Mgoda simtwange
Senior Member
- Sep 7, 2012
- 168
- 64
Unapata safari ya kikazi wiki 2 nje ya mkoa, Kabla ya kuondoka Unamuachia mkeo hela ya matumiz ya familia ndani ya nyumba sh 400,000 (laki nne), halafu unampa sh 300,000 (laki 3) akalipe ada ya shule ya mtoto. Ada halipi, bali hela ya ada anapeleka kwenye vikoba bila kukujulisha. Ukimuuliza kama ada umelipa anajibu amelipa. Unaporudi toka safari unamwambia alete risiti aliyolipia ada anajifanya kuitafuta, kisha anasema haionekani imepotea. Unakwenda shuleni kufuatilia kama ada ya mtoto imelipwa unakuta haijalipwa. Ikitokea huyu ndio mke wako utamchukuliaje? utamfanya nini labda?