Mke wangu nimfanye kitu gani? Anatembea na mfanyakazi mwenzie

Haya mambo haya!Hapo utakuta analiiia ukimwambia kuwa umejua.Sisi binadamu bwana yaani ni wa hivihivi.
 
Haya mambo haya!Hapo utakuta analiiia ukimwambia kuwa umejua.Sisi binadamu bwana yaani ni wa hivihivi.
 
Kimbia Kaka toka nduki Kimbia Kimbia....inaumiza Sana....isitoshe Umeona kwa macho sms..km s kUtaka kuuza software
 
Baada ya kuona kama mke wangu ameanza kuwa na katabia kabaya nilianza kumfatilia katika simu yake na kugundua kama kuna kijana anayefanya kazi pamoja anamsumbua sana.Nilikuta meseji nyingi sana za kutongozana na nikazikopi kwangu baadhi yake huku nasuburi nimuulize.

Niiliipomuuliza kuhusu huyo jamaa alisema hakuna kitu kibaya kati yao ni just rafiki kikazi lakini nilipombana sana kuhusu meseji wanazotumiana alijitetea kwamba jamaa amejaribu kumtaka kimapenzi kwa miaka mingi lakini alimkatalia.

Baada ya kuona nimeanza kumfatilia aliamua kufuta jina la jamaa katika tlf contacts yake na hapo ndipo na mimi nilianza kuweka spysoftware katika simu yake na kweli imenisaidia sana kupata kujua kama mke wangu yupo katika mahusiano na jamaa kila siku napata meseji zaidi ya 50 chats kwani hutumia chats sana kuliko kupigiana simu. Kila meseji anayotuma na kutumiwa mimi huzipata katika simu yangu tena alivyokua hana haya tunakua mara nyingi tuko wote barazani yuko busy na jamaa bila kujua kama na mimi napata copy ya meseji zao na mpaka sasa sijamuuliza lolote bado nafatilia nakusanya Data.

Juzi niliona meseji ambayo ndiyo iliyonidhihirisha kama mke wangu ameisha toa penzi kwa jamaa kwani nilipata meseji ya jamaa anamsifia sana mke wangu kwamba: you are so unique, huwa mwenye furaha nikiwa na wewe, you have nice body, huyo ni jamaa anamwagia sifa mke wangu na Bibie kwa upande wake anamwambia jamaa kwa mke wako hayuko hivyo? jibu la jamaa ni kwamba :-wewwe una vitu vizuri ambavyo mke wangu hana huku wana wanapeana kisses emojy.
Hapohapo jamaa akamuomba tena mchezo wa marudio mke wangu unaoaje kama ukinipa tena mchezo? Mke wangu anamwambia jamaa, dont worry we are going to program together.


Ndugu wanajamii wenzangu hayo ndiyo niliyoyaona au kuyapata katika upelelezi wangu mpaka sasa, lakini mimi na yeye tuko vizuri wala simuonyshi kama kuna kitu nafatilia ndio kwanza nimemzidishia mapenzi pia kumbuka pia tumejaliwa kupata watoto 2 twins, boy and girl 3.5yrs old na tunaishi Ughaibuni Ulaya Magharibi.

Je nijilipue vipi jamani maana ushahidi wote ninao mezani na tlf ya jamaa yake ninayo naomba nasaha na ushauri wenu wa busara kwani usiombe yakukute iauma sana.
Una moyo wa paka mkuu, hongera sana kupita kiasi, hali hiyo bado unajiuliza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom