Mkemia Mkuu wa Serikali akutwa amekufa hotelini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,804
MKEMIA Mkuu wa Serikali, Ernest Mashimba amekutwa amekufa katika chumba
cha Hoteli ya Executive Lodge iliyo nje kidogo ya mji wa Lushoto mkoani hapa.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa ambazo pia zimethibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema, kifo hicho kilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye hoteli hiyo ya kitalii ambayo alifikia katika safari yake mjini hapa ya kuhudhuria mahafali ya Shule ya Sekondari ya Kifungilo.

Kwenye mahafali hayo, Mashimba alikuwa akitarajiwa kuwa msoma risala mkuu kwa niaba ya wazazi.

“Hatujajua ni muda gani hasa alikufa lakini inahofiwa ni usiku baada ya
kuingia chumbani kwake kulala. Hivi ninavyozungumza uchunguzi unafanywa
na madaktari pamoja na polisi ili kujua chanzo,” alisema Mjema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema taarifa rasmi juu ya tukio hilo itatolewa
baada ya kufanyika kwa uchunguzi, hasa ikizingatiwa kuwa kuna utata katika tukio zima.
Alisema kifo cha mkemia huyo kilibainika Jumamosi asubuhi baada

ya wahudumu wa hoteli hiyo kuingiwa na shaka kutokana na mkemia huyo kutumia muda mrefu chumbani . Wahudumu waliwasiliana na uongozi ambao uliamua
kufungua mlango wa chumba alicholala na kumkuta kitandani akiwa tayari
ameshakufa.

“Polisi walipokwenda walikuta amekufa muda mrefu sasa hatujajua ni saa
ngapi yalimkuta mauti na ni sababu gani,” alisema Mjema.

Uongozi wa shule hiyo ya Kifungilo uliifahamisha Mwananchi kuwa mgeni
rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meja
Jenerali Said Kalembo wakayti Mashimba alipangwa kusoma risala maalumu kwa
niaba ya wazazi wenye watoto shuleni hapo.

Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi huo ni kwamba sherehe za mahafali
zilianza kama kawaida na ilipofika zamu ya kusomwa risala ya wazazi,
iliwalazimu kumteua mzazi mwingine kuchukua nafasi yake.

Watu waliokuwepo kwenye mahafali hayo wameeleza kuwa wakati wa kuimba
nyimbo walitangaziwa juu ya kifo, tangazo ambalo lilisababisha wahitimu
kuishiwa nguvu kwa kuwa Mashimba ni baba wa mwanafunzi mwenzao.
 
RIP, lakini nina swali la kuuliza. Mbona kunachanzo kingine kilisema kuwa alifia bafuni?:confused2:
 
Back
Top Bottom