Mkimgusa Edward Lowassa mtasahaulika katika siasa za Tanzania!

see the point is to restore public confidence. Tangu ijulikane kuwa ni fisadi hajakanusha waziwazi na jk/serikali ikashindwa kujitetea kama unavyosema. Mwambie aitishe press conference ajisafishe
 
chondechonde kikwete achana na agenda hiyo ya upole, inakiua chama chako na serikali yako,

ni karibu miezi 28 sasa, edward lowassa amekuwa agenda kuu ndani ya ccm na wanaccm wenye, si mwenyekiti wala mjumbe wote mioyo yao ni lowasa tu, wengi wakitaka ajipambanue nakuwa nyota huru ya chama na wachache walio juu ya chama wakitaka kumpoteza gwiji huyu wa siasa za ukwasi na fitina msonge!

Ikumbukwe kuwa doa kuu linalotajwa kuwa lowa ni fisadi ni richmond, lakini nani asiyejua richmond ni nani na ilikuwaje? Pale dodoma lowasa ameweka wazi mbele ya mwenyekiti kuwa hakuna kilichotendeka ambacho mwenyekiti hakukijua ama kumtuma! Narudia tena uchafu wa lowassa ni richmond tu!

Nauliza tena richmond ni nani? Mwenyekiti alijibu nini siku ile pale dodoma wakati lowassa anamhiji zaidi ya kuinamisha kichwa chini hali iliyopelekea bwm kumtuliza lowasa?

Sasa lowassa anakitaka chama na agombee urais na ameshashinda ndani ya chama na nusu uwanja nje ya chama, shime ccm, ili muendelee kuitwa chama cha siasa japo mwaweza kuwa wapinzani zuieni jaribio la mwenyekiti wenu la kujaribu kumzika lowassa angali amekibeba chama!

Kuna juhudi za kitoto ndani ya ccm eti wapo kwenye harakati za kumuuandaa january makamba kugombea urais 2015, wanatumia raslimali za nchi kujijenga kisiasa kwa upinde wa mvua ya siasa!

Chondechonde mwenyekiti wa ccm ndugu jakaya mrisho kikwete, amini lowassa ndie chaguo la wanaccm wote hata hao wanaojifanya wapo na wewe mioyo yao ipo kwa lowassa! Wanakula na kunywa kwa mgongo wa lowassa!

Mwenye ushahidi wa wazi juu ya ufisadi wa lowassa aulete hapa, sio stori za kulishwa vijiweni kisha mnakuja hapa kupiga ngonjera ooho lowasa fisadi, oooho sijui nini! Leteni utetezi hapa

mimi nitampa kura yangu ikiwa atagombe japo hata shinda, lakini atakinusuru chama kufutika kabisa duniani!

Rejao, zomba, malaria sugu msianze kuugua matumbo ya ghafla!

El2015

you are too cheap ndo maana unaongea hivyo! Who is lowasa takataka tu! Vimekuwepo visiki hapa dunia mwisho vimeng'oka sembuse huyu mwizi???? Utajiuza, utavuliwa chupi utafanya vyovyote lakin urais sahau! Shiiitttts!
 
huwa sipendi kuongea sana


Tangia amalize Elimu yake Chuo Kikuu DSM miaka ya katikati ya 70,ambako pia ndiko alipokutana na Mkewe Regina, na baadae kwenda Nottingham, Uingereza kwa elimu ya juu zaidi mwishoni mwa miaka ya 70,ENL hakuwahi kushika wadhifa wowote mkubwa au kiutendaji ndani ya serikali. Kabla ya mwaka 1985, ENL aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa CCMmikoa ya Shinyanga (ambako mtoto wake Fred ndiko alipozaliwa) na pia kushikilia nafasi hiyo hiyo Arusha miaka ya mwanzo ya 80.
Katika kipindi cha 1980 hadi mwaka 1988, ENL hakuwa anamiliki nyumba ya aina yoyote, na alikuwa na gari moja tu aina ya Volkswagen namba TAP 180, kwa miaka mingi sana. Nyumba ya kwanza ya ENL, mbali na ya kwa wazazi
vijijini ilikuwa ni flat ya Msajili wa Majumba pale Sanawari Arusha kama mpangaji, akiwa CCM Arusha.

