Mkimgusa Edward Lowassa mtasahaulika katika siasa za Tanzania!

Lowasa nimjuaye mimi ni yule aliyekuwa hana pesa alipokuwa chuoni UDSM na hata alipokwenda UK kusoma.
Alipopewa uDirector AICC alikuwa hana hata suti na usafiri wa maana. AICC akaifanya kijiwe chake cha kujipalilia kwa jumuiya za CCM hasa vijana. Mapato ya AICC yakashuka kupita kiasi. Mikutano AICC ikawa ni jumuiya za CCM kuliko ya kimataifa.

Then alipoingia Wizara ya Ardhi, akaendelea kujipanga. Akamchukua mshikaji wake yule mnyarwanda, Haruni Masebu akamuweka NHC, si unajua tena NHC kulivyo. Baadaye akamuweka EWURA, kule kwenye mambo yote ya mafuta.

Halafu akapitisha mkwara hapo wizarani na kufukuza watu kazi akiwasingizia ubadhilifu, kisha yeye akaketi chini kuanza kuinywa wizara taratibu na kujitajirisha. Ghafla yule masikini akawa ananukia utajiri. Akawa hata na uwezo wa kujenga majumba ya mamilioni overnight, likiwemo lile la Masaki lililopangishwa na ubalozi wa SA, licha ya kipato chake tu cha utumishi serikalini. Labda mwenzetu alishinda bahati nasibu ya Power Ball.

Mara akaanza kujishaua, akaweza kukodisha ndege ya kumpeleka Dodoma kugombea uraisi, kabla ya kupigwa buti na mwalimu. Juzi juzi tena akakodi nyingine ya kumpeleka kwenye mazishi ya Mwalimu na Monduli alipofukuzwa uPM. Hivi ni watumishi wangapi wa serikalini tena waliofukuzwa kazi lakini bado wanakuwa na uwezo wa kukodisha ndege ya kuwarudisha majimboni kwao? Kumbuka huyu ndiye yule yule Lowasa aliyekuwa masikini miaka michache iliyopita na ajira yake, ukiachilia ile ya AICC, ni hizi za serikali ambazo mishahara na marupurupu yake tunayajua.

Ingekuwa vema watu wote wanaogombea uraisi wafanyiwe auditing ya mapato/matumizi yao na kodi walizolipa. Hapo madudu mengi yangegundulika.

Umeweka simulizi ya mapito ya rais mtarajiwa,

Hiyo ni hadithi ya kufikirika tu!
Ili ueleweke leta ushahidi halisi wa ufisadi wa Lowasa hapa!

Skani nyaraka zinazo onyesha kuwa Edward Lowassa ni Fisadi na zilete hapa
 
kwa hiyo hiyo Richmond unaona ni kitu kidogo sana?Pia hata huyo rafiki yake ambaye hawakukutana bara2ni pia tungekuwa na uwezo tungemtoa Ikulu maana ndo wale2,Yaani usiwadanganye watu eti anapendwa huo ni uongo unataka upinzani wapite tu wakimsimamisha el,au unadhani watampa kwa ajili ya michango yake makanisani,yeye atoe tu lakini hicho si kigezo cha kupata Urais
 
Soma maelezo ya mleta uzi anasema kuna watu wanakunywa na kula kwa LOWASA

Uzi nimeuleta mimi, nimesema waliondani ya ccm ndio wanaokula na kusaza kwa baba Lowassa, lakini wewe umesema mimi nimelipwa hapa mtandaoni ndiomaana nikauliza kuwa EL anagawa hapa jf?
 
kwa hiyo hiyo Richmond unaona ni kitu kidogo sana?Pia hata huyo rafiki yake ambaye hawakukutana bara2ni pia tungekuwa na uwezo tungemtoa Ikulu maana ndo wale2,Yaani usiwadanganye watu eti anapendwa huo ni uongo unataka upinzani wapite tu wakimsimamisha el,au unadhani watampa kwa ajili ya michango yake makanisani,yeye atoe tu lakini hicho si kigezo cha kupata Urais

Nimeshasema kuwa Lowassa hahusiki na Richmond! Alifanya kazi kama mwajiriwa wa umma chini ya maagizo ya bosi wake Jk
 
chondechonde kikwete achana na agenda hiyo ya upole, inakiua chama chako na serikali yako,

ni karibu miezi 28 sasa, edward lowassa amekuwa agenda kuu ndani ya ccm na wanaccm wenye, si mwenyekiti wala mjumbe wote mioyo yao ni lowasa tu, wengi wakitaka ajipambanue nakuwa nyota huru ya chama na wachache walio juu ya chama wakitaka kumpoteza gwiji huyu wa siasa za ukwasi na fitina msonge!

