Mkoa wa Mara unaendelea kuikomboa nchi yetu

Prof.Mhongo,na Eliakimu Maswi-Hawa pia ni ndume wa Mara.Shupaavu hasaa
 
Kiukweli Mara ni watu wenye kujitoa hata pale penye upinzani ambao hauna masilahi kwa wengi au taifa.

mifano ni kama huo wa JK Nyerere kujitoa kupigania uhuru wa Tanganyika.
2:Wakati wa harakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa Mara ni moja ya mikoa iliyodhubutu kuasisi siasa za vyama vingi chini ya Mabere Marando na chama cha NCCR-MAGEUZI ikumbukwe uchaguzi wa kwanzq wa vyama vingi wa mwaka 1995 majimbo manne mkoani Mara yalishikiliwa na chama cha upinzani;
1.Musoma vijijini-Magesa.
2, Bunda- Wasira
3,Tarime-Mabere Marando.
4:Mwibara-Tegambwage
na hata Musoma mjin isingekuwa mizengwe ya ccm ingechukuliwa Masumbuko enzi hizo hao wote kutoka NCCR-MAGEUZI.
Kwa hiyo hili la Waryoba na Butiku sio geni kwa watu wa Mara just waungwe mkono tu watatuongoza kupata katiba bora.
 
Sisi Watanzania sijui tuna akili za vipi? Hili nalo tunalipeleka katika ukabila?
 
jaman hapa hatujalipeleka kwenye ukabila bali ni uhalisia wa mambo tu na uzuri wa Mara ni mkoa pekee wenye makabila mengi kuliko mkoa wowote hapa nchini japo mengine ni madogo lakini wote wanaishi kama kawaida ya watz wengine.
 
Acha mawazo finyu,nchi hii haikuanza kukombolewa wakati wa vita ya kagera,ukombozi wa nchi hii umeanza hata kabla nyerere hajazariwa,nikupe mfano kidogo bwana mdogo,

vita ya majimaji iliongozwa na kinjekitile,hakuwa mzariwa wa mara,mtemi mirambo wa Tabora,mkwawa wa Iringa wote hawa walipigania nchi hii,

kuna watu wamepigania nchi hii,na kupoteza maisha yao,

Mwanajopo unaweza kuwa sahihi ila lengo la muweka uzi ukisoma na kutafakali utajua ni nini.
Kwani hata hao unaosema walikuwa wakombozi kabla au baada ya kambarage mbona walio HAI hawaonekani kushiriki kuwaunga mkono ktk (maneno ya mtoa mada) ili kupata kile ambacho mzee Warioba na Butiku wanataka jamii ielewe?
 
Just for record - Jaji Waryoba si Mzanaki; ni Muikizu wa pale Nyamuswa kilometa kama 25 kutoka Butiama.
 
Kiukweli Mara ni watu wenye kujitoa hata pale penye upinzani ambao hauna masilahi kwa wengi au taifa.

mifano ni kama huo wa JK Nyerere kujitoa kupigania uhuru wa Tanganyika.
2:Wakati wa harakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa Mara ni moja ya mikoa iliyodhubutu kuasisi siasa za vyama vingi chini ya Mabere Marando na chama cha NCCR-MAGEUZI ikumbukwe uchaguzi wa kwanzq wa vyama vingi wa mwaka 1995 majimbo manne mkoani Mara yalishikiliwa na chama cha upinzani;
1.Musoma vijijini-Magesa.
2, Bunda- Wasira
3,Tarime-Mabere Marando.
4:Mwibara-Tegambwage
na hata Musoma mjin isingekuwa mizengwe ya ccm ingechukuliwa Masumbuko enzi hizo hao wote kutoka NCCR-MAGEUZI.
Kwa hiyo hili la Waryoba na Butiku sio geni kwa watu wa Mara just waungwe mkono tu watatuongoza kupata katiba bora.

hukutaja vita ya kagera na military commanders toka Mara achilia mbali ushupavu wa askari wa miguu.

waingereza walijua wanafanya nini walipowaingiza wana mara kwa wingi kwenda kupigana vita kuu ya pili.

tatizo wanalopambana nalo kwa kina Waryoba ni kuwa mwana mara anaposema Yes huwa ni YES na akisema NO huwa ni NO.

Kuna jamii humu bongo hazipendi kusikia NO.
 
Jamani hivi wengine mbona akiri zenu zimekaa tenge sana!!!, hivi mleta mada alimaanisha watu walioikomboa nchi au ni watu waliopigania sehemu zao kama watemi???.Jk nyerere alipigania Tanganyika yote bila kubagua na kweli alifanikiwa kuikomboa na uhuru kwa makabila yote ya Tanganyika ulipatikana.Hao akina Mkwawa,Kimweri,Isike,Mirambo na wengine hawakukomboa chochote zaidi ya kujiua na kuuliwa, ila walijaribu.

yaani nyie inaonekana mmepitia shule za kata,hao machifu,walipigana na wajerumani,sasa hao wajerumani walikuwa wanatawala baadhi ya mikoa,au tanganyika nzima? wakati hao wazanaki wenzenu wanakuja kuwa viongozi wa wazee waliodai uhuru wa nchi hii,mambo yalikuwa tayari tambarare mjerumani ameishatoka,yupo muingereza,acheni umazwaza,kasomeni historia vizuri
 
Mwaka 1961 Mwl Nyerere aliongoza mapambano ya kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa wakoloni, alionyesha umahili wa kizanaki kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa wanaweza kuwa huru na hatimaye nchi ikakombolewa kutoka kwa wakoloni wa kizungu.
Mwl Nyerere ni chimbuko la Mkoa wa Mara kabila la Wazanaki.

Baada ya ukombozi wa wakoloni weupe sasa nchi yetu imebaki kuwa kwenye mikono ya wakoloni weusi.
Hapa tena bado Mkoa wa Mara umeamua kuikomboa nchi yetu kutoka kwa Wakoloni weusi(CCM).

Jaji Warioba ni Mzanaki wa kutokea Mkoa wa Mara, Butiku ni Mzanaki kutokea mkoa wa Mara, hawa wazee wanapata uchungu kuona nchi ikirudi kwa wakoloni ambapo uliondolewa na kaka yao Nyerere na hapo ndo maumivu yanawashika na kuamua kuchukua maamzi kama ya kaka yao Nyerere maana wamefikia mahali wamechoka japo nao ni makada wa ccm.
Hawa watu wa Mara nimeamini waliletwa kwa mara moja duniani na maamzi ya pamoja...

Kwanini tuu harakati za ukombozi huu unafanywa na watu hawa wa huu mkoa kwa nyakati tofauti, na kwanini mikoa mingine inakuwa nyuma?

Hao unaowasema ni makada wa CCM,kwa kipindi kirefu sana cha maisha yao,wamefanya mengi mazuri,na mabaya kibao,wakati wa awamu ya pli ya mzee Mwinyi,walikuwa wapi wakati nchi inaharibika? wakati mkapa anaharibu uchumi wa nchi hii,hawa makada walikuwa wapi? mbona hawakusema chochote,chama chao ni chama cha mafisadi,mbona hawathubutu kujitoa? hawana lolote ni walewale majizi tu
 
Ndio maana tunataka Rais 2015 atoke Mara ili tuimarishe Taasis ya Urais na Chama.
Stephen Wasira atosha wengine wa nini?
 
Hao unaowasema ni makada wa CCM,kwa kipindi kirefu sana cha maisha yao,wamefanya mengi mazuri,na mabaya kibao,wakati wa awamu ya pli ya mzee Mwinyi,walikuwa wapi wakati nchi inaharibika? wakati mkapa anaharibu uchumi wa nchi hii,hawa makada walikuwa wapi? mbona hawakusema chochote,chama chao ni chama cha mafisadi,mbona hawathubutu kujitoa? hawana lolote ni walewale majizi tu

kuna haja ya kuwa-fair kwa mleta mada. yeye kaeleza kuwa vijana wanaotoka mkoa wa mara wamechangia sana ukombozi wa bongo. Sio kwa CCM wala vyama pinzani. mwelekeo ni huo huo

Lakini kama umepitia elimu ya juu hapa bongo ni kila mara utakuta vijana toka mkoa huo wapo katika top leaders wa serikali za wanafunzi

Kwenye vita ya kagera ni mkoa huo peke yake vijana walijitolea kwenda vitani kuliko mikoa mingine yote

performance ya makamanda wa kijeshi toka mkoa huo wakati wa vita ya kagera na vya ukombozi na hata wakati wa amani haijawahi kuwa tatizo
 
Huo ni mfano mdogo sana,chukua kwa mfano vyama viwili vikuu vya upinzani,hebu tuambie wabunge wenye mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Mtanzania,wangapi wanatoka mara?ukiangaria vizuri kila kona ya nchi hii kuna watu wenye weredi wa uongozi,na siasa sio mara tu,

Vyuo vikuu sio UDSM, peke yake mimi nimepita DIT,tumekuwa na viongozi mbarimbari kutoka makabira tofauti sio watu wa mara tu,kitu kikubwa nirichojifunza kwa wenyeji wa mara sanasan vijana wanaokuwa katika hizi taasisi za elimu ya juu,ni kwamba ni watu wanaonunurika kiraisi,ni wala rushwa wazuri,mwaka 1999-2000,rais wa serikali ya wanafunzi DIT,ALISHITAKIWA kwa ubadhirifu wa fedha za wanafunzi,hata vyeti vyake vilishikiliwa na uongozi wa chuo,

Jamaa mwingine,wa huko huko mwaka 2005,alisaliti mipango ya wanafunzi ya kugoma,kwa kuhaidiwa ajira na Principal,ambaye na yeye ni wahuko huko,

