Mke wangu kaning'ata usoni nimfanyeje?

Mke wangu kaning'ata usoni nimfanyeje?

Ndenji five

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
1,985
Reaction score
3,120
Mi ndio yule kijana wa hovyo

Ipo hivi tumetulia zetu kibalazani tunacheki TV baada ya mlo wa usiku, mara meseji titiip kwenye simu ya wife uzuri tulikuwa tumekaa jirani akachukua simu na kusoma ile kupiga jicho nakuta wife kaikimbiza.

Akajua sijamuona nikamwambia, tusome wote, akajibu, we zinakuhusu nini, halafu mbele ya watoto nikasema sawa, ila sio kwa ubaya au ni mchepuko, akanijibu kwa kejeli, mi ooh kumbe unataka kunipanda kichwani.

Nikazima tv na kuwaambia watoto mkalale, nikachukua simu nikaenda chumbani, bas akaja chumban na kuanza kuongea ooh ujue wewe unanifuatilia sana, nikamshika kwa jazba, nikamwambia angalia kauli zako, dah ni kama moto umetiwa petroli.

Akaja akanitia meno kwenye jicho kwa juu, ghafla damu, kibao kwenye kitanda, basi nikabaki kumuangalia coz sikuwa na cha kumfanya punde wakaja majiran, wakanicheki nimelowa dam, ajabu wife anasema nilikuwa najihami, wakati hata sijamfanya chochote wakuu nipo naugulia maumivu, hivi mtu kama huyu nimfanye nini?
 
Huwa natamani wa kwangu afanye hivi hata siku moja lakini sijabahatika kabisa. Kila wakati nikilianzisha ananikwepa. Nadhani siku atakayojaribu breki ya kwanza itakuwa kwa dentist kufunga dental braces ili kukaza meno.​
 
Mkuu mpaka anakungata kwenye jicho Kwa juu ulikua unamwangalia Tu ?

Kuongezea tengeneza mazingira yakuheshimian na Mke wako Mkuu kuna kitu hakipo sawa
hii nimeipenda, huyo mwanamke anamchukulia huyu mwanaume ni dhaifu, kacheza faulo ya kwanza simu ya mchepuko, anaulizwa anang'ata jicho, makosa mawili na bado mume anakimbilia JF kuuliza afanye nini...khaa
 
Mkuu mpaka anakungata kwenye jicho Kwa juu ulikua unamwangalia Tu ?

Kuongezea tengeneza mazingira yakuheshimian na Mke wako Mkuu kuna kitu hakipo sawa
sizan kama nimemkosea mpaka kufikia huko ila dah ngoja kwanza nipone japo kaomba msamaha nimemjibu sawa ila roho inakataa kumsamehe kwanza kanikosea pili katoka nje kani dhalilisha yakuwa nampiga kila siku huku akilia wakati si kweli meno yake sio shida, shida kutoa nje mambo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom