Mke wangu nimfanye kitu gani? Anatembea na mfanyakazi mwenzie


K

kayuguyugu

Member
Joined
Oct 30, 2013
Messages
29
Likes
24
Points
5
Age
40
K

kayuguyugu

Member
Joined Oct 30, 2013
29 24 5
Baada ya kuona kama mke wangu ameanza kuwa na katabia kabaya nilianza kumfatilia katika simu yake na kugundua kama kuna kijana anayefanya kazi pamoja anamsumbua sana.Nilikuta meseji nyingi sana za kutongozana na nikazikopi kwangu baadhi yake huku nasuburi nimuulize.

Niiliipomuuliza kuhusu huyo jamaa alisema hakuna kitu kibaya kati yao ni just rafiki kikazi lakini nilipombana sana kuhusu meseji wanazotumiana alijitetea kwamba jamaa amejaribu kumtaka kimapenzi kwa miaka mingi lakini alimkatalia.

Baada ya kuona nimeanza kumfatilia aliamua kufuta jina la jamaa katika tlf contacts yake na hapo ndipo na mimi nilianza kuweka spysoftware katika simu yake na kweli imenisaidia sana kupata kujua kama mke wangu yupo katika mahusiano na jamaa kila siku napata meseji zaidi ya 50 chats kwani hutumia chats sana kuliko kupigiana simu. Kila meseji anayotuma na kutumiwa mimi huzipata katika simu yangu tena alivyokua hana haya tunakua mara nyingi tuko wote barazani yuko busy na jamaa bila kujua kama na mimi napata copy ya meseji zao na mpaka sasa sijamuuliza lolote bado nafatilia nakusanya Data.

Juzi niliona meseji ambayo ndiyo iliyonidhihirisha kama mke wangu ameisha toa penzi kwa jamaa kwani nilipata meseji ya jamaa anamsifia sana mke wangu kwamba: you are so unique, huwa mwenye furaha nikiwa na wewe, you have nice body, huyo ni jamaa anamwagia sifa mke wangu na Bibie kwa upande wake anamwambia jamaa kwa mke wako hayuko hivyo? jibu la jamaa ni kwamba :-wewwe una vitu vizuri ambavyo mke wangu hana huku wana wanapeana kisses emojy.
Hapohapo jamaa akamuomba tena mchezo wa marudio mke wangu unaoaje kama ukinipa tena mchezo? Mke wangu anamwambia jamaa, dont worry we are going to program together.


Ndugu wanajamii wenzangu hayo ndiyo niliyoyaona au kuyapata katika upelelezi wangu mpaka sasa, lakini mimi na yeye tuko vizuri wala simuonyshi kama kuna kitu nafatilia ndio kwanza nimemzidishia mapenzi pia kumbuka pia tumejaliwa kupata watoto 2 twins, boy and girl 3.5yrs old na tunaishi Ughaibuni Ulaya Magharibi.

Je nijilipue vipi jamani maana ushahidi wote ninao mezani na tlf ya jamaa yake ninayo naomba nasaha na ushauri wenu wa busara kwani usiombe yakukute iauma sana.
 
Norshad

Norshad

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Messages
3,448
Likes
6,361
Points
280
Norshad

Norshad

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2013
3,448 6,361 280
nitaivunja-jpg.626052
AISEE HONGERA SANA.Nakupa hongera sababu una moyo wa kiuanaume, nahisi umefika muda wa kumruhusu huyo mwanamke aendelee na hamsini zake, labda tu uwe ni marioo ndio waweza ishi nae..kila la kheri ndugu
 
D

Dr Chew Ing Gum

Senior Member
Joined
Aug 7, 2017
Messages
134
Likes
173
Points
60
D

Dr Chew Ing Gum

Senior Member
Joined Aug 7, 2017
134 173 60
Pole mkuu, hii ngumu kumeza. Ila maamuzi unayo wewe mwenyewe, kusuka au kunyoa. Kama jamaa ameisha kula game, wewe hujui kama walitumia kinga (risk ya maradhi). Aanza na DNA za watoto, je ni wako? Halafu mwambie mkeo kama amekuchoka, basi kila mtu achukue hamsini zake. Mijitu mingine haitosheki na haina shukrani hata chembe. Asije akakuletea maradhi bure!
 
manumbu1

manumbu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2012
Messages
600
Likes
76
Points
45
manumbu1

manumbu1

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2012
600 76 45
Pole sana na usijaribu kumfanyia ubaya wowote kwani western Europe sio nchi ya kupiga mwanamke.
Ushauri kaa nae chini confront her usimwonyeshe ushahidi wowote baada ya hapo maamuzi utayapata kutokana majibu yale.
Pole sana bro.
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
8,424
Likes
13,552
Points
280
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
8,424 13,552 280
hongera kwa kuwa na moyo wa subira mkuu.
hapo pazito, duuuu!!!
kwa moyo huohuo subiri hadi watakapopanga apointment umkamate live, hapo mnaweza kuongea lugha moja.
 
mbere

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Messages
6,678
Likes
5,523
Points
280
mbere

mbere

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2015
6,678 5,523 280
Kwani ina shomboo hiyo mkuu? Kashapiga hajaacha shombo wee endeleza life tu
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
29,441
Likes
82,596
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
29,441 82,596 280
Mueleze kuwa unafahamu na utoe maamuzi yako. Ingawa watoto ni wadogo lakini ni kheri upate shared parental responsibilities, watoto wawe wanakuja kwako na unakaa nao sawa na wanavyokaa na mama yao. Hapo hamna ndoa mnadanganyana.
 
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
13,260
Likes
20,818
Points
280
Madame S

Madame S

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
13,260 20,818 280
Mungu apitishe mbali yasinitokee. Kwa maana kwa hakika sijui nitafanya maamuzi gani.

Ee Mungu ninusuru
Aaamyn!!

Kuna vitu vya kusoma tu na kupata experience lakini si va kuviwaza au kuona vinakutokea ni ngum kusema kipi kitafanyika
 
Cousin

Cousin

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Messages
12,206
Likes
35,440
Points
280
Cousin

Cousin

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2014
12,206 35,440 280
Mimi ushauri wangu ni huu;Ukitaka umalize tatizo bila shida deal na mwanaume.... chukua namba yake mtafute, au ikiwezekana kama humjui kwa sura jitahidi umjue bila kupanic wala kuharibu mambo.....tafuta siku ukutane naye sehemu kama atakubali,akizingua mtafute sehemu nyingine lakini usiende ofisini kwao....mueleze kila kitu unachokijua kuhusu uhusiano wake na mkeo ikiwemo chats muonyeshe...kama atakuwa muelewa ataacha mara moja kutoka na mkeo.

NB: Usijaribu kumtongoza au kutoka na mke wa jamaa kwa nia ya kulipiza kisasi utakuwa hujasolve bali umeongeza tatizo.
Asante.
 

Forum statistics

Threads 1,235,962
Members 474,920
Posts 29,241,835