Kwa ufupi kila mtanzania bira kujari anatokea upande gani wa nchi hii,ameifanyia na anaweza kuifanyia nchi hii jambo zuri,hakuna utafiti unaoonyesha kwamba watu wa eneo fulani ndio wamechangi zaidi katika mustakabari na ustawi wa Taifa hili,
Au tuseme kwamba Wachaga ndio wanoshikiria uchumi wa nchi hii,kwa elimu yao ya biashara na ukusanyaji kodi,maana bira kodi hata nchi aiendi,hata hao wenyeji wa mara waliopo jeshini hawatapata mishahara,sinzani kama ni kweli,mtu yeyote akipewa nafasi anaweza kufanya mazuri yanayo fanyika kwenye taasisi hiyo,bila kujari anatoka upande gani wa nchi,
 
yaani nyie inaonekana mmepitia shule za kata,hao machifu,walipigana na wajerumani,sasa hao wajerumani walikuwa wanatawala baadhi ya mikoa,au tanganyika nzima? wakati hao wazanaki wenzenu wanakuja kuwa viongozi wa wazee waliodai uhuru wa nchi hii,mambo yalikuwa tayari tambarare mjerumani ameishatoka,yupo muingereza,acheni umazwaza,kasomeni historia vizuri

Nadhani mtoa mada alikuwa na kusudio zuri na wala sio majigambo,tumwele tu.Manake watu wengne waliopgania ukombozi wa nchi waamke tena, nchi imevamiwa tena na wakoloni mara hii ni weus.
 
Huo ni mfano mdogo sana,chukua kwa mfano vyama viwili vikuu vya upinzani,hebu tuambie wabunge wenye mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Mtanzania,wangapi wanatoka mara?ukiangaria vizuri kila kona ya nchi hii kuna watu wenye weredi wa uongozi,na siasa sio mara tu,

Vyuo vikuu sio UDSM, peke yake mimi nimepita DIT,tumekuwa na viongozi mbarimbari kutoka makabira tofauti sio watu wa mara tu,kitu kikubwa nirichojifunza kwa wenyeji wa mara sanasan vijana wanaokuwa katika hizi taasisi za elimu ya juu,ni kwamba ni watu wanaonunurika kiraisi,ni wala rushwa wazuri,mwaka 1999-2000,rais wa serikali ya wanafunzi DIT,ALISHITAKIWA kwa ubadhirifu wa fedha za wanafunzi,hata vyeti vyake vilishikiliwa na uongozi wa chuo,

Jamaa mwingine,wa huko huko mwaka 2005,alisaliti mipango ya wanafunzi ya kugoma,kwa kuhaidiwa ajira na Principal,ambaye na yeye ni wahuko huko,

Kwa ufupi kila mtanzania bira kujari anatokea upande gani wa nchi hii,ameifanyia na anaweza kuifanyia nchi hii jambo zuri,hakuna utafiti unaoonyesha kwamba watu wa eneo fulani ndio wamechangi zaidi katika mustakabari na ustawi wa Taifa hili,
Au tuseme kwamba Wachaga ndio wanoshikiria uchumi wa nchi hii,kwa elimu yao ya biashara na ukusanyaji kodi,maana bira kodi hata nchi aiendi,hata hao wenyeji wa mara waliopo jeshini hawatapata mishahara,sinzani kama ni kweli,mtu yeyote akipewa nafasi anaweza kufanya mazuri yanayo fanyika kwenye taasisi hiyo,bila kujari anatoka upande gani wa nchi,

Mkuu, Pole kwa yaliyokupata. Uzoefu wangu ulikuwa kinyume na uliyoyaeleza. Kisha utumiaji wako wa "R" mahali pa "L" unanipa mashaka kuhusu ulikotokea.
 
Mwaka 1961 Mwl Nyerere aliongoza mapambano ya kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa wakoloni, alionyesha umahili wa kizanaki kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa wanaweza kuwa huru na hatimaye nchi ikakombolewa kutoka kwa wakoloni wa kizungu.
Mwl Nyerere ni chimbuko la Mkoa wa Mara kabila la Wazanaki.

Baada ya ukombozi wa wakoloni weupe sasa nchi yetu imebaki kuwa kwenye mikono ya wakoloni weusi.
Hapa tena bado Mkoa wa Mara umeamua kuikomboa nchi yetu kutoka kwa Wakoloni weusi(CCM).

Jaji Warioba ni Mzanaki wa kutokea Mkoa wa Mara, Butiku ni Mzanaki kutokea mkoa wa Mara, hawa wazee wanapata uchungu kuona nchi ikirudi kwa wakoloni ambapo uliondolewa na kaka yao Nyerere na hapo ndo maumivu yanawashika na kuamua kuchukua maamzi kama ya kaka yao Nyerere maana wamefikia mahali wamechoka japo nao ni makada wa ccm.
Hawa watu wa Mara nimeamini waliletwa kwa mara moja duniani na maamzi ya pamoja...

Kwanini tuu harakati za ukombozi huu unafanywa na watu hawa wa huu mkoa kwa nyakati tofauti, na kwanini mikoa mingine inakuwa nyuma?

Huo sasa ndo unasikia Ukabila na Ukanda, kumbuka kuwa kidole kimoja hakivunji chawa.
 
Back
Top Bottom