Miaka michache baadae, alibahatika kupata nyumba nyingine ya msajili kama mpangaji, mtaa wa mahando, Masaki Dares-salaam.Mambo yakaanza kubadilika kuanzia Mwaka 1989 baadaya Mzee Mwinyi kumteua kuwa Mkurugenzi wa Kitu cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC). Nafasi hii aliitafuta mwenyewe. Mwaka 1990, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Waziri Mkuu mteule (1990),John Malecela, kumuomba Mzee Mwinyi. Mawaziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mara nyingi wanapatikana baada ya Rais kushauriana na waziri mkuu.Mwaka 1991, Mwinyi akamhamishia ENL Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, na hapo ndipo alipokutana na Haruna Masebu kama Mkurugenzi Mkuu wa NHC,na kuanza urafiki mkubwa sana wa kikazi na kimaslahi. Mwaka muhimu kukumbuka ni ule wa 1992 ulioruhusu viongozi wa CCM na Serikali kumiliki mali. Kufikia mwaka 1994, ENL akawa mmoja wa viongozi wa kizazi kipya kuwana nyumbazakupanga,mojawapoikiwamakaziyaBaloziwaAfrika KusiniTanzania kulemasakiambapo alikuwa analipwa $5,000 kama kodi ya mwezi kuanzia mwaka 1994. Mandela alipokuja Tanzania, alitembelewa na Nyerere palekwa Balozi, na kufanya Press Conference pale pale. Ni katika hafla ile ndio Nyerere akaambiwa ile ni nyumba ya ENL, kitu kilichomsononesha sana. Ndipo Nyerere akatumia nafasi ile kufanya uchunguzi zaidi na kubaini mengi.

TISS walimtengenezea Mwalumu Faili maalum juu ya hilo. Mwaka 1995, Mwalimu alikuwa anatembea katika vikao vyote vya maamuzi alipokuwa anaalikwa kutoa msimamo wake juu ya wagombea. Alipomfuta ENL, mtandao wote ulifyata,na aliebakia kumtetea ENL alikuwa ni Sitta ambae alimweleza Mwalimu waziwazi kwenye vikao kwamba sasa ni zamu ya vijana, na wamechoka kuendelea kuchaguliwa na wazee. Mwalimu alibishana sana na Sitta, na baadae Mwalimu akamwambia “Wewe ni waziri wa sheria na katiba, sasa kwa nafasi yako, nimepewa faili juu ya mtu huyu, naomba uchukue faili hili la ENL, na kwa nafasi yako kama waziri wa sheria, utusaidie kufafanua yaliyomo humo ili tubaini kama ENL anaonewa.” Sitta akakaa chini na hakusimama na wala kuzungumza tena.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, ENL alitupwa nje ya baraza la mawaziri kutokana na shinikizo la Nyerere. Kikwete ilikuwa ngumu kumuacha kwenye baraza kwani alikuwa namba mbili kule chimwaga (akiwa namba moja katika
matokeo ya awali). Njia pekee ya kuumaliza Kikwete ikawa ni kumpa uwaziri wa mambo ya nje ili asiwe na wizara yenye mashiko na wapiga kura (mfani kilimo n.k), lakini pia kumtoa katika mizunguko/ziara ndani ya nchi, hivyo kupunguza nguvu yake katika grassroots level. Walichokosea kina Mkapa ni kwamba kwa ENL kuwa nje ya baraza, ilimpa muda mwingi sana kuendelea na mikakati ya 2005. Lakini ENL pia aliumia sana, na aliyemrudisha kwenye
Cabinet ni Abson, baada ya kumuombea sana msamaha kwa Mkapa.

