Mkiambiwa mke wa mtu sumu nimeamini sumu kweli

Huna kosa mkuu huyo mwanaume kama angeleta shida nae angekuwa mbweha tu kwa sababu hukuwa unamjua. Huyo mkewe nae chenga kwa mwanamke mwenye akili kwenye mazingira kama hayo angekutambulisha au angekujulisha yupo na baba watoto usilipie nauli.
asee kwamba huyo mwanamke jamaa ataenda nae kila mahali mwanamke kama anajielewa anajielewa tu kama ni kwa kuliwa ataliwa hata bila kulipiwa nauli
 
Umepigwa nauli kizembe Sana, hapo matumaini yako ilikua ni kuomba namba, matumaini yako yaliyeyuka baada ya sauti ya konda kusema dada keshalipiwa, ulitamani kumwambia konda chukua hiyo ya mmewe u irudishie ya kwangu ila ukaona aibu..
 
Jana nimepanda daladala ile kuingia tu nikakaa siti moja na mdada kumbe yeye ananifaham na mimi nilishamsahau, kumbe niliwahi kufanya nae kazi kipindi flani, akaanza kunichangamkia kwa stori mbili tatu, hapo hapo konda kudai nauli nikamlipia na yeye.

Kumbe bwana yule dada siti ya nyuma alikuwa amekaa mumewe na mtoto wao mchanga aloo, ile konda anadai nauli siti ya nyuma mumewe nae akalipa ila konda akamwambia huyo dada hapo mbele kashalipiwa.

Mumewe akawa anawasiwasi kalipiwa kivipi, ile wanashuka yule dada kuniaga mumewe kanikata jicho sio la nchi hii

Na kwa bahati nzuri sikuomba hata namba ya sim sijui ningeomba ingekuwaje aloo, , ila niwasihi tu mkifika mahali mkakuta wanawake wamekaa sehem msome kwanza mazingira wengine huwa wapo karibu na waume zao
Uzi huu utakimbiza sana
 
Nilikusoma tangu muda, maamuzi yangu yatakuwa ya chini chini ila yenye maumivu makali. Nakusihi linda hayo maspika yako, vijana wangu wa kazi wapo na picha yako
 
Ivi kwamba kuwa mume ndo unaweza kupigana au mbona kila siku wanaume tunatishana na kupigana kwa ishu mbali mbali hili la mume kuonekana ye ndo atashinda vita tu kila siku limekaaje
Jaribu kuchukua mke wa mtu chief halafu mumewe akufumeni ndio utajua nani mshindi.
 
Back
Top Bottom