Mke wangu kanunua kiwanja bila kunishirikisha na anataka kuanza kujenga

Habar
Wanajamvi, maneno yafuatayo nimetamkiwa na Mke wangu usiku wa Leo,

"Nimenunua Kiwanja,na nataka kuanza ujenzi,ukiona inafaa waweza kunishauri"
Haya yananasemwa ikumbukwe sisi wenyewe hatuna nyumba ya kuishi ,

swali : ni vzur yeye aanze ujenzi wa kwake wakati hatuna pa kuishi na tuna watoto 2? Kwann anunue Kiwanja bila kunishirikisha? Naomba ushauri wenu tafadhari
Kama umeshajua shirikiana naye mkajenge tu acha maneno
 
Ndo hapo ukute ni mama ntilie alafu kanunua kiwanja cha ml 20. Shtuka poyoyo Unaibiwa by rayvanny
 
Umeangalia kwenye mauziano ametumia jina gani? Usianze kulalamika bila kuwa na uhakika. Je kama ametumia Sr name yako wewe kama mme wake si unajua ni nyumba yenu? Kama amenunua kwa jina ambalo hulitambui basi njoo ulalamike. Tuna mifano mingi ya wanaume wasiowaza kujenga unakuta wanawake ndo wanahangaika halafu wakishaingia mme anakoroma na mara cheche wengine wamelazimishwa kuondoka nyumba walizojenga wenyewe kwa kupika vitumbua. Check karatasi ya mauzo ndo utuletee mrejesho.
 
Hiyo yote inadepend kama anafanya kazi na anapata kipato chake sijaona kama kuna shida iko poa tu ulitakiwa umpongeze na ummpe moyo aendelee na ujenzi ikiwezekana umsupport tena kitu kizuri alichofanya amekueleza ni jambo jema lakini kama hana kipato kinachoeleweka kuweza kununua kiwanja hapo ndio unaweza kuuliza maswali na kuwa na mashaka
 
hapo jiongeze mkuu, changamka agiza tofali, nunua cement mpandishe mjengo, mkeo kafanya maarifa
Kifuatacho ataanza kurudi saa7 usiku akimuuliza atamwabia akimuuliza atamwambia usiniulize ulize nipo kwangu,jamaa akisema upo kwako wakati nyumba nilijenga mimi atamwabia ichukue niachie kiwanja changu sikukwambia ujenge nilikwambia unishauri...karne wanawake siyo kabisa yani ni pasua kichwa bora ahangaike anunue kiwanja ajenge mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
yaani mkuu wewe ni suruali tupu, na ushaambiwa unachoweza kufanya ni kushauri tu, tena hata huo ushauri atauchuja, yaani mkeo kakuzidi utafutaji mpaka akili, jiongeze. Asante
 
Itakua kuna sehemu unakosea, angeamua kukuficha hata asingekuambia chochote hadi anamaliza ujenzi.

Inaelekea wewe ni wale waume jina hamueleweki starehe zimewazidi familia hamuhudumii halafu mkija humu mnawaponda wanawake.
 
Habar
Wanajamvi, maneno yafuatayo nimetamkiwa na Mke wangu usiku wa Leo,

"Nimenunua Kiwanja,na nataka kuanza ujenzi,ukiona inafaa waweza kunishauri"
Haya yananasemwa ikumbukwe sisi wenyewe hatuna nyumba ya kuishi ,

swali : ni vzur yeye aanze ujenzi wa kwake wakati hatuna pa kuishi na tuna watoto 2? Kwann anunue Kiwanja bila kunishirikisha? Naomba ushauri wenu tafadhari

-mnahusianaje kwenye maamuzi mengine yaki maisha yanayohusiana na fedha, mali uwekezaji na matumizi, mmekua na mpango wa kujenga na utekelezaji ukoje? maana kwa mazingira hayo inaonesha tatizo unalotakiwa kutatua ni mahusiano yenu na sio la kununua uwanja, ilo la uwanja ni matokeo tu ya kubomoka kwa maisha yenu yakimaisha. na hata ukitatua tatizo hilo la uwanja, yatakuja mengine maana root of the problem is the relationship.

otherwise, kwa watanzania wengi kununua uwanja ni process yani mtu anajikusanya haswa esp wakati huu ubanaji matukizi.haiji tu kama sentensi yako apo juu.. so inastahili pongezi bila kujali changamoto iliyokuja nayo.
 
eti ukiona inafaa waweza kunishairi.. shenzi! umepigwa knock out baba.. kichwani hadi kwenye maneno! nakupa pia pole mkuu..
 
Lazima wewe utakua na shida sio bure,amekaa miaka mingi kaona ajiongeze tu wewe hadi watoto mmefikisha wawili hujawahi kuwaza kununua hata kiwanja unategemea afanyaje?
 
Anza kuishi kama anavyoishi yeye,... Akikuuliza imekuaje, nawe Muulize unaonaje?....
 
Ameona huna dira, kutwa unakunywa unasema umenunua mbili tuu, kaamua kufanya yake. Sasa km unaweza jitazame na ujitafakali upya saidia ujenzi.Kama huwezi subiri ukaribishwe ndani ya house baby
 
Back
Top Bottom