ENL hakuacha kuendelea kujijengea mtandao kwa ajili ya mwaka 2005 na baadae. ENL hajijengei mtandao kwenye siasa tu bali kwenye vyombo vya usalama, taasisi za Umma, Binafsi n.k. Ana mtandao mkubwa sana kwenye sekta za Umma kama Ewura ambako alimweka ndugu yake Haruna Masebu ambae alikuwa NHC, ENL alipokuwa waziri wa ardhi. ENL pia ana mtandao mkubwa sana TRA, Tanesco, kampuni za mawakili, wamiliki wa ma-baa, taasisi mbalimbali za kidini (dinizote), polisi, TISS, taasisi za kimataifa zenyewawakilishi wake Tanzania, n.k.

Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa “his fallback position” (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO,
waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo. Pia walikuwa wanalalamika sana kwamba hawapati kabisa muda na Waziri wa Mambo ya Nje, na hivyo katika kipindi cha miaka kumi (1995 – 2005), kuishia kuwa na ukaribu zaidi na manaibu mawaziri wan je, katika nyakati tofauti, Balozi Shariff na Mwambulukutu.

Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoawengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA,akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

Kuhusu Kikwete kujiunga na kina Lowassa, swali la kujiuliza ni je, kamaNyerere alishindwa kuwazuia mwaka 1995, na baadae Nyerere kufanikiwa kwa mbinu za kiintelejensia, Mkapa atawezaje kuwa kambi tofauti na ENL
katika mazingira ya sasa? Suala lingine la kujiuliza hapa - nini kilibadili msimamo wa Sitta (mwaka2007) juu ya ENL ikifananishwa na misimamo yake huko nyuma juu ya ENL - mwaka 1995 na mwaka 2005? Msimamo wake (Sitta) Sitta ulimgharibu sana kisiasa kwani alitoweka kabisa katika nafasi ya uwaziri kwa kipindi chote cha Mkapa 1995 – 2005, huku ENL na Kikwete wakiendelea kupeta......


ngoja niishe hapa kwanza...ntarudi

Umetoa simulizi nzuri sana juu ya EL hata wale waliokuwa wanasita kumpa kura sasa watampa!

Lakini jambo kuu muhimu ni kuthibitisha UFISADI wa Lowassa!

Ungekuwa umemmaliza kabisa laiti hilo faili alilokabidhiwa Mzee Nyerere na TISS ungelimwaga hapa tulichambue hatua kwa hatua!

Nazidi kusisitiza mwenye pingamizi dhidi ya Lowassa na alete pingamizi lake lenye kujitosheleza hapa!

Lowassa SIO FISADI hata chembe!
 
you are too cheap ndo maana unaongea hivyo! Who is lowasa takataka tu! Vimekuwepo visiki hapa dunia mwisho vimeng'oka sembuse huyu mwizi???? Utajiuza, utavuliwa chupi utafanya vyovyote lakin urais sahau! Shiiitttts!

Hehee Lowasa MWIZI wa nini? Lete hapa ushahidi wa wizi au ufisadi wake!
 
Acheni ndoto hapa! Mwenye ushahidi wa ufisadi wa Lowasssa aumwage hapa. Msiishi kwa majungu. Mimi namkubali sana.

