Mkimgusa Edward Lowassa mtasahaulika katika siasa za Tanzania!

Mkuu mimi siongei maneno mareeeeefu!

Naomba ushahidi wa ufisadi wake tu!
 
Bora kuvaa kofia za Lowassa kuliko mgombea mwingine ndani ya CCM jamaa ananifurahisha jinsi anavyo wafyatisha Mkia hao wanao jiita wenye chama
 
Hahaa hawanajeuri ya kumkanya wala kunyoosha kidole juu ya Lowassa!
Kaka yericko naunga mkono na mguu hoja, Na ccm hawawezi mwonya hata siku moja,katika historia hakuna siku mtoto alisha mfumania mama yake au baba hivyo ccm wanyaze kimya tu. tunasubiri bwn mayega aseme mwl nyerere alimweleza nini edward kura yangu anayo haina shida.
 

Nilikuwa sijakusoma,ila hapa nimekuelewa.
 
Haya bana! Lakini mjue wapiga kura halisi tuko kimya maana tunajua nani tutamchagua siku hiyo kuongoza nchi. Nyie wasomi (msiokuwa na muda wa kwenda kupanga foleni kupiga kura) endeleeni kujadili ndoto msizoweza kutimiza!
 
Unajua CDM wanatapatapa sana yaani wanafikirui ccm ni kama CDM.Kwa taarifa yako CCM hawachagui mgombea kwa ukwasi au fitina wanaangalia mambo ya msingi na yenye manufaa kwa Taifa.Uzalendo kwanza,mtu baadae.Hivyo huyo CDM mnaemtaka awe mgombea wa CCM wala hatakuwa kwa CCM ina wanachama wanaojua ni mtu wa aina gani anaefaa kupeperusha bendera ya CCM na kupata ushindi wa Kishindo.
 
Ni yeyote yule lakini siyo EL,
Wewe uogopi hata hilo jina unalotumia? Mwenye hilo jina kabla hajafa alishasema EL hafai wewe ni nani wa kumsafisaha mpaka atakasike?
Alikuwa mungu? Alitoa sababu za kumkataa? Je wewe unasababu za kumkataa?

Usiwe mtu wa kuambiwa tafakari mkuu!
 

Kwa hili utakuwa umebaki mwenyewe na wahafidhina wengine wachache "the Hear no evil, See no evil type of praise singers"!! The fact that may be JK was informed about richmond can not absolve EL of the blame, kwa hiyo kama alivyofanya then kuwajibika kisiasa ilikuwa sahihi vinginevyo siku ile alipopewa fursa na spika wa UKWELI Sam Sitta aliambie taifa kuhusu alichokijua kuhusu sakata hilo yeye akaishia kulalama kwamba "Tatizo ni uwaziri mkuu" badala ya kutoa full account ya mradi aliousimamia kwa nguvu zake zote na vimemo kedekede! then kwa mshangao wa watu wengi akatamka "Naachia ngazi"
So EL still has to come clean and tell the nation kwa nini kama mikono yake ilikuwa misafi then why did he decide to jump instead of waiting to be pushed"
It is better for him to stay out in the cold than open a pandoras box which he may not survive at all given what is already in the public domain since the unravveling of the infamous Richmonduli saga.
 
Haya bana! Lakini mjue wapiga kura halisi tuko kimya maana tunajua nani tutamchagua siku hiyo kuongoza nchi. Nyie wasomi (msiokuwa na muda wa kwenda kupanga foleni kupiga kura) endeleeni kujadili ndoto msizoweza kutimiza!
Usijali tupo pamoja siku ya siku mbele ya sanduku la kura!

EL2015
 

Mkuu, yote kwa yote mimi naomba kama unaushahidi wa ufisadi wa Lowassa uuweke hapa!

Hizo hadithi za kufikirika hazina mafaa kwa siasa safi labda kwa siasa za majitaka tu!
 

Kukikomboa chama HAPANA ila nakubaliana na wewe kuwa hakuna ufisadi mwingine anaotuhumiwa LOWASA zaidi ya RICHMOND na pia huyu jamaa ni MCHAPAKAZI wa kweli, angalia shule za kata zilivyokuwa nyingi na amaewaachia jamaa kuzalisha wakimu wa kutosha ila WANACHEMSHA
Anaejiita mtoto wa MKULIMA hana lolote kila kitu anaomba ruhusa kwa BWANAMKUBWA hana maamuzi yake hata kama akikosea
 
huwa sipendi kuongea sana


Tangia amalize Elimu yake Chuo Kikuu DSM miaka ya katikati ya 70,ambako pia ndiko alipokutana na Mkewe Regina, na baadae kwenda Nottingham, Uingereza kwa elimu ya juu zaidi mwishoni mwa miaka ya 70,ENL hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa au kiutendaji ndani ya serikali. Kabla ya mwaka 1985, ENL aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCMmikoa ya Shinyanga (ambako mtoto wake Fred ndiko alipozaliwa) na pia kushikilia nafasi hiyo hiyo Arusha miaka ya mwanzo ya 80.
Katika kipindi cha 1980 hadi mwaka 1988, ENL hakuwa anamiliki nyumba ya aina yoyote, na alikuwa na gari moja tu aina ya Volkswagen namba TAP 180, kwa miaka mingi sana. Nyumba ya kwanza ya ENL, mbali na ya kwa wazazi
vijijini ilikuwa ni flat ya Msajili wa Majumba pale Sanawari Arusha kama mpangaji, akiwa CCM Arusha.

Miaka michache baadae, alibahatika kupata nyumba nyingine ya msajili kama mpangaji, mtaa wa mahando, Masaki Dares-salaam.Mambo yakaanza kubadilika kuanzia Mwaka 1989 baadaya Mzee Mwinyi kumteua kuwa Mkurugenzi wa Kitu cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Nafasi hii aliitafuta mwenyewe. Mwaka 1990, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Waziri Mkuu mteule (1990),John Malecela, kumuomba Mzee Mwinyi. Mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mara nyingi wanapatikana baada ya Rais kushauriana na waziri mkuu.Mwaka 1991, Mwinyi akamhamishia ENL Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, na hapo ndipo alipokutana na Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa NHC,na kuanza urafiki mkubwa sana wa kikazi na kimaslahi. Mwaka muhimu kukumbuka ni ule wa 1992 ulioruhusu viongozi wa CCM na Serikali kumiliki mali. Kufikia mwaka 1994, ENL akawa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya kuwana nyumbazakupanga,mojawapoikiwamakaziyaBaloziwaAfrika KusiniTanzania kulemasakiambapo alikuwa analipwa $5,000 kama kodi ya mwezi kuanzia mwaka 1994. Mandela alipokuja Tanzania, alitembelewa na Nyerere palekwa Balozi, na kufanya Press Conference pale pale. Ni katika hafla ile ndio Nyerere akaambiwa ile ni nyumba ya ENL, kitu kilichomsononesha sana. Ndipo Nyerere akatumia nafasi ile kufanya uchunguzi zaidi na kubaini mengi.

TISS walimtengenezea Mwalumu Faili maalum juu ya hilo. Mwaka 1995, Mwalimu alikuwa anatembea katika vikao vyote vya maamuzi alipokuwa anaalikwa kutoa msimamo wake juu ya wagombea. Alipomfuta ENL, mtandao wote ulifyata,na aliebakia kumtetea ENL alikuwa ni Sitta ambae alimweleza Mwalimu waziwazi kwenye vikao kwamba sasa ni zamu ya vijana, na wamechoka kuendelea kuchaguliwa na wazee. Mwalimu alibishana sana na Sitta, na baadae Mwalimu akamwambia "Wewe ni waziri wa sheria na katiba, sasa kwa nafasi yako, nimepewa faili juu ya mtu huyu, naomba uchukue faili hili la ENL, na kwa nafasi yako kama waziri wa sheria, utusaidie kufafanua yaliyomo humo ili tubaini kama ENL anaonewa." Sitta akakaa chini na hakusimama na wala kuzungumza tena.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, ENL alitupwa nje ya baraza la mawaziri kutokana na shinikizo la Nyerere. Kikwete ilikuwa ngumu kumuacha kwenye baraza kwani alikuwa namba mbili kule chimwaga (akiwa namba moja katika
matokeo ya awali). Njia pekee ya kuumaliza Kikwete ikawa ni kumpa uwaziri wa mambo ya nje ili asiwe na wizara yenye mashiko na wapiga kura (mfani kilimo n.k), lakini pia kumtoa katika mizunguko/ziara ndani ya nchi, hivyo kupunguza nguvu yake katika grassroots level. Walichokosea kina Mkapa ni kwamba kwa ENL kuwa nje ya baraza, ilimpa muda mwingi sana kuendelea na mikakati ya 2005. Lakini ENL pia aliumia sana, na aliyemrudisha kwenye
Cabinet ni Abson, baada ya kumuombea sana msamaha kwa Mkapa.

ENL hakuacha kuendelea kujijengea mtandao kwa ajili ya mwaka 2005 na baadae. ENL hajijengei mtandao kwenye siasa tu bali kwenye vyombo vya usalama, taasisi za Umma, Binafsi n.k. Ana mtandao mkubwa sana kwenye sekta za Umma kama Ewura ambako alimweka ndugu yake Haruna Masebu ambae alikuwa NHC, ENL alipokuwa waziri wa ardhi. ENL pia ana mtandao mkubwa sana TRA, Tanesco, kampuni za mawakili, wamiliki wa ma-baa, taasisi mbalimbali za kidini (dinizote), polisi, TISS, taasisi za kimataifa zenyewawakilishi wake Tanzania, n.k.

Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa "his fallback position" (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO,
waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo. Pia walikuwa wanalalamika sana kwamba hawapati kabisa muda na Waziri wa Mambo ya Nje, na hivyo katika kipindi cha miaka kumi (1995 – 2005), kuishia kuwa na ukaribu zaidi na manaibu mawaziri wan je, katika nyakati tofauti, Balozi Shariff na Mwambulukutu.

Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoawengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA,akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

Kuhusu Kikwete kujiunga na kina Lowassa, swali la kujiuliza ni je, kamaNyerere alishindwa kuwazuia mwaka 1995, na baadae Nyerere kufanikiwa kwa mbinu za kiintelejensia, Mkapa atawezaje kuwa kambi tofauti na ENL
katika mazingira ya sasa? Suala lingine la kujiuliza hapa - nini kilibadili msimamo wa Sitta (mwaka2007) juu ya ENL ikifananishwa na misimamo yake huko nyuma juu ya ENL - mwaka 1995 na mwaka 2005? Msimamo wake (Sitta) Sitta ulimgharibu sana kisiasa kwani alitoweka kabisa katika nafasi ya uwaziri kwa kipindi chote cha Mkapa 1995 – 2005, huku ENL na Kikwete wakiendelea kupeta......


ngoja niishe hapa kwanza...ntarudi
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…