukaa kwenye viti kama wenzake!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliniambia eti Rais amesema Tulia atakuwa Spika na 2025 ndiye atakuwa Rais. Mkakati wa kufanikisha Wanyakyusa eti unaratibiwa na wafanyabiashara wakubwa wa kinyakyusa.
Kawaida ni kama sheria, 2025 ni zamu ya wenzetu Waislamu!
 
SHADI JUMA,

Mkuu hoja yako nyepesi sana. Hapo si mfuasi wa Tulia, sioni chochote cha maana ulichoandika. Kwamba wachaga wasimchague mchaga mwenzao kwa kuwa tu itaonekana ni ukabila hata kama anaonekana anafaa. Hivi kuna yeyote aliekatazwa kufanya kama Tulia na kwa taarifa yako wananchi wa Mbeya huwahawaendekezi ukabila. Yeyote atakayeinekana anafaa atachaguliwa...iwe ni juhudi alizoonesha kutatua matatizo yao, ukaribu na wananchi n.k. Ni upuuzi kudhani uchaguzi utaleta ukabila wakati umeyaacha makabila yanayojulikana hivyo kama wachaga..
 
Nina imani kubwa kwamba Mbeya ndiyo itakuwa chachu ya Ukombozi wa kisiasa Tanzania!
 
Back
Top Bottom