EL haogopewi na yeyote isipokuwa ukweli ni kwamba nani wa kumtoa mwenzie kibanzi ktk jicho wakati wanachama wa ccm walio katika kamati na wasiokuwapo wanavitu katika macho yao? Je ni kweli EL ndiye aliyesababisha ukosefu wa ajira kwa vijana wa kitanzania?, je ndiye anasababisha hali ngumu ya maisha kwa watanzania, na je ndiye anasababisha utendaji mbovu wa serikali kuu katika kukamilisha malengo yake? Na kama leo ataamua kutoka CCM ili aikoe CCM UNA HAKIKA CCM ITAFANIKIWA? KWA KIPI KITAKACHOFANYIKA. Naomba ieleweke mwisho wa jambo ukifika hakuna sababu itakayozuia, Ssemei ushabiki CCM wakati wa kuishi umekuishia KUBALI badilisha jina la chama jipange upya ingia kazini baadaye sana kurudi kwenye dola kama YESU atakuwa bado kuchukua KANISA LAKE. ASILAUMIWE KIKWETE, NAPE, MUKAMA, EL, WALA WAJUMBE WA KAMATI KUU!
 
kila nikisikia huyu jamaa kugombea urais ccm naagiza bia,maana nafahamu CDM 2015 HIYOOOOOOOOOOOOOOO INAJONGEA
 
Umetoa simulizi nzuri sana juu ya EL hata wale waliokuwa wanasita kumpa kura sasa watampa!

Lakini jambo kuu muhimu ni kuthibitisha UFISADI wa Lowassa!

Ungekuwa umemmaliza kabisa laiti hilo faili alilokabidhiwa Mzee Nyerere na TISS ungelimwaga hapa tulichambue hatua kwa hatua!

Nazidi kusisitiza mwenye pingamizi dhidi ya Lowassa na alete pingamizi lake lenye kujitosheleza hapa!

Lowassa SIO FISADI hata chembe!


invincible ignorance!!

 
kila nikisikia huyu jamaa kugombea urais ccm naagiza bia,maana nafahamu CDM 2015 HIYOOOOOOOOOOOOOOO INAJONGEA
Ndio kusudi la sisi wote wenye mapenzi mema na nchi hii,

Kwapamoja tuhakikishe Lowasa anagombea 2015 ili chadema tuingie magogoni bila jasho!
 
Kilasiku wanazunguka Mbuyu lakini hamna anayejaribu kuugusa na pia anauwezo wa kuzungumzia mahali popote na kuwakemea viongozi wote wa CCM mpaka Mkuu na wasimfanye chochote huyo ni mwamba Ndani ya CCM. jamaa akichukua form ya Urais ndani ya CCM lazima wafyate mkia wote

kosa la Ngoyayi ni kuiba au kushiriki wizi(conspiracy). Yaani alishirikiana na Jehikeh kuiba kupitia rechmondi au alimwona mkulu anaiba akaamua ambebe mshikaji at expense ya wa-tz. Angejiuzulu kwa sababu amesirishwa na wizi angezoa kura za wanachadema wote. kwa sasa its too late kujisafisha na kutoka salama nje ya madirisha hayo mawili
 
kosa la Ngoyayi ni kuiba au kushiriki wizi(conspiracy). Yaani alishirikiana na Jehikeh kuiba kupitia rechmondi au alimwona mkulu anaiba akaamua ambebe mshikaji at expense ya wa-tz. Angejiuzulu kwa sababu amesirishwa na wizi angezoa kura za wanachadema wote. kwa sasa its too late kujisafisha na kutoka salama nje ya madirisha hayo mawili

Ajiuzuru kutumwa na bosi wake? Sio asili ya siasa za afrika mkuu!

Yeye alitumwa na alitekeleza kisha katoka na yuumsafi bila mawaa!

Hata jehikehi aje hapa aseme Lowassa ni fisadi na atuthibitishie hapahapa!
 
Ndio kusudi la sisi wote wenye mapenzi mema na nchi hii,

Kwapamoja tuhakikishe Lowasa anagombea 2015 ili chadema tuingie magogoni bila jasho!