Ikumbukwe kuwa doa kuu linalotajwa kuwa lowa ni fisadi ni richmond, lakini nani asiyejua richmond ni nani na ilikuwaje? Pale dodoma lowasa ameweka wazi mbele ya mwenyekiti kuwa hakuna kilichotendeka ambacho mwenyekiti hakukijua ama kumtuma! Narudia tena uchafu wa lowassa ni richmond tu!

Nauliza tena richmond ni nani? Mwenyekiti alijibu nini siku ile pale dodoma wakati lowassa anamhiji zaidi ya kuinamisha kichwa chini hali iliyopelekea bwm kumtuliza lowasa?

Sasa lowassa anakitaka chama na agombee urais na ameshashinda ndani ya chama na nusu uwanja nje ya chama, shime ccm, ili muendelee kuitwa chama cha siasa japo mwaweza kuwa wapinzani zuieni jaribio la mwenyekiti wenu la kujaribu kumzika lowassa angali amekibeba chama!

Kuna juhudi za kitoto ndani ya ccm eti wapo kwenye harakati za kumuuandaa january makamba kugombea urais 2015, wanatumia raslimali za nchi kujijenga kisiasa kwa upinde wa mvua ya siasa!

Chondechonde mwenyekiti wa ccm ndugu jakaya mrisho kikwete, amini lowassa ndie chaguo la wanaccm wote hata hao wanaojifanya wapo na wewe mioyo yao ipo kwa lowassa! Wanakula na kunywa kwa mgongo wa lowassa!

Mwenye ushahidi wa wazi juu ya ufisadi wa lowassa aulete hapa, sio stori za kulishwa vijiweni kisha mnakuja hapa kupiga ngonjera ooho lowasa fisadi, oooho sijui nini! Leteni utetezi hapa

mimi nitampa kura yangu ikiwa atagombe japo hata shinda, lakini atakinusuru chama kufutika kabisa duniani!

Rejao, zomba, malaria sugu msianze kuugua matumbo ya ghafla!

El2015


ok bwana kila mtu na maoni yake unaona anafaa lowasa mpe kura yako,si ndiyo uhuru/haki
ya kila mtu wa kikatiba.ila mimi naona kama watamsimamisha wasira(tyson)huyu atatufaa zaidi.ccm
tufikirie zaidi juu ya hili.
 
ok bwana kila mtu na maoni yake unaona anafaa lowasa mpe kura yako,si ndiyo uhuru/haki
ya kila mtu wa kikatiba.ila mimi naona kama watamsimamisha wasira(tyson)huyu atatufaa zaidi.ccm
tufikirie zaidi juu ya hili.

Hehee yote kheri mkuu!
 
Wewe na nani hammtaki Lowasa? Lete ushahidi wa ufisadi wake hapa!

We tapika tu sikununulii ndimu kwa mangi ng'ooo!

Ni kweli kwa hali halisi ilivyo sasa ndani ya CCM na Serikali yake ni KWELI Lo hasa kwa sasa ndie bingwa wa SIASA za UKWASI na ZENGWE kwa yoyote asie upande wake.Na CCM ilipofika inaitaji watu WELEVU/MAKINI na BRAVE wenye uwezo wa kufanya LISILOTEGEMEWA ili kumstopisha LOWASA asizame na CCM.

Kwa ilivyo sasa upande wa pili nao kama ndio wanajipanga na hayo unayoyasema naona kama haiwezekani kwa kuwa toka mwanzo January yuko upande wa GWIJI na huku kwingine labda iwe ni changa la macho kuwa wawili wanafahamiana na kinachoendelea kuwa na DEVIL PLAN kuwa nilushie jiwe likinipiga nami nitalia kama niumeumia kwa jiwe hilo.

Ubaya wa Mchezo mzima
1: Alivyochafuka LO HASA kusafishika ili apate kuwa Rais wa Tanzania,ni kazi ngumu na ili kuvuka uchafu huo ni mahakama na vyombo vya dini vyenye kuaminika na waumini wake viongozi wake wasimame mbele ya hadhara ya umma na kuwaambia kuwa mtu huyu ni msafi na kuwa wawe tayari kujibu maswali ya umma.

