PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametoa maelekezo kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) nchi nzima kuhakikisha hakuna foleni zisizo na sababu zitakazokwamisha na kuzorotesha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Ulega ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana wakati akikagua maendeleo ya upanuzi wa barabara ya Mbagala Rangi Tatu - Kongowe (km 3.8) ambapo alizungumza na wananchi wa eneo hilo na kuwaeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha zaidi ya Shilingi Bilioni 54 kutumika kwa ajili ya kutatua kero ya foleni kwa wakazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
"Wakurugenzi kutoka TANROADS, ninaagiza kwa Mameneja wote nchi nzima nikisikia habari za foleni zinalalamikiwa na wananchi na hakuna suluhu ya muda mfupi na ya muda mrefu hufai kuwa Meneja," alisema Waziri Ulega.
Aidha, Ulega ametoa angalizo kwa Mameneja hao katika kipindi hiki cha mvua zinazotarajiwa kunyesha kuhakikisha barabara hazileti athari kwa wananchi na kusababisha kushindwa kufanya shughuli zao kutokana na kukosa suluhu ya jambo hilo mapema.
"Mameneja fanyeni kazi, msikae kimazoea na kuona jambo hilo ni la kawaida, kukatika kwa barabara tafsiri yake Meneja hukagui barabara yako na kuona hapa kuna udhaifu ambao lolote likitokea pataharibika," amesisitiza Ulega.
Vilevile, Ulega amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Pwani kuhakikisha anaitengeneza barabara ya zamani ya Morogoro haraka iwezekanavyo ili iweze kuwa njia mbadala ya kutatua changamoto za magari kukwama katika barabara kuu ya Dar es Salaam hadi Chalinze.
Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Lazeck Alinanuswe ameeleza kuwa upanuzi wa barabara hiyo unatekelezwa na Mkandarasi STECOL Corporation kutoka China na kusimamiwa na Kitengo cha TECU kutoka TANROADS kwa muda wa miezi 15 na hivyo mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2026.