Halafu Mkuu kinacho nifurahisha zaidi huyu Mwamba akichukua form hamna wakushindana naye huko CCM kwasababu hamna msafi kuliko yeye ambaye aliweza kujiuzulu kuokoa serikali isiangamie hii itatusaidia sisi CDM kusimamisha hata jiwe nakupata ushindi kilaini
 
ivi unajua ukimtetea mtu umjue kiundani ndugu zangu hapo lowassa na kikwete wake hakuna msafi ivi unajua kuwa bwana kikwete akijaga monduli huwa wanaingia kwenye chumba cha siri kuongea mambo yao na kikwete na hakuna anayeruhusiwa kuingia hata mlinzi wake wewe una hiyo habari?ivi unajua siku lowassa alipojiuzulu aliletewa magari ma3 na baba riz sasa hapo unaona kwa uhusiano huo tu kuna mwaminifu hapo
 
Mkuu Yericko Nyerere nimeamini hii thread ilikuwa sumu kwa wale pro-ccm kama wakina Ritz, Tume ya Katiba , Mafilili, Zomba na Rejao utafikiri walikuwa na ban. waoga sana mbona sisi za zitto na cdm tunaingia? Tuntemenke kaingiza ya kwake akala ban ndio wamezoea kama hizo
 
Halafu Mkuu kinacho nifurahisha zaidi huyu Mwamba akichukua form hamna wakushindana naye huko CCM kwasababu hamna msafi kuliko yeye ambaye aliweza kujiuzulu kuokoa serikali isiangamie hii itatusaidia sisi CDM kusimamisha hata jiwe nakupata ushindi kilaini

Kumbe umenisoma vema kamanda,

Naona pro ccm kama zomba kajigandisha kwenye thread yake ya Zitto, kutwa kucha ana refresh na kucomment upuuzi tu!

Kama wana hoja waje wajibu hapa maana mimi nilishawafuata hukohuko na nikawajibu kuwa chadema hatufanyiki kazi kwamaelekezo ya wanaccm bali kanuni na katiba ya chama ndio hutuongoza!

Sasa tunasema Lowassa anafaa wakimutosa, wajue wamejitosa wao!
 
ivi unajua ukimtetea mtu umjue kiundani ndugu zangu hapo lowassa na kikwete wake hakuna msafi ivi unajua kuwa bwana kikwete akijaga monduli huwa wanaingia kwenye chumba cha siri kuongea mambo yao na kikwete na hakuna anayeruhusiwa kuingia hata mlinzi wake wewe una hiyo habari?ivi unajua siku lowassa alipojiuzulu aliletewa magari ma3 na baba riz sasa hapo unaona kwa uhusiano huo tu kuna mwaminifu hapo

Hayo nayasikia toka mdomoni mwako kama wewe ulivyosikia, na huwa siyafanyii kazi japo huyasikiliza!

Ninachotaka ni ushahidi wa ufisadi wa Lowassa uletwe hapo!
 
Mkuu Yericko Nyerere nimeamini hii thread ilikuwa sumu kwa wale pro-ccm kama wakina Ritz, Tume ya Katiba , Mafilili, Zomba na Rejao utafikiri walikuwa na ban. waoga sana mbona sisi za zitto na cdm tunaingia? Tuntemenke kaingiza ya kwake akala ban ndio wamezoea kama hizo

Hahaaha waje tuwafundishe siasa za kistaarabu na za fitina zilizochanganyika na majitaka!
 
Hayo nayasikia toka mdomoni mwako kama wewe ulivyosikia, na huwa siyafanyii kazi japo huyasikiliza!

Ninachotaka ni ushahidi wa ufisadi wa Lowassa uletwe hapo!

unataka ushahidi ok iyo kazi rahisi sana kipindi kuna sakata la richmond waziri mkuu alikuwa lowassa na inaonesha kulikuwa kuna makubaliano baina yao hawa wawli lowasaa na kikwete sasa hapo kuna msafi angekuwa msafi angekubali huu upuuzi kama anawapenda kweli wananchi wake wa tanzania............
 
Hakunaaaa msafiii hapo wote ni mafisadi tu mimi binafsi siwezi kuteteaa ujinga kama huo
 
Back
Top Bottom