2: Na kama wakimsimamisha basi URAIS unaenda chama cha CHADEMA.Kwa kuwa mabomu ya VIONGOZI WA CCM yatalipuliwa na Wanachadema.Kwa kuwa tulipofika sasa hakuna chombo kitakachoweza kuzuia nguvu za umma,na hata kama viongozi wa CHADEMA watanunuliwa wajue kuwa UMMA sasa hivi wamekuwa MAKINI na wanajua nini kinachoendelea.SUGU na MWENYEKITI wake wanajua shughuli nzima ya wananchi na busara ya SUGU kulusha turufu yake kwa wananchi na kuepuka offer,leo hii anajisifu kwa kuchagua njia sahihi ya kuwatumika Wananchi kuliko ambako angechagua the other way round leo pengine tungekuwa na hadithi nyingine kwa uchungu wa umma.Kwa kuwa wanambeya walishatendwa.Hivyo viongozi wanaotegemea Cash kuwa itanyoosha barabara hakika hizo ni ndoto kwa kuwa watu ndio wananjaa lakini pia njaa hiyo imewapa maarifa ya kungamua kuwa wanauwezo wa kuingia deal na Mwanasiasa na bado wakamkaanga kikaangoni pia.

3: Na CCM ili iweze kucheza na kuibuka na ushindi wa Urais haina budi kumtumia Candidate ambae anakubalika na na wananchi na hata vyama vya upinzania vinamkubali kwa kuwa si mmoja wa mafisadi.Na wanejua kuwa anakubalika na wananchi na vyama vya siasa wao kama chama hawana IMANI nae kwa kuwa wanaona atawageuka,wanasahau kanuni ya Zimwi likujualo halikuli likakwisha na kuwa ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili.Hivyo kama wana busara basi wakae wakubaliane je wapoteze vyote kabisa ikiwemo vifungo magerezani au aje anae wajua awanyanganye mali walizokwapua Serikalini na kuweka RECONCILIATION.Ninavyojua mimi ni lahisi kuwa na likorenciliation inawezekana kufanyika kwa kuwa na MwanaCCM alie lahisi kuliko Chadema.Kwa kuwa upinziani wakiingia madarakani kinachofuata ni vifungo.!!
 
Chondechonde Kikwete achana na agenda hiyo ya UPOLE, inakiua chama chako na serikali yako,

Ni karibu miezi 28 sasa, Edward Lowassa amekuwa agenda kuu ndani ya CCM na wanaccm wenye, si mwenyekiti wala mjumbe wote mioyo yao ni Lowasa tu, wengi wakitaka ajipambanue nakuwa nyota huru ya chama na wachache walio juu ya chama wakitaka kumpoteza gwiji huyu wa siasa za ukwasi na fitina msonge!

Ikumbukwe kuwa doa kuu linalotajwa kuwa Lowa ni fisadi ni Richmond, lakini nani asiyejua richmond ni nani na ilikuwaje? Pale dodoma Lowasa ameweka wazi mbele ya Mwenyekiti kuwa hakuna kilichotendeka ambacho mwenyekiti hakukijua ama kumtuma! Narudia tena UCHAFU wa LOWASSA ni RICHMOND tu!

Nauliza tena RICHMOND ni nani? Mwenyekiti alijibu nini siku ile pale Dodoma wakati lowassa anamhiji zaidi ya kuinamisha kichwa chini hali iliyopelekea BWM kumtuliza Lowasa?

Sasa Lowassa anakitaka Chama na agombee urais na ameshashinda ndani ya Chama na nusu uwanja nje ya chama, shime ccm, ili muendelee kuitwa chama cha siasa japo mwaweza kuwa wapinzani zuieni jaribio la mwenyekiti wenu la kujaribu kumzika Lowassa angali amekibeba chama!

Kuna juhudi za kitoto ndani ya ccm eti wapo kwenye harakati za kumuuandaa January Makamba kugombea Urais 2015, wanatumia raslimali za nchi kujijenga kisiasa kwa upinde wa mvua ya siasa!

Chondechonde mwenyekiti wa ccm ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Amini Lowassa ndie chaguo la wanaccm wote hata hao wanaojifanya wapo na wewe mioyo yao ipo kwa Lowassa! Wanakula na kunywa kwa mgongo wa Lowassa!

Mwenye USHAHIDI wa wazi juu ya UFISADI wa Lowassa aulete hapa, sio stori za kulishwa vijiweni kisha mnakuja hapa kupiga ngonjera ooho Lowasa fisadi, oooho sijui nini! Leteni utetezi hapa

Mimi nitampa kura yangu ikiwa atagombe japo hata shinda, lakini atakinusuru chama kufutika kabisa duniani!

