Mkiambiwa Kitenge, Zembwela na PJ ni wajinga msiwe wabishi

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Wajumbe, mara kadhaa mmekuwa mkiambiwa kuwa wachekeshaji wa redio ya Wasafi Maulid Kitenge, Zembwela na Paul James au PJ ni wajinga, wavivu wa kufikiri na pengine wanaoshambiliwa na ugonjwa mbaya wa ujinga msiwe mnabisha.

Leo asubuhi wameendeleza komedi yao huko Morogoro wakiendelea na kile wanachokiita "Wekeza Tanzania ya Samia". Hapa walikuwa "serious" kumshauri RC wa Mkoo huo Adam Malima wakisema;

"Mhe, unajua sisi tunazunguka sana ndani na nje ya nchi wananchi wengi sana wanatuambia na hata kabla ya kuja hapa wametuomba tukuambie hivi,

"Kwa kuwa Moro Kuna fursa nyingi za uchumi kama Utalii, Kilimo nakadhali wanaomba ujenge hapa kiwanja kikubwa Cha ndege kama Julius Nyerere International Airport ili watu wawe wanakuja na midege mikubwa ya mizigo kuchukua bidhaa hapa hapa na kuruka nayo kwenda Ulaya". Wote wakaitikia hata na PJ ambaye walau amesoma kidogo kati Yao.

Yani hawa wachekeshaji hawaioni uwanja wa ndege unaojengwa Msalato Dodoma. Hawaioni JNIA. Hawaioni SGR. Eti Hawa ndio watetezi wa DP World! Hebu Serikali tuweni basi serious hata mara moja moja kwa mwaka.
 
Wajumbe, mara kadhaa mmekuwa mkiambiwa kuwa wachekeshaji wa redio ya Wasafi Maulid Kitenge, Zembwela na Paul James au PJ ni mazwazwa, wavivu wa kufikiri na pengine wanaoshambiliwa na ugonjwa mbaya wa ujinga msiwe mnabisha.

Leo asubuhi wameendeleza komedi yao huko Morogoro wakiendelea na kile wanachokiita "Wekeza Tanzania ya Samia". Hapa walikuwa "serious" kumshauri RC wa Mkoo huo Adam Malima wakisema;

"Mhe, unajua sisi tunazunguka sana ndani na nje ya nchi wananchi wengi sana wanatuambia na hata kabla ya kuja hapa wametuomba tukuambie hivi,

"Kwa kuwa Moro Kuna fursa nyingi za uchumi kama Utalii, Kilimo nakadhali wanaomba ujenge hapa kiwanja kikubwa Cha ndege kama Julius Nyerere International Airport ili watu wawe wanakuja na midege mikubwa ya mizigo kuchukua bidhaa hapa hapa na kuruka nayo kwenda Ulaya". Wote wakaitikia hata na PJ ambaye walau amesoma kidogo kati Yao.

Yani hawa wachekeshaji hawaioni uwanja wa ndege unaojengwa Msalato Dodoma. Hawaioni JNIA. Hawaioni SGR. Eti Hawa ndio watetezi wa DP World! Hebu Serikali tuweni basi serious hata mara moja moja kwa mwaka.
Eti Hawa ndio watetezi wa DP World! Hebu Serikali tuweni basi serious hata mara moja moja kwa mwaka.
Screenshots_2023-07-07-10-52-49.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mazwazwa hawajui kuwa mkoa wa Morogoro hauna uwanja wa ndege jwa sababu za kiusalama?
 
Kama wamesema uwanja wa ndege ujengwe morogoro hawajui chochote.Kwanza anga ya morogoro ni military controlled airspace ,ndio maana hakuna airport kwa ajili ya commercial operation. Kingine huyo kitenge na wenzake wajifunze uwanja wa ndege wa kimataifa haujengwi mahali ni mahali . Kuna vigezo vinapaswa kufikiwa na wala sio tu vya ndani bali vya kimataifa vya IATA, ICAO na vya FAA. Akiwa kama mwandish wa habari anapaswa kujifunza vitu.
 
Back
Top Bottom