Mkoa wa Dar es Salaam sasa kuwa na Wilaya tano

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,693
1,701
RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.

“Hatua hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.

Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. Aidha, alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na kuongezeka kwa wilaya, Sadiki aliwataka watendaji wake kuwa waadilifu katika ugawaji wa mipaka na rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufi kia jana, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubongo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni.

Source:JPM ARIDHIA WILAYA ZA UBUNGO NA KIGAMBONI | Uhuru
Maswali Muhimu ya kujiuleza kwa yeyote anayeweza kutoa ufafanuzi:
1. Je ni kweli kuongeza wilaya kutaleta maendeleo ya haraka? Vipi kuhusu gharama za uendeshaji zitakazotokana na kuongeza watendaji na kujenga makao makuu ya wilaya?
2. Je ni kweli usimamizi thabiti hautakuwa na kisingizio?
3. Vipi kuhusu mipaka?
4. Vipi kuhusu mabaraza ya Madiwani?
 
Kwa nini umesema hivyo Mkuu? Uandhani DSM haina umuhimu wa kugawanywa na kwa nini?
 
Tangu 2014 wao waliegemea.kwenye kigezo cha kusogeza maendeleo,saea na ugawaj wa majimbo tu tumeona jana limezungunziwa jimbo la Kibamba na changamoto zake kwenye umeme while zaman ilikua ni Ubungo,
 
DSM yote ni sawa na wilaya moja ya kilombero au bagamoyo, lakini nashangaa inakuwa na wilaya tano!!!
Mkuu Ibilisi, ulaaniwe (hiyo ni salamu ya kiibilisi)
Unafananisha Jiji la DSM na Kilombero au Bagamoyo kweli !!??? Ili Maendeleo na huduma muhimu za Kijamii kuweza kuwafikia Wananchi kwa muda na haraka nafikiri serikali iko sahihi kugawa Wilaya ya Kinondoni na Temeke.
 
Uwepo wa wilaya mpya kutapelekea ongezeko la matumizi ya serikali. Sijui hii dhana ya kubana matumizi uwa inatumika kipindi gani tu?!? Wilaya mpya zitahitaji ofisi, magari, mishahara na marupurupu ya wakuu wa wilaya na watumishi wengine, malipo ya bills za maji, umeme n.k. kwenye ofisi za wilaya, gharama za matunzo ya vyombo vya usafiri vya wilaya n.k.

Hii dhana ya kugawanya maeneo ili kuleta maendeleo ni potofu sana. Pengine serikali na mnaotetea hii dhana mtuambie kwa takwimu maeneo mapya ya kiutawala (wilaya na mikoa) hali zao za maisha na maendeleo kiujumla zimekuwaje baada ya kugawanywa huko.

Ukisema ugawaji wa wilaya mpya unasogeza huduma za jamii karibu na watu. Lakini tunasahau, unaweza kusogeza huduma hizo bila ya kuwa na wilaya au mkoa mpya. Ni utayari tu wa serikali katika kufanya hivyo. Sidhani kama kujenga hospitali, kupelekea umeme, maji n.k. kunahitaji mpaka eneo liwe wilaya.

Alternatively, kama kweli serikali ina nia ya kubana matumizi haswa katika kupunguza kugharamia ofisi nyingi na mishahara ya watumishi wapya wa wilaya, inaweza kutumia utaratibu kama ule wa mabalozi wa nchi wanapowakilisha nchi zao katika zaidi ya nchi moja. Hivyo, kunaweza kuwa na wilaya mpya sawa, lakini mkuu wa wilaya kwa mfano ya Temeke ndiyo anatumikia pia wilaya mpya ya Kigamboni. Vivyo hivyo kwa Ubungo, mkuu wa wilaya ya Kinondoni anatumikia pia Ubungo. Na watumishi katika wilaya hizo wanakuwa watumishi katika wilaya mpya hizo.
 
Mkuu,
Kuongeza Wilaya mbili hakuna maana ya kwamba ni lazima waongezeke Wakuu wa Wilaya wawili na watumishi katika hizo Wilaya. Hawa watumishi wa Wilaya zinazogawanywa wanatosha kabisa kugawanywa katika "vikosi kazi" katika hizo Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni. Kuna uzembe wa hali ya juu katika hizo Wilaya kwa kisingizio cha ukubwa wa Wilaya na kuelemewa na kazi. Nafikiri ndio maana Serikali imeona kuna umuhimu wa kuzigawa.

Tusipende kukurupuka na kuhusisha Siasa kwenye kila Jambo. Hii inatupotezea busara na hekima ya kuweza kutafakari na kuchanganua mambo ya msingi katika Maendeleo ya TAIFA.
 
Back
Top Bottom