Rejao, Zomba, Malaria Sugu msianze kuugua matumbo ya ghafla!

EL2015

Nimesema sana kuhusu Lowassa, magamba hawasikii. Bila Lowasa 2015, CDM haitapiga kampeni. CDM inamhofia Lowasa pekee kama atasimama kwa tiketi ya magamba!
 
ok bwana kila mtu na maoni yake unaona anafaa lowasa mpe kura yako,si ndiyo uhuru/haki
ya kila mtu wa kikatiba.ila mimi naona kama watamsimamisha wasira(tyson)huyu atatufaa zaidi.ccm
tufikirie zaidi juu ya hili.
Ni kweli mkuu lakini wasira hawezi kuchukua form mbele lowassa uwezo huo hana kabisa
 
Mpaka anaiba kote huko na kwa kiwango hicho hakuchukuliwa hatua zozote?

Kwani nchi hii haina vyombo vya usalama?

Hebu acheni porojo elezeni ukweli kuwa mnafuata mkondo msioujua wa siasa chafu!

Hapa ss unanishangaza,hasa achukuliwe hatua na nani?......wangapi unawajua ww wnye case km hizo wamechukuliwa hatua zaidi ya kujiuzulu?...acheni kutetea ujinga! Yy km anaona hana kosa aitishe press conference aongee ukweli,ndo nitaamini kweli yy ni nguli,Full stop!,hatutaki habari za ushahidi hapa
 
Hapa ss unanishangaza,hasa achukuliwe hatua na nani?......wangapi unawajua ww wnye case km hizo wamechukuliwa hatua zaidi ya kujiuzulu?...acheni kutetea ujinga! Yy km anaona hana kosa aitishe press conference aongee ukweli,ndo nitaamini kweli yy ni nguli,Full stop!,hatutaki habari za ushahidi hapa

Mkuu ili uitwe fisadi ni lazima vyombo vya dola ikiwemo mahakama vikuthibitishie!

Hayo unayoyaamini ni ya dhahania tu!
 
Mkuu mbumbumbu ondoa shaka, kimsingi ndani ya ccm, mwenyekiti yupo tayari CDM ibebe nchi ila sio Lowassa kuwa rais kupitia ccm,

Lowassa keshajua kuwa hali kwake ndani ya ccm upepo umegeuka baada ya kudhani jk yupo nae kumbe kamtosa!

Mkuu ccm hata isimamishe wagombea watatu haishindi!

Hata leo aamke mzee Nyerere pale Butiama kisha aambiwe agombee atakataa katakata kwa kuogopa aibu ya karne!


hizi hoja za kishabiki shabiki sana...haina mantiki
 
Mkuu ili uitwe fisadi ni lazima vyombo vya dola ikiwemo mahakama vikuthibitishie!

Hayo unayoyaamini ni ya dhahania tu!

Ok....unachosema ni kweli,kwamba lzm mahakama ithibitishe!...bt kwny hii TZ yetu hizo sheria zinafuatwa?...zaidi ya kutumika kwa vidagaa,then mapapa na manyangumi kuachwa au kushinda kesi? Tuwe wakweli tu,tuweke ushabiki pembeni!
 
Ok....unachosema ni kweli,kwamba lzm mahakama ithibitishe!...bt kwny hii TZ yetu hizo sheria zinafuatwa?...zaidi ya kutumika kwa vidagaa,then mapapa na manyangumi kuachwa au kushinda kesi? Tuwe wakweli tu,tuweke ushabiki pembeni!
Ikiwa vyombo vyetu vya dola vimeshindwa kututhibitishia ufisadi wa Lowassa nini kifanye?
 
Hapo kwenye RED Lowasa hakuwahi kujialika kanisani, huwa anaalikwa na viongozi wa makanisa husika kwa kuwa ni mtoaji mzuri yeye na marafiki zake. Hivyo hata wenye msikiti wakimwalika hakatai mwaliko na atawachangia vile vile.
Kawashauri viongozi wako wa dini waandae mwaliko fasta.

Mnyonge, mnyongeni lakini haki yake mumpe.
Lowasa simpendi ila kwa hili nitamtetea.


anahonga pesa nyingi sana ili ahalikwe ili ajisafishe¬! he is purely dirty!
 
Back
Top Bottom