Mkitaka kuolewa basi punguzeni 'kujipura' kuliko pitiliza

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Wanaume wengi tumekuwa tunatishwa sana na mwonekano wa wanawake kwa sasa, kwanza wengi wao wamepoteza uhalisia.

Ukimtathmini mwanamke nywele mpaka kucha gharama alizotumia, unaogopa, maana wengi haziendani na kipato chetu wanauame na hata ukitaka kumweka ndani unahofia ataniumiza kichwa maana hutoweza kumudu gharama.

Kwa namna hii ndomana wanawake wengi wa dizaini hii wameishiwa kuchezewa au kutumiwa kama nyumba ndogo Bila kuolewa.

Maana wanaume wengi wanahitaji mwanamke simple wakujenga naye maisha, ambaye ataweza kupambana na kila hali itayojitokeza, je kwa dizaini ya mwanamke kama huyu ataweza pikia kuni kama gesi imeisha?

Huwa tunajiuliza baadhi ya maswali kama haya na kisha tunafanya maamuzi. ndo maana matajiri wengi au watu wengi maarufu wameowa wanawake simple sana na matokeo yake wamefanikiwa.

Angalizo

Sina lengo la kupinga wanawake kujipura hapana ila kuna kiwango chake,
Sio kama hawa wa leo unajikuta mtu kajibandika rangi kama mia katika mwili wake utasema kama jini la kutumwa? Khaaaa!

Hata kama urembo ila sio huu
 
Mdada unataka kumrukia mahanjam yaanze anakwambia ngoja kwanza nivue wigi,shaabash.

Kwangu mwanamke anayevaa mawigi,manywele ya katani,brazilian sjui ushuzi gan,too much make up,kutinda nyusi,kufuga makucha kama jini am kuweka za bandia kwangu ni haraaaaaam labd itokee tu dharura,natural beauty is the best beauty
 
Mdafa unataka kumrukia mahanjam yaanze anakwambia ngoja kwanza nivue wigi,

Kwangu mwanamke anayevaa mawigi,manywele ya katani,brazilian sjui ushuzi gan,too much make up,kutinda nyusi,kufuga makucha kama jini am kuweka za bandia kwangu ni haraaaaaam labd itokee tu dharura,natural beauty is the best beauty
yaan ww mkuu kama mimi sipendi hayo mawigi make up sijui hayo makucha yao na marangi yao ndo usiseme.

mimi nampenda mwanamke natural hata kama ananywele zake za kipilipili
 
Anakwambia yeye keshazoea kwenda kufanyiwa massage week mara tatu... Hawezi kaa na nyewele hizo hizo za kubandika zaidi ya week... Hawezk rudia nguo akivaa akivua anagawa... Hawezi kujibana bana kwa kutumia chini la laki moja kwa siku...

Wakati kwenye mkoba wake ana mia tano ya mwendo kasi tu...
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Back